Mzee Malecela, Mzee Warioba, Dk. Salim, Mzee Msuya, Mzee Butiku mko wapi majadala wa kitaifa kuhusu Bandari?

Stuka

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
282
Reaction score
906
NCHI Yetu bado ina hazina na viongozi wastaafu, Mzee Samwel John Malecela, Mzee Joseph Sinde Warioba, Mzee David Cleopa Msuya, Dk. Salim Ahmed Salim, Mzee Joseph Butiku mbona mko kimya mjadala unaohusu kuuzwa kwa bandari?

Tunawaomba na ninyi kama wazee wetu mtoe neno kuhusu mkataba huu.



Mzee Msuya



Mzee Malecela


Mzee Warioba



Dk. Salim



Mzee Butiku
 
Hakuna mzee mnafiki kama Butiku! Wakati wa Mwendazake alikuwa anasafiri katiba ibadilishwe ili Magu awe Rais wa milele. Mzee hana maana kabisaa!
 
Mzee marechela na Mzee salim una hakika wana uwezo wa kiakili kujadili ? ,Huyu salim kuna siku nimeona mwanaye kampost ana stroke
 
Umemsahau Msekwa.

Ila hawa viongozi Wastaafu wa CCM huwezi kuwaamini. Labda tuseme kimya chao tayari ni jibu tosha kuwa hawakubaliani na mkataba. Usually wangeshajitokeza kutetea Chama.
 
Je wewe kijana umefanya nini?,vijana wenzako walifanya street battles, wakakamatwa na police wa ccm,wakalala jela na wapo nje kwa dhamana, wewe unakimbilia humu na kusukuma uoga wako kwa wazee!!,battles za mabadiliko ziko kwenye streets sio humu
 
Ili iweje?

Waache wazee wamestaafu. Vipi umezidiwa hoja unaomba poo?

Mama anaupiga mwingi Kimataifa.
 
Ukiona kimya ujue wazee wameridhika na namna Watanganyika wanavyotetea nchi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…