Mzee Makamba: Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo

Mzee Makamba: Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo

Shetani at unafiki mkubwa. Wakati akisema Gwajima ni hatari kwa Pengo, Mungu anajua ni namna gani haka kamzee na familia yake wlaivyo hatari kwa nchi ya Tanzania.

Ibilisi kuba.

Mzee Makamba anadai kuwa Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo. Na kwa tafsiri ya kiafrika mtu mwenye laana siku zote hufanana na mtu aliyechanganyikiwa. Ayafanyayo huwa kituko kwa wanaomzunguka, huwafanya watu waingiwe na huruma.

Lakini naamini lengo la Mzee Makamba kumsema Askofu Gwajima ni kumuongezea uadui miongoni mwa wanajamii kwa kuanzia na watu wanaosali kwake. Lengo jingine ni kumchongea kwa Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM.

Vyovyote iwavyo siuoni mwenendo mzuri katika siku zijazo kwa Askofu huyu. Ni hatari sana pale unapojaribu kujikomba kwa mtu mmoja kwa kumponda mwingine bila ya kuifahamu kwa undani wanapokuwa wamekaa pamoja wawili hao wanaongea vipi na wanaaminiana kwa kiasi gani.

Kiongozi mstaafu siku zote hapungukiwi ushawishi kwa aliyepo pale Magogoni. Askofu alipaswa kupima uzito wa kauli yake ili akwepe kufananishwa na mtu aliyelaaniwa.
 
Mwenyekiti wa CCM anayemaliza muda wake Jakaya Kikwete amesema CCM haikuvunjika mwaka jana basi haitakaa ivunjike tena, akidai mwaka jana ndio mafisi yalikaa ukumbini Dodoma yakisubiri mkono udondoke lakini haukudondoka
Na CCM itaendelea kuwepo sio kwa kutumia nguvu ila kwa sababu wanashughuikia matatizo ya watu na wanapanga sera nzuri

Kwa maneno ya m/kiti mstaafu Kikwete leo niamini ccm lazima isambaratike kwa macho ya wote muda si mrefu kama alivyonena askofu Kakobe kupitia waraka wake maalum mwaka jana kwa rais mstaafu J.Kikwete.

Mzee Makamba anadai kuwa Mchungaji Gwajima anayo laana ya kumtukana Kardinali Pengo. Na kwa tafsiri ya kiafrika mtu mwenye laana siku zote hufanana na mtu aliyechanganyikiwa. Ayafanyayo huwa kituko kwa wanaomzunguka, huwafanya watu waingiwe na huruma.

Lakini naamini lengo la Mzee Makamba kumsema Askofu Gwajima ni kumuongezea uadui miongoni mwa wanajamii kwa kuanzia na watu wanaosali kwake. Lengo jingine ni kumchongea kwa Mwenyekiti Mtarajiwa wa CCM.

Vyovyote iwavyo siuoni mwenendo mzuri katika siku zijazo kwa Askofu huyu. Ni hatari sana pale unapojaribu kujikomba kwa mtu mmoja kwa kumponda mwingine bila ya kuifahamu kwa undani wanapokuwa wamekaa pamoja wawili hao wanaongea vipi na wanaaminiana kwa kiasi gani.

Kiongozi mstaafu siku zote hapungukiwi ushawishi kwa aliyepo pale Magogoni. Askofu alipaswa kupima uzito wa kauli yake ili akwepe kufananishwa na mtu aliyelaaniwa.

Nilivyomtaza huyo Mzee jana na maandiko ya #Biblia yasemavyo Yeye ndiye aliyepatwa na laana ya dezo siyo askofu #Gwajima na watu wote wataona [emoji23]
 
Lowassa ni ngome iliyojengwa kwa zege na vyuma imara!!! Mpka ndan ya mkutano mkuu wa CCM wanashindwa kuongelea habar zao wanamzungumzia mmoja tu Lowassa???? Kwel pagumu hapa ndan ya CCM
 
Huyu mzee Makamba sijawah kumskia anaongea point za muhim tofauti na mipasho
 
Ukiwa kiongozi wa kitaifa katika siasa si vizuri kuongelea mambo ya kidhanifu yaa idealism kwa kujenga hoja mahali pasipohusika. Haya yana sehemu zake. tunataka atuambie ukiweka mbolea shambani mazao yanaongezeka au ukikikata miti unasababisha ukame si atuambie mambo ya chuma ulete! Hayo ya idealism tutayapata kwa watu wake!
 
Jakaya Kikwete aliwabatiza kwa Maji ila Magufuli atawabatiza kwa Moto. Yusuph Rajabu Makamba July 23 2016 Dodoma.
Kwahiyo huyo wa zamani hastahili hata KUFUNGA kamba za viatu vya huyu mpya.Haya maandiko yana maana iliyo KUU ZAIDI sijui kama huyu mzee aliyeongea alitafakari hilo.Yaleyale ya kichuguu na mlima Kilimanjaro.
 
Huku kwetu Mkuranga hakuna barabara umeme maji dawa na shule za maana

Inna lillahi wa Inna Illayhi Rajiun
 
Huku kwetu Mkuranga hakuna barabara umeme maji dawa na shule za maana

Inna lillahi wa Inna Illayhi Rajiun
Mkuranga sehemu gani wewe usie na shukrani upo,sotele au mpafu?
Katika wilaya iliopendelewa ni mkuranga,baada ya kumegwa kutoka wilaya kongwe ya kisarawe,unataka kudanganya nini hapo umeshashiba mihogo ya nazi na ng'onda toka kisiju
 
Hahahaha
 
Makamba jana kuna sehemu aliangusha sana , eti Magufuli alikataa kimemo chake ili mwanae ateuliwe ukuu wa wilaya
Inaonyesha hio ndio tabia yake ata January nae aliteuliwa kwa style hio hio
 
Hili zee linalinda ulaji qa matoto yake .ndio maana linaropoka ropoka .
 
Naona viongozi wa dini nao watambue wajibu wao kanisani au msikitini sio jukwaa la siasa wasituchanganye wanakondoo!
 
Makamba ana laana ya watu wa tarime ipo siku anaweza akajikuta anatembea uchi
 
Back
Top Bottom