Mzee Kingunge alisema CCM imekata Pumzi, kwa sasa inapumulia mashine?

Mzee Kingunge alisema CCM imekata Pumzi, kwa sasa inapumulia mashine?

Ni ajabu Sana mtu anayetuhumiwa kukatisha uhai wa watu CCM ndiyo imempa madaraka.

Hazina yetu kakabidhiwa fisadi mwenye mapesa chekwa yasiyo na maelezo kayapataje.

CCM Kuna ufisadi wa kimfumo.
surely gentleman,
yaan chama cha siasa kiendeshwe na vibaka kwa utapeli wa matone ya pesa za maskini wa Tanzania kwa kuwarubuni kidigitali?🤣
 
CCM ni imani na imani haina ubaya......

Mizizi ya IMANI ya CCM ni mitakatifu mno..... UTAKATIFU wake umejichimbia mbali sana kule ambako kila uchao kunanadiwa UTULIVU ,AMANI NA USALAMA wa watanzania.....

#Amka na ufungue macho yako!
Imani ya kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake? Nyie majambazi!
 
Matendo yapi ?!!

Matendo makuu ni kuwafanya watanzania waishi kwa UTULIVU ,AMANI NA USALAMA....

Lini hapa umewahi kuyaona ya Somalia ,DRC na Sudan?!!
Afrika nzima yanatokea ya somalia, Sudan na DRC?

Yaani wewe upande wa maisha unaouona wewe ni vita tu?
 
surely gentleman,
yaan chama cha siasa kiendeshwe na vibaka kwa utapeli wa matone ya pesa za maskini wa Tanzania kwa kuwarubuni kidigitali?🤣
Wale walioiba zile trilioni 1.5 zama za Magufuli na zile nyingine trilioni 1.8 walitumia dijitali gani kuiba?

Au mnadhani tumeshasahau jinsi mlivyokwapua zile bilioni 365 za Tegeta Escrow na kusema eti si fedha za umma?
 
Ni ajabu Sana mtu anayetuhumiwa kukatisha uhai wa watu CCM ndiyo imempa madaraka.

Hazina yetu kakabidhiwa fisadi mwenye mapesa chekwa yasiyo na maelezo kayapataje.

CCM Kuna ufisadi wa kimfumo.
Tuhuma koko na za uongo hizo....hakuna kiongozi anayekatisha uhai wa mtu kwa uonevu ....

#Amka hapo ulipolala
 
CCM hatutoki madarakani leo wala kesho. Halafu tutoke kwa sababu ipi?

Kwa waleo mnaoota kwa sisi ccm kuachia madaraka, niwaambie hivi: tafuteni mashamba huko msomera, kibaoni etc makalime.

Mama ni gwiji la maendeleo si sgr, stigila goji, daraja la kigogo - busisi, shule, zahanati zimejengwa kila mkoa, barabara za lami hadi vijijini, maji kila kijiji, wilaya, miji. Na umeme ndiyo usiseme mpaka unamwagika.
 
Afrika nzima yanatokea ya somalia, Sudan na DRC?

Yaani wewe upande wa maisha unaouona wewe ni vita tu?
Ndio maisha yanaanza kwa uwepo ama kutokuwepo VITA....

Katika vita hakuna maendeleo , utulivu wala umoja wa "kifamilia" wacha umoja wa wananchi....
 
Ndio maisha yanaanza kwa uwepo ama kutokuwepo VITA....

Katika vita hakuna maendeleo , utulivu wala umoja wa "kifamilia" wacha umoja wa wananchi....
Hapa Sasa maendeleo yake tofauti na DRC ni yapi. Au hujui bandari yetu inategemea mizigo toka DRC?
 
Hapa Sasa maendeleo yake tofauti na DRC ni yapi. Au hujui bandari yetu inategemea mizigo toka DRC?
...kabla ya uwekezaji wa DP WORLD nchi yetu ilikuwa inapata TRILIONI 1 kwa mwaka kwa ule uwekezaji wa TICTS...na mizigo ya DRC ilikuwemo pia....

Leo mwarabu amejicommit TRILIONI 26 kwa mwaka...

Endelea kuombea kuchangamke pale "KASTAM"....
 
Ni matone mangapi ya damu za watanzania yatamwagwa ili CCM itoke madarakani?

Ni matone mangapi ya jasho la watanzania yatamwagika ili CCM itambue ukatili na unyonyaji wanayofanya kwa watanzania?

Ni matone mangapi ya machozi ya watanzania yamwagike ili CCM Ione aibu kuiba kura na kutumia udhalimu na utesaji wakati wa chaguzi ?

Tone tone la Kila Nia njema ya watanzania kuchangishana ni manukato mbele ya kiti cha enzi cha Mungu.
Hakuna tone la damu litamwagika. CCM kila uchaguzi inashinda kihalali na mwaka huu itashinda kihalali ila kama watajitokeza vibaka kama wewe and your team kuharibu uchaguzi mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za TZ.
 
Mwaka 2015 Hayati Kingunge Ngombale Mwiru au Komredi kama Mwalimu alivyopenda kumwita, alisema hadharani kuwa CCM imekata Pumzi.

Leo miaka kumi baadae inaonekana kabisa kumbe CCM ilipokata pumzi mwaka 2015, haikuzinduka na kumbe maisha yake yanategemea kupumulia mashine.

Kumbe woga wa CCM kwa uchaguzi huru ni kwa kuwa yenyewe Iko mahututi haijiwezi.

Pumzika kwa amani msemakweli Mzee Kingunge.
Ghafla akakata yeye pumzi tuchunge ndimi zetu!
 
Hakuna tone la damu litamwagika. CCM kila uchaguzi inashinda kihalali na mwaka huu itashinda kihalali ila kama watajitokeza vibaka kama wewe and your team kuharibu uchaguzi mtashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za TZ.
Kwa CCM watanzania wanaouawa ni sawa na mbuzi tu wanavyochinjwa pale vingunguti. Damu ya watanzania haijawahi kuwa na thamani kwa CCM.
 
Kwa CCM watanzania wanaouawa ni sawa na mbuzi tu wanavyochinjwa pale vingunguti. Damu ya watanzania haijawahi kuwa na thamani kwa CCM.
Huo ni uongo wa wazi au huna exposure ya sehemu zenye machafuko na watu wanauwawa. Nenda Goma, Somalia, Gaza, na Sudan ili ukapate exposure then urudi hapa TZ kisiwa cha amani. Na kwasasa nipo baa nakunywa kwa starehe zangu!!
 
Huko kote ulikokutaja Kuna vita vilivyoanzishwa na waliokuwa madarakani kutokujali maslahi ya wengi kama wafanyavyo CCM hapa Tanzania.

Halafu umesema upo Bar, basi inawezekana unaandika mambo ukiwa umelewa.
 
CCM ni genge la kigaidi linalotumia mabavu ya vyombo vya dola kuendeleza utawala wao wa kidhalimu.
 
Huko kote ulikokutaja Kuna vita vilivyoanzishwa na waliokuwa madarakani kutokujali maslahi ya wengi kama wafanyavyo CCM hapa Tanzania.

Halafu umesema upo Bar, basi inawezekana unaandika mambo ukiwa umelewa.
Ngoja tule raha muda wa kuishi ni mfupi sana wewe endelea na stress zako na Saccos yako ya CDM ila kuongoza TZ bado sana labda mwaka 2100 mkijitahidi sana na kusiwe na chama kingine cha upinzani. Nyerere alishasema upinzani wa kweli utatoka ndani ya CCM
 
Back
Top Bottom