Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,611
Mzee Makamba anadai kuwa Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo. Na kwa tafsiri ya kiafrika mtu mwenye laana siku zote hufanana na mtu aliyechanganyikiwa. Ayafanyayo huwa kituko kwa wanaomzunguka, huwafanya watu waingiwe na huruma.
Lakini naamini lengo la Mzee Makamba kumsema Askofu Gwajima ni kumuongezea uadui miongoni mwa wanajamii kwa kuanzia na watu wanaosali kwake. Lengo jingine ni kumchongea kwa Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM.
Vyovyote iwavyo siuoni mwenendo mzuri katika siku zijazo kwa Askofu huyu. Ni hatari sana pale unapojaribu kujikomba kwa mtu mmoja kwa kumponda mwingine bila ya kuifahamu kwa undani wanapokuwa wamekaa pamoja wawili hao wanaongea vipi na wanaaminiana kwa kiasi gani.
Kiongozi mstaafu siku zote hapungukiwi ushawishi kwa aliyepo pale Magogoni. Askofu alipaswa kupima uzito wa kauli yake ili akwepe kufananishwa na mtu aliyelaaniwa.