Mzee Makamba: Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo

Ongeza na ya Samwel Sitta
 
M
Nini? Y. Makamba is a political lunatic. Aliwahi kumwambia Nape kafungiwa duniani hadi mbinguni!
 
Ni ajabu kwamba wanasiasa wakuja juu sana kulinda kitumbua chao cha SIASA kisiguswe na viongozi wa dini. Lakini wakati huo huo wanampigia makofi kiongozi mwenzao wa siasa anayetumia vitabu vya dini kutimiza malengo ya kisiasa. Na mbaya zaidi anafanya hivyo kwa kupotosha, tena kwa makusudi.

Makamba ametumia vibaya maandiko matakatifu juu ya kubatiza kwa maji na kubatiza kwa moto na huo ni upotoshaji wa makusudi au kukejeli kitabu cha Biblia Takatifu ambayo ameifanya bila kujali kama ataumiza hisia za waumini wanaotumia na kuiheshimu Biblia. Kwa kufanya hivyo, anashindwa hata kuwaheshimu Wakristo ambao ni wana CCM.
Iwapo mzee huyu ana uwezo wa kuona ubaya wa kufanya hivyo, na iwapo anaheshimu misingi ya kuheshimu imani za wengine, jambo la kwanza anapaswa kuwaomba radhi Wakristo, iwapo alifanya hivyo bila kukusudia. Jambo la pili ni kwamba, iwapo anataka kuendelea kuitumia biblia kwenye jukwaa kubwa namna hiyo kama afanyavyo, basi aende chuo cha Biblia, akafundishwe Biblia na wenye Biblia yao. Najua kila mtu anaweza kununua Biblia kama anavyoweza kununua novel, lakini Makamba haiamini Biblia, kwani kama angeiamini angebatizwa, kwa hiyo Biblia sio yake. Ni hatari sana kutumia kitabu cha imani ya watu wengine unavyotaka wewe. Sote tunajua Salman Rushdie alinunua Quran Tukufu kama vile kununua novel na akakitumia alivyotaka yeye, matokeo yake? Aliwaudhi wenye kitabu chao.

Naomba niishie hapa ili nisije nikaamsha hisia kali.
Makamba, kama unaamini Salman Rushdie alifanya kosa, iheshimu Biblia!
 
Hoja yangu ni JK kumpaisha huyo mzee pamoja nakusikia alichokisema,akatamba kabisa ndio faida ya kuwa na wazee wa chama as if Makamba aliongea vema sana!
JK alishangilia madongo, ilikuwa ni siku yake ya mwisho kama mwanasiasa mwenye dhamana fulani, rohoni mwake alikuwa huru sana kwani alikuwa anaachana rasmi na siasa akiwa mtu mwenye madaraka. Ndio maana akamrushia madongo FTS kwamba alikuwa waziri mkuu lakini sasa anagombea chaguzi za Kibaha na kina Kubenea.
JK aliamua kuwa mtu wa masikhara mengi kwani hakuwa na cha kupoteza kwa jioni ile.
 
ajibishane ili aaibike zaidi hahaha
 
Usipotoshe umma, Salman Rushdie ni muislam halisi, Rushdie ni utamkaji wa kizungu, jina lake ni Salman Rashidi.
Kabla hujaandika kitu jaribu kufanya japo kautafiti kadogo. Rushdie alipoamua kuukosoa uislam alikuwa akiandika mambo anayoyafahamu kwani amekuzwa katika dini hiyo.
Yusuf Makamba sio mtoto mdogo, mtoto wake January amezaliwa mwaka 1974. Anayo haki ya kutolea mifano vitabu vyote vya dini kama anao uelewa wa kile kinachoandikwa. Mbona waislam wengi tu wanaanzisha mihadhara maalum ya kuichambua Biblia?. Mbona wakristo wengi wanaisoma Quran tena wakiwa seminary wakati wakiwa kwenye harakati ya kuwa mapadre?. Huna sababu ya kuchukizwa na tabia ya Mzee Makamba kuchambua vitabu vyote vya dini, hakuna binadamu mwenye haki maliki ya vitabu hivi vitakatifu.
 
Jakaya Kikwete aliwabatiza kwa Maji ila Magufuli atawabatiza kwa Moto. Yusuph Rajabu Makamba July 23 2016 Dodoma.
Abomination!!! Na nitashangaa wakristo wakikaa kimya bila kupinga kauli za kudhalilisha ukristo.
 
Ubarikiwe mkuu, ni wakristo wapuuzi tu ambao hawataona kejeli ya ukristo inayofanywa na Mzee Makamba na kuangalia eti dhihaka ya Gwajima kwa Pengo (mpinga msimamo wa ukristo kuhusu kuchinja na katiba)
 
Mawazo yako si sahihi mkuu, kwanza unajaribu kutuaminisha kuwa ukubwa ni ufahamu. Pili, unaamini kitendo cha Makamba kuchambua kwa kulinganisha ukristo na uislam ni sahihi (siku za nyuma alisema YESU ni Nabii Issa). Tatu, mfano aliotumia unauunga mkono (kumlinganisha Magu na Mungu)

All in all Makamba's statement is sacrilegious
 
Yesu ni Nabii Issa, Nabii Issa ni Yesu, haya ni majina tu lakini sisi tunaojifanya tunaijua dini kuliko waliotuletea tunadai kuwa eti hawa ni watu wawili tofauti!!. Simaanishi kwamba ukubwa ni ufahamu, nachojaribu ni kuelewesha wengi kwamba mtu anaweza kutumia mifano ya kidini kwa nia ya kutaka kujenga hoja na sio zaidi ya hapo. Wale wapotoshaji ndio huenda mbali zaidi kwa kujaribu kujifanya wanaijua dini iliyokuja na watu waliokuwa kwenye majahazi kuliko wao wenyewe wanaovyoijua.
Kuna dhambi ya kujihesabia haki, hii ni dhambi ambayo hawa wanaojifanya wao wameokoka, huwa wanaitenda kila siku maishani mwao. Kujaribu kuyatafsiri maandiko bila hata ya kujua wale waliyoyaandika walikuwa na kusudio gani wakati wanayaandika.
Hoja ni ya kisiasa na hata hii thread nilipokuwa naaindika sikutegemea kwamba watu wanajifanya wanamjua zaidi Mungu kiasi cha kusahau maudhui halisi ya ujumbe.
 
Nawe pia nakuweka kundi moja la kutukana ukristo. YESU na Nabii Issa ni tofauti kabisaaaa mkuu. Huu ndiyo upuuzi wa kujifanya unajua kumbe hujui, na tabia hii hata baba yako Makamba anayo. Sacrilegious
 
Kwa hiyo unafurahia kuzikwa upinzani? Mbona katiba pendekezwa haijasema kuwe na mfumo wa chama kimoja? au namaanisha nini kusema upinzani
Kifo hakiepukiki hasa baada yakugeuza chama cha wapiganaji kuwa chama cha wapigaji
 
Gwajima nasikia kasema kwao huwa hawawajibu walevi
 
wamestaafu lakini wanakingia kifua watoto wao. kijana gani atakaye gombea uraoa baada ya Magu kung'atuka
 
Kama Gwajima alisema uongo, je na Bulembo alisema uongo pia, ebu nijibu hapo??
 
Mkuu wewe umeona mbali, jk alimuandaa makamba aseme vile, na Gwajima amejua kua yule katumwa ndio maana alimjibu Hana leseni ya kuendesha Bajaj na guta, ana leseni ya kuendesha magari makubwa makubwa, that means hataki kumjibu, kamdharau
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…