#COVID19 Mzee Makamba: Askofu Gwajima na Polepole hawavumiliki. Lazima wajue uhuru wao unaishia Bungeni

Mzee Makamba anasema Askofu Gwajima na Polepole hawavumiliki ndani ya CCM kwakuwa wamekuwa wamekuwa wakipingana na Serikali hasa kwenye swala hili la chanjo.

Mzee Makamba anasema baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakimdharau sana Rais samia hivyo ametaka washughulikiwe mara moja.

Mzee Makamba anasema yeye si msemaji wa CCM lakini anashangaa ukimya wa baadhi ya Wana CCM na viongozi wa CCM hasa katika hali ya Rais kuonekana ana dharauliwa na baadhi ya wana CCM.

Mzee Makamba ametaka wana CCM kuwachukulia hatua Gwajima na Pole pole.. kwani hawavumiliki.

=====

BAADHI ya viongozi waandamizi ndani ya chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali, wanadaiwa kuwa na mkakati wa makusudi wa kumdharau Rais wa Taifa hilo, Samia Suluhu Hassan.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho, zinasema hatua ya viongozi wake wakuu, kunyamazia matendo ya Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima na mwenzake, Humphrey Polepole, inatafsiriwa ni dalili tosha kuwa “wanamdharau na kumpuuza,” Rais Samia.

Polepole, ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, pamoja na Askofu Gwajima, wamekuwa na kampeni ya wazi ya kupinga chanjo ya corona, kinyume na maelekezo ya chama chao.

Kutokana na hayo, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Mzee Yusuf Makamba, Naibu Katibu Mkuu Bara wa NCCR-Mageuzi, Anthony Komu na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Profesa Edward Hoseah wamezungunzia kadhia hiyo na hatari wanayoiona ndani ya serikali na CCM.

Undani wake, soma Gazeti la Raia Mwema toleo la leo Ijumaa tarehe 20 Agosti 2021.
Huyu Mzee chenga si ndo huyu alikuwa amamsimanga kumbagaza na kusemgenya jpm,

Alifanya vikao vya kumpindua mwenyekiti yeye na akina kinana na genge lao ovu tukambaini

tulipombaini kupitia ule mtambo wetu wa kudukua tulioununua israel akaja mbio kuomba msamaha
 
Baada ya kusahaulika, Makamba anafuata nyayo za Mzee Mwinyi, kujipendekeza chamani ili mwanawe January akumbukwe kwenye uraisi, simple like that.
 
Mzee Makamba anazeeka vibaya. Kutumia hiari iliyowekwa na kwenda kinyume na mitazamo ya mwenyekiti sio kosa. Huyu mzee na wenzie wanadhani bado tupo mwaka 1958 ambapo fikra za mwenyekiti zilipaswa kudumu milele
 
Kama ni hiari sasa wanampinga nini...
Mzee Makamba is right.
Hao kina polepole na gwajima wakiona chanjo haziwafai sasa wanabwabwaja nini hadharani?

Wajue kuongea kinyume na mama ni kumdharau hadharani.
 
Waandishi wa habari, waacheni wazee wapumzike..
 
Mzee Makamba anasema Askofu Gwajima na Polepole hawavumiliki ndani ya CCM kwakuwa wamekuwa wamekuwa wakipingana na Serikali hasa kwenye swala hili la chanjo.

Mzee Makamba anasema baadhi ya viongozi wa CCM wamekuwa wakimdharau sana Rais samia hivyo ametaka washughulikiwe mara moja.

Mzee Makamba anasema yeye si msemaji wa CCM lakini anashangaa ukimya wa baadhi ya Wana CCM na viongozi wa CCM hasa katika hali ya Rais kuonekana ana dharauliwa na baadhi ya wana CCM.

Mzee Makamba ametaka wana CCM kuwachukulia hatua Gwajima na Pole pole.. kwani hawavumiliki.

=====

BAADHI ya viongozi waandamizi ndani ya chama tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Serikali, wanadaiwa kuwa na mkakati wa makusudi wa kumdharau Rais wa Taifa hilo, Samia Suluhu Hassan.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho, zinasema hatua ya viongozi wake wakuu, kunyamazia matendo ya Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima na mwenzake, Humphrey Polepole, inatafsiriwa ni dalili tosha kuwa “wanamdharau na kumpuuza,” Rais Samia.

Polepole, ambaye ni mbunge wa kuteuliwa na Rais na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa, pamoja na Askofu Gwajima, wamekuwa na kampeni ya wazi ya kupinga chanjo ya corona, kinyume na maelekezo ya chama chao.

Kutokana na hayo, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Mzee Yusuf Makamba, Naibu Katibu Mkuu Bara wa NCCR-Mageuzi, Anthony Komu na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Profesa Edward Hoseah wamezungunzia kadhia hiyo na hatari wanayoiona ndani ya serikali na CCM.

Undani wake, soma Gazeti la Raia Mwema toleo la leo Ijumaa tarehe 20 Agosti 2021.
Yote hayo ni kutaka kuwanyamazisha viongozi waliyoaminika na magufuli wasiwe na sauti. Polepole ni mbunge tu kwa nini asiwe na uhuru wake kutoa maoni hata kama ni tofauti na viongozi wa chama. Rais kasema kuchanja au kutochanja ni hiari sasa kwanini iwe nongwa mtu akisema hachanji. Na huyo mzee makamba atoe unafiki wake. Enzi za comedy zake kufanikisha hila zake zimepita.
 
Mzee Makamba apumzike tu, ile ndoto yake ya kumuona mwanae february akiongoza JMT imeyeyuka ghafla amebaki kubwabwaja tu. 2025 nchi mikononi mwa wapinzani !!!
 
Back
Top Bottom