#COVID19 Mzee Makamba: Askofu Gwajima na Polepole hawavumiliki. Lazima wajue uhuru wao unaishia Bungeni

Namheshimu sana Mzee Makamba ila nimwambie tu kuwa huku Kudharauliwa na Kujaribiwa kwa Mwenyekiti wetu CCM Taifa na Rais Samia Suluhu Hassan ametaka mwenyewe.

Tulimuonya na alionywa sana tu tena hapa hapa JamiiForums kuwa kuna baadhi ya Watu kama akina Dotto, Mwigulu, Bashiru, Polepole, Diwani, Ummy, Jenister na Kheri James akatupuuza na kuendelea Kuwakumbatia na wengine hadi Kuwateua.

Mama Samia kayataka haya Mwenyewe.
 
Kasahau utovu wa nidhamu alioufanya yeye na mwanawe kwa mwenda zake, naona hapa ameanza kujikomba kwa mama ili amkumbuke mtoto wake, Mzee makamba hana tofauti na Steve Nyerere.
 
Makamba na mwanawe ni wanafiki sana.
 
Hata kama wanakosea, bado wana uhuru wa maoni. Na kama raia wengine, uhuru wao siyo bungeni tu.
 
Wewe mzee ndio hauvumiliki unataka kuigeuza tanzania ncji ya ukoo wako
 
Hashtag GWAJIMA AFUKUZWE CCM ..
 

Uhiari wa hii chanjo uendelee kuheshimiwa. Maisha ya mtu sio mali ya chama. Kwa CCM kuweka msimamo kusichukuliwe kumaanisha kwamba mwanachama mmoja mmoja wa CCM haruhusiwi kuwa na msimamo unaotofautiana na wa chama chake hata kama hakisemei chama.

Mimi sijamsika Gwajima au Polepole akikisemea chama chake. Juhudi zozote za kuwanyamazisha ni juhudi za kukiuka dhana ya uhiari wa hii chanjo. Hata kama wanapinga hii chanjo hadharani waachwe wafanye hivyo, kwasababu hata wanaoiunga mkono nao wanafanya hivyo hadharani.

Lectures zote zinazotolewa na pro-vaccine crusaders na anti-vaccine crusaders zinaangukia kwenye “akili za kuambiwa” ambazo Watanzania watachanganya na za kwao na kuamua, kila mtu kivyake vyake, whether achanje au asichanje. Hiari iachwe itamalaki.
 
Wee Mzee Makamba Umeshajichokea.Waache Vijana Hawa akina GwajiBoy na polepole wawe huru kutoa Maoni yao.Zama zakusema zidumu fikra za Mwenyekiti zimezeeka Kama nyie mlivyozeeka.Mawazo na matisho Kama ya kwako Sio ya Zama hizi za ki-Digital.Wee Mzee vipi Wewe.
 
Mimi ninachojua chanjo ni hiari. Anayetetea kuchanja ana haki sawa na anayekataza watu wasichanje.

Hivyo, wote wapo sawa, wote haki zao ni sawa.
Unavyosema wewe tukiwa na serikali yaivi kila mtu na jambo lake, hatuwezi kuendelea. Serikali kama serikali inatakiwa iwe na mmsimamo mmoja , na iwe nchi moja na iendelee. Kustawi kwa umoja.
 
Makamba na mwanawe ni wanafiki sana.
Mwana wa Yusufu ambae ni January, Watanzania wameanza kumwona kama exceptional toka 2014, baada ya kuanza kuonekana kama Presidential material na 2015 kwenye mchakato ndani ya CCM akapenya kwenye 5 bora.

Bila shaka huo upekee ipo siku aka-bounce back na kuibukia IKULU ya magogoni; wakati utatujuza; ila mwana akiwa mkulu, ni nani ataweza kumsaidia achague maneno ya kusema???
 
Serikali yenyewe imekosa msimamo kwa kusema eti chanjo ni hiari.
Maana yake mtu yuko huru kujiua na kuuwa wengine.

The HALLMARKS of bad governance:
1. Ambiguity
2. Arbitrariness
3. Capriciousness

Sent from my G80 using JamiiForums mobile app
 
Ni sawa tu zilivokuwa dharau za Kinana, Makamba Sr, Nape, J. Makamba kwa late Magu. Tena wao walifikia kumuita Rais mshamba. Bora hawa wa hoja mahsusi ya corona.
 
Unavyosema wewe tukiwa na serikali yaivi kila mtu na jambo lake, hatuwezi kuendelea. Serikali kama serikali inatakiwa iwe na mmsimamo mmoja , na iwe nchi moja na iendelee. Kustawi kwa umoja.
Wazo lako zuri, hivyo serikali inatakiwa iamue, kama kuchanja wote wachanje... Kama hamna kuchanja basi tusichanje.
 
Kuna hiyari ya kupokea au kukataa kupokea chanjo. Lakini nina shaka kama ni rukhsa kufanya kampeni ya kuipinga chanjo.
 
Nyerere alikua anawaita WANASIASA wenye Tabia za KIMALAYA ndio hawa mzee lakini bado unatabia za kimalaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…