Mzee Makamba anasema 2025 hakuna mjadala Rais Samia Suluhu atagombea urais tena. "Uchaguzi umekwisha sasa tunajiandaa na ligi ya 2025, na tunashinda kwa sababu wapinzani wetu ajenda zao ni mbili tu Katiba na Tume ya uchaguzi tu, kule kwetu Bumbuli hawashibi katika, wala mama yangu ukimuuliza kuna tume ya uchaguzi anakuuliza ni nini?"
Lakini pia amesema "Kama mnataka mumchague mtu lazima mumsifu ili watu wajue kwamba ana sifa, kwahiyo hata wale wanaopinga tukisema umeupiga mwingi ni nahau, nina shemeji yangu pale ana tatizo na kuupiga mwingi, kuupiga mwingi maana yake ni mtu aliyefanya kazi nyingi na kubwa"