#COVID19 Mzee Makamba: Askofu Gwajima na Polepole hawavumiliki. Lazima wajue uhuru wao unaishia Bungeni

Huyu mzee naye anazeeka vibaya sana, kwa katiba ya nchi hii ilivyo, na wananchi wake walivyopiga usingizi wa Pono kuna mtu anaweza kumdharau Rais? Akiamua kumfinya mtu si anamfinya mara moja tu!! Hawa wazee wana umuhimu wao, ila kwa sasa wapumzike kwanza, TZ ya miaka ya 90s aliyoizoea yeye siyo TZ ya sasa!! Hao akina Polepole waachwe waongee, mwisho wa siku wenyewe watachoka na maisha yataendelea!! BTW, kila siku yanaibuka mambo mapya, ukizuia watu kuongelea chanjo leo kesho wataibuka watu wataongelea tozo, makato ya Luku, Ugaidi wa Mwamba, Katiba mpya, mikutano ya hadhara, dini kusajiliwa, teuzi mbovu n.k.! ukisema ujibu na kuyaweka moyoni hayo yote si utakufa na pressure kama mwendazake?? Acha watu waongee..
 
Wapeni KESI ya UGAIDI ndio MILA ZENU

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Kwaniniwachukuliwe hatua?!?! Serikalini imeshasema chanjo ni hiari Sasa tatizo liko wapi? Kama Kuna viongozi wanahamasisha chanjo ili watu wachanjwe Kuna ubaya gani Kama Kuna kundi la watu litasema chanjo ni hatari na kutoa sababu? Binafsi naipenda serikali lakini kwa hili la chanjo serikali imejichanganya mno...Kama Corona ipo na chanjo ipo kulikuwa hakuna sababu ya kusema chanjo ni hiari...je chanjo ya ndui ilikuwa ni hiari?! Je kwa chanjo zote zilizopita zilikuwa ni hiari kwa mtu kuchanjwa?
 
How come kukataa kuchanjwa mwili wangu iwe ni dharau kwa mwingine?!
Tatizo sio kukataa kuchanja ila tatizo ni wewe kukataa kuchanja halafu unaanza kudanganya na wananchi wasichanje hapo ndipo shida ilipo.
 
Mimi ninachojua chanjo ni hiari. Anayetetea kuchanja ana haki sawa na anayekataza watu wasichanje.

Hivyo, wote wapo sawa, wote haki zao ni sawa.
Hakuna anayesema chanjo ni lazima ila unapowalazimisha waumini wako waigomee unaondoa uhiari wa chanjo, unatakiwa uwaache waumini wako wajiamulie wenyewe bila kuwakataza.
 
Tatizo sio kukataa kuchanja ila tatizo ni wewe kukataa kuchanja halafu unaanza kudanganya na wananchi wasichanje hapo ndipo shida ilipo.
Kama kuna wanaohamasisha tuchanjwe lazima wawepo na wanaohamasisha tusichanje halafu sasa sie tuchague upande. It's natural. Mawazo kinzani hayapigwi rungu. Imagine kuna makanisa yanampinga Mungu na Yesu hata Muhammad, why chanjo isipingwe?!
Watanzania wana akili ya kuchagua upande sahihi.
 
Tuliona hivi hivi kwa Mzee Mwinyi alipokuwa anataka mwanae awe rais mzanzibari, mzee wa watu alijikomba komba sana kwa Magufuli.
 
Mzee Makamba anasema baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakimdharau sana Rais samia hivyo ametaka washughulikiwe mara moja.
Sukuma GANG/ MATAGA hawataki kutawaliwa na mwanamke tena ni mzanzibar na ni muislamu.. wanamtazama Samia wanasema Hiiiiiii!!!!… 😄😄😄
 
Kuna haja ya kutenganisha kofia mbili
 
Mimi ninachojua chanjo ni hiari. Anayetetea kuchanja ana haki sawa na anayekataza watu wasichanje.

Hivyo, wote wapo sawa, wote haki zao ni sawa.
Sawa ni hiari lakini usitumie nafasi yako katika jamii kushawishi wengine wasichanje
 

..Tatizo la Askofu Gwajima ni madai yake kwamba viongozi wamehongwa, wamechomwa feki, na chanjo zina magnetic force / chip.

..Kama Askofu angepinga chanjo kwa hoja kwamba hazijafanyiwa majaribio ya kutosha kujua ubora, na madhara yake, hakuna ambaye angemlaumu.

..Askofu Gwajima angekuwa ni mwana Chadema na akatoa tuhuma alizotoa kuhusu chanjo leo angekuwa mahakamani akijibu mashtaka mabaya dhidi yake.
 
Kama kuna jinai apambane na jinai yake. Ila drama za chanjo waachane nazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…