Mzee Kinana ataja ugumu vijana kupenya uongozi, ataka wapewe nafasi

Mzee Kinana ataja ugumu vijana kupenya uongozi, ataka wapewe nafasi

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
kinana-pic2-data.jpg
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Abdulrahmani Kinana amewataka vijana na wanawake kujitokeza kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama hicho.

Amesema makundi hayo mawili yanapojitokeza kugombea yapewe nafasi huku akieleza ugumu uliopo kwa vijana kupenya kwenye uongozi ndani ya chama hicho.

Kinana amesema hayo leo Jumapili Aprili 10, 2022 katika hafla ya kupokewa na chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam inayofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Amesema kuwa wakati Chama hicho kinapoelekea kwenye uchaguzi wa ndani wana CCM wajitokeze kwa kuwa kila mwanachama ana haki ya kugombea.

“Nichukue nafasi hii kuwahimiza makundi mawili makubwa, kundi la kwanza vijana, gombeeni nafasi kwenye chama na inapowezekana wapeni nafasi kwa sababu wakati mwingine nayo kupenya inakuwa vigumu kwa vijana, kweli si kweli?”

“Kundi la pili akinamama tunataka kuona akinamama wengi kwenye nafasi za uongozi kwenye nchi yetu, jitokezeni tutawapeni nafasi za ushindi,” amesema.

Kinana amesema baada ya kuchaguliwa kushika nafasi hiyo ya Makamu Mwenyekiti atafanya kazi kwa nguvu na uadilifu.

“Nataka niwahakikishie kuwa nitafanya kazi kwa nguvu, kwa bidii, uadilifu na nikitanguliza utumishi na sio utukufu,” ameahidi Kinana ambaye ashawahi kuwa Katibu Mkuu wa chama hicho.

Amewasihi viongozi wengine wa chama kufanya kazi kwa bidii na kuacha kujitukuza

“Niwaombe viongozi wenzangu, kuchaguliwa na kupewa nafasi ya uongozi ni utumishi wa umma, ukifanya kazi vizuri watakutukuza, usijitukuze mwenyewe.''

Makamu huyo wa CCM amesema baada ya kuzoea majukumu ya nafasi hiyo ataanza ziara katika mikoa minne na baada ya kumaliza ziara hiyo atafanya nyingine kwenye mikoa saba.

“Baada ya kukaa ofisini na kuizoea umakamu mwenyekiti, nitafanya ziara Pwani, Tanga, Kilimanjaro na Arusha. Baada ya kumaliza mikoa hii minne, nitaanza ziara ya mikoa saba kwa mpigo. Lazima chama chetu kiwe imara na tusipokuwa na chama imara Taifa letu litayumba,” amesema


Chanzo: Mwananchi
 
Ccm ianze kujenga vijana imara kwa ajili ya CCM ya miaka 50 ijayo
 
Hata kabla alikuwa hapo hapo na alizunguka nchi karibu yote huwa hakuna jipya zaidi ya kutengeneza mazingira ya kula, japo now ni kula Asali.
 
Safi sana,hayo ndio tunataka kusikia,hongera Kinana.
 
Back
Top Bottom