TeamLowassa
JF-Expert Member
- Nov 30, 2013
- 1,495
- 936
Wapumbavu na malofa waliopoteza wapendwa wao kwa kukosa hela ya kuhonga hospitalini!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
That is too LOW from you..again.
Lazima uwavutie watu wajadili sera zako ili zifahamike na wengi na watu wajue umejipangaje.
Lodilofa amesababisha watu wasijadili sera wala shopping list yake. Hiyo sio positive point unless you encourage watu kumpitisha mtu wasiejua anataka kufanya nini KIPYA na kwa namna gani ambayo wenzake walishindwa.
Shopping list yake ni ileile ya Mkapa na JK, 20 years ago, na anashangaa kwamba hayo hayajafanyika.
Atueleze....Afya vipi?...., dispensary nchi nzima anafikiri ni sawa na peremende?
View attachment 280076
Hivi mkiitwa wapumbafu na malofa mtakataa? Mnatumia mda mwingi kujadili maneno mawili ya Nkapa badala ya kujadili hoja za Magufuli, au mmeona kuongea point tupu mmekosa cha kumkosoa?Punguzeni ULOFA basi
Wapumbavu na malofa walioshindwa kuendelea na masomo yao kwa kukosa ada!
Ni Hatareeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
Jana mzee Mkapa alimwaga radhi, CCM nayo ikamwaga radhi.
Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani wa Jangwani, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.
Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na TANU, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuikomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli, alisema.
Mzee niliyemzoea kwa hoja zenye mashiko na takwimu akageuka mlevi asiyejiheshimu.
Kweli ufalme wa CCM umefitinika.Kati ya mambo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiitofautisha brand ya CCM na Upinzani ni kule kutumia lugha zenye staha,kuhubiri amani na kuiishi.Jana rasmi CCM imevunja ndoa yake na sifa hizi.
Sasa tunaanza kupata picha tukimtazama Makonda, baadae Nape,Wasira,Kamani,Job Ndugai na sasa Mkapa tunaona CCM mpya inayozaliwa; brand ya ngumi,matusi na lugha za mihemko.
Mimi niwaambie tu,busara na hekima ni tunu ila ujinga hafundishwi mtu.Ni suala la kuamua tu!
Magufuli karibu UKAWA,you are a good manager but not a leader.
BURIANI CCM!

Amen, mungu ibariki people's power.Hofu ya watawala wetu ccm; Wapo radhi kufanya chochote ili mradi waendelee kuwepo madarakani kwasababu ya kulinda masilahi yao ya utajiri waliojilimbikizia kwa sababu wanahofu upinzani ukishika dora wa watachukuliwa hatua za kisheria.
Hofu ya Makada wa ccm wanaokihama chama kwenda upinzani inawanyima usingizi hofu inapanda maana hawa makada walikuwa ni viongozi wakubwa ndani ya serikali ccm wanayajua mambo mengi ni jinsi gani taifa linaibiwa wanainchi tukiachwa masikini wakutupwa na watoto wa vigogo wakineemeeka na kutunza fedha ughaibuni.
Kauli (wapumbavu na malofa) ya Rais msitaafu benjamini w mkapa nikauli ya kihuni ambayo haipaswi kutolewa na kiongozi mkubwa kama yeye.
WATANZANIA TUBADILIKE TUNAHITAJI MABADILIKO YA KIMFUMO SERA ILI TWENDE NA WAKATI TANZANIA BILA CCM NI TANZANIA MADHUBUTI ITAKAYO WAJALI WOTE NA KUGAWANA SUNGURA WETU KWA MLINGANYO SAHIHI MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA
MALOFA wote na WAPUMBAVU wote, Tuhakikishe ULOFA na UPUMBAVU wetu unakuwa Historia Jumapili ya Oktoba 25, 2015
Kwa mitusi ile na povu lile nani atampa tuzo yule?
Hizo in dalili za utawala uliochoka kumbuka hata gadafi alifikia hatua ya kuwaita wananchi wake panyaSalaam.
Kampeni za uchaguzi zimefunguliwa na sasa Kumekucha Tanzania!
Nipende kuwapongeza wanaCCM kwa kufungua rasmi kampeni yao hapo jana (23.08.2015) lakini kwa namna mpya ya kejeli, vijembe, matusi(vilivyokataliwa na tume) kutawala ufunguzi huo. Nilishtushwa na kauli za viongozi wa CCM kama vile Mh. Benjamin W. Mkapa kutukana hadharani. Mengi yamesemwa ikiwa ni pamoja na kusema "upumbavu na ulofa" si tusi. Nabaki najiuliza hata kama si tusi hakuna maneno makali ya kutumia tofauti na hayo, hasa kwa Rais mstaafu? Nakumbuka Mh. Tundu Lissu aliwahi kutamka maneno hayo Bungeni(haikuwa hekima), kwa kuwa alikosea basi ndiyo inahalalisha matumizi yake? leo inaonekana kama mtindo!
Wazungu wanasema 'Great minds discuss ideas, average minds discuss events and small minds discuss people" Nilitegemea kwa kikosi kile pengine kutoa maneno ya busara na kutofanya kuwa kijiwe cha chuki kwa waliokatwa.(wakiwakejeli wakiokatwa, na baadhi ya waliokatwa walio ndani ya CCM kumalizia hasira zao pale kwa kuwa walikatwa)!
Wengi wa viongozi hawa hawajui maisha halisi ya mtanzania wa chini(Kama wanajua wanajua kwa namna kufikirika tu), leo hii hawa ni watu wa kufanyiwa hivi
Kauli kama "Wapigwe tu...",
"Wapinzani(Waliokwenda Upinzani) ni wapumbavu na malofa",
"Mil. 10 ni fedha ya mboga tu",
"Mkishindwa kulipa nauli mpige mbizi",
"Tutashinda tu hata kama kwa goli la mkono" na aina nyingine nyingi ya matusi, kejeli na dharau vinamdhalilisha mwanananchi!
Ninahitaji Kiongozi anayesimamia sheria, inaposemwa mwisho wa mkutano ni saa kumi na mbili jion(saa 12:00), basi na iwe hivyo lakini si saa 1231!
Ninahitaji kiongozi mwenye busara katika matamshi ya maneno na mwenye kuulinda ulimi wake!
Nahitaji kiongozi mwenye kunadi ilani yake, sera zake kwa umakini na namna nitakayoelewa na si kuponda upande mwingine(wa pili) kwasababu ya umasikini wa hoja anazoshindwa kutoa.
Tatizo wengi wa viongozi wanadhani "immunity" waliyonayo inawakinga na UHAI wao! Wananchi pia wana 'threshold' yao ya uvumilivu na hasira. Niwakumbushe tu kuwa kulikuwa na viongozi makini sana 'Nchi za watu' waliouawa tena wakiwa na Ulinzi wa kutosha kwa sababu ya kauli mbovu tu pamoja na umakini wao. Tena kwa sisi na vijana wetu(waliokwenda jeshi) na hawana ajira(ninyi mwawaita vibaka), watakaowa-assassinate, mmoja baada ya mwingine ndipo mtakapotambua 'maskini jeuri' wa nchi hii.
Wengi wanadhani bado wanaweza kupumbaza watu kwa vyombo vya habari vya ndani(Local Media) lakini niseme Afrika Mashariki sasa inaona Afrika na Dunia nzima sasa inaona kinachoendelea Tanzania(ikitazama Viongozi wakubwa wakitukana hadhari, wakistaajabu aibu kubwa ya viongozi kujiandaa kusimama kuponda upande wa pili bila ya wao kuwa na hoja).
Kwa sasa ilani ya CCM imekuwa ni UKAWA, Hoja zao ni UKAWA. Bila UKAWA CCM haitaweza kuwepo!
Hivyo basi mimi na upumbavu, ulofa wangu nikiwa 'kibaka' na 'mnywa viroba' nitaisubiri Oktoba 25, 2015 kwa Mapenzi ya MUNGU kuonyesha ubora wangu na kichinjio changu.