Mzee Mkapa awasilisha salamu za Rais Magufuli kumuaga Mzee Moi, asema alikuwa 'mentor' wake

Mzee Mkapa awasilisha salamu za Rais Magufuli kumuaga Mzee Moi, asema alikuwa 'mentor' wake

Mimi naona wewe ndiyo unachukulia powa maana haujali hata usalama wa Rais wako. Unadhani mambo haya huwaga yanakwenda kirahisi rahisi tu. Msiwe mnachangia kama hakuna sababu ya kufanya hivyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
Labda uzungumzie usalama wa siri nisio ujua...
Lakini huyu JPM mara zote ni mzito na mvivu kuhudhuria matukio ambayo yataipa milestone nchi yetu...
Anajifungia ndani alafu akienda kanisani anajaza wana usalama wengi kuliko idadi ya wahumini...
Kama vipi si aende nao tu huko kimataifa...
Anaogopa nini kama kweli anatenda mema??
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mbowe kutoenda Kenya ni utani?

Mbwiga katika ubora uliotukuka!
Magufuli ameogopa kuonyeshwa vidole na Wakenya kwamba jamani muoneni yuleee aliyempiga risasi zaidi ya 30 Mh. Lisu aliyekuwa anatibiwa hapa Nairobi!
 
Rais mstaafu mzee Mkapa amesoma salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Magufuli katika msiba wa Mzee Moi.

Mzee Mkapa amesema yeye binafsi amefanya kazi na Mzee Moi kwa miaka 7, akiwa na Rais na mzee Kikwete aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Mkapa amesema Rais Magufuli amewatuma wao wawili kama ishara ya upendo na ushirikiano wa kindugu kati ya nchi zetu mbili.

=======

Akitoa salamu hizo, Mzee Mkapa amesema:

“Rais wangu Dkt. John Joseph Magufuli, kwa dhati kabisa ametuleta sisi wawili (na Mzee Kikwete) kuthibitisha ukaribu, undungu na umoja uliopo kati ya nchi zetu mbili”

“Nimekuwa Rais kwa miaka 10. Katika miaka hiyo 10, miaka 7 nilikuwa nafanya kazi na Rais Moi. Kwahivyo, kama alivyosema Dkt. Ruto, pamoja na kwamba ni mzee wetu, lakini kwangu mimi alikuwa ‘mentor’ katika utawala na uongozi. Ndiyo sababu nilisema lazima nije na ku-pay tribute kwa uhusiano huu niliokuwa nao, lakini vilevile kushirikiana nanyi katika kumuombea apumzike mahali pema peponi, kwa Mungu wetu ambaye alimpenda sana”

Mzee Mkapa pia ameambatana na Rais wa Awamu ya Nne, Dkt. Jakaya Kikwete ambaye ameeleza kumfahamu Mzee Moi tangu yeye (Kikwete) akiwa shule akisoma.

“Nimemfahamu Mzee Moi tangu nikiwa shule, nikisoma habari za Kenya, harakati za kudai uhuru wa Kenya. Baadaye na mimi nilipokuwa katika Serikali, nikiwa Waziri, niliwahi kuja. Nilitumwa na Rais wangu, Rais Ali Hassan Mwinyi nikiwa Waziri wa Nishati na Madini, kuja kuzungumza naye juu ya ushirikiano kati ya Tanzania na Kenya katika mradi tuliokuwa tumefikiria kuuanza wa kujenga bomba la gesi kutoka Songosongo kuja Dar es Salaam”

View attachment 1354416
Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Benjamin W. Mkapa akiwasilisha salamu za rambirambi kwa Wakenya, kwa niaba ya Rais John Magufuli.

View attachment 1354484
Rais wa Nne wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akitoa salamu zake kwa Wakenya kufuatia kifo cha Mzee Moi. Kikwete ameeleza mchango mkubwa wa Mzee Moi katika kuimarisha umoja wa wana Afrika Mashariki.
​

Source: Citizen TV
Mkapa msalimie Moi
 
Back
Top Bottom