Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Wapumbavu na malofa waliopoteza wapendwa wao kwa kukosa hela ya kuhonga hospitalini!
 
ila issue ya kuweka namba hapa sio nzuri sana

Mods wa hii forum hawaaminiki kabisa

wape watu email yako na wakutumie huko

Au toa ya kwako watu wakutumie huko boss
 
Wapumbavu na malofa waliopoteza wapendwa wao kwa kushinda kumudu gharama za matibabu!
 
Safi kabisa mkuu

Naomba niibe picha yako tafadhali niitume kwenye magroup mia sita

na kwenye kila thread ya mafisadi
 
Hivi mkiitwa wapumbafu na malofa mtakataa? Mnatumia mda mwingi kujadili maneno mawili ya Nkapa badala ya kujadili hoja za Magufuli, au mmeona kuongea point tupu mmekosa cha kumkosoa?Punguzeni ULOFA basi

Malofa ni wananchi wote wa kawaida pamoja na wewe. Huo ndiyo ujumbe alioutoa Mzee Nkapa kama hukuupata sawasawa. Sasa wewe unatukanwa kwa vile tu uko CCM huoni kuwa umetukanwa. Poor you ... Wewe utakuwa ni zaidi ya Lofa!!
 
Ni msemo ulitolewa na Mzee Mkapa katika mkutano wa ufunguzi wa kampeni za CCM.

Tangu kutolewa msemo/sifa/tusi hili, nimejaribu kupitia katika mitandao mingi ya kijamii...nimeona watu wengi mpaka wagombea wa udiwani na ubunge kupitia ukawa wakijadili "sifa/tusi" hili kwa wingi sanaaa (posts/ comments).

Tumejikuta tukisahau, dhima, malengo, mikakati, sera, taratibu na mambo mbalimbali ya kuwaeleza wananchi juu ya ukawa.

Tunamaliza muda mwingi kujadili hoja ya sifa/ msemo wa mzee huyu. tukiacha kutambua muda wa kampeni ni mchache sanaa wao wameanza kuzurura sasa mikoani...sisi tunashinda kwenye mitandao tukisema tuuuuuuu, wakat ni 15% ya watanzania wenye sifa ya kupiga kura ndio utumia mitandao.

Mwisho naomba turudi kwenye kuelemisha mwananchi nia ya ukombozi wa pili kupitia ukawa.
 
Hofu ya watawala wetu ccm; Wapo radhi kufanya chochote ili mradi waendelee kuwepo madarakani kwasababu ya kulinda masilahi yao ya utajiri waliojilimbikizia kwa sababu wanahofu upinzani ukishika dora wa watachukuliwa hatua za kisheria.
Hofu ya Makada wa ccm wanaokihama chama kwenda upinzani inawanyima usingizi hofu inapanda maana hawa makada walikuwa ni viongozi wakubwa ndani ya serikali ccm wanayajua mambo mengi ni jinsi gani taifa linaibiwa wanainchi tukiachwa masikini wakutupwa na watoto wa vigogo wakineemeeka na kutunza fedha ughaibuni.
Kauli (wapumbavu na malofa) ya Rais msitaafu benjamini w mkapa nikauli ya kihuni ambayo haipaswi kutolewa na kiongozi mkubwa kama yeye.
WATANZANIA TUBADILIKE TUNAHITAJI MABADILIKO YA KIMFUMO SERA ILI TWENDE NA WAKATI TANZANIA BILA CCM NI TANZANIA MADHUBUTI ITAKAYO WAJALI WOTE NA KUGAWANA SUNGURA WETU KWA MLINGANYO SAHIHI MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA
 
Nakuongezea na wewe acha upumbavvu maana una ugonjwa wa kusahau mpumbavu mkubwa tena uwe na heshima kwa viongozi wako inaonekana wewe hata wazazi wako umewashinda
 
Last edited by a moderator:
Hofu ya watawala wetu ccm; Wapo radhi kufanya chochote ili mradi waendelee kuwepo madarakani kwasababu ya kulinda masilahi yao ya utajiri waliojilimbikizia kwa sababu wanahofu upinzani ukishika dora wa watachukuliwa hatua za kisheria.
Hofu ya Makada wa ccm wanaokihama chama kwenda upinzani inawanyima usingizi hofu inapanda maana hawa makada walikuwa ni viongozi wakubwa ndani ya serikali ccm wanayajua mambo mengi ni jinsi gani taifa linaibiwa wanainchi tukiachwa masikini wakutupwa na watoto wa vigogo wakineemeeka na kutunza fedha ughaibuni.
Kauli (wapumbavu na malofa) ya Rais msitaafu benjamini w mkapa nikauli ya kihuni ambayo haipaswi kutolewa na kiongozi mkubwa kama yeye.
WATANZANIA TUBADILIKE TUNAHITAJI MABADILIKO YA KIMFUMO SERA ILI TWENDE NA WAKATI TANZANIA BILA CCM NI TANZANIA MADHUBUTI ITAKAYO WAJALI WOTE NA KUGAWANA SUNGURA WETU KWA MLINGANYO SAHIHI MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA
 
Amen, mungu ibariki people's power.
 
MALOFA wote na WAPUMBAVU wote, Tuhakikishe ULOFA na UPUMBAVU wetu unakuwa Historia Jumapili ya Oktoba 25, 2015

Kuna msemo unasema 'Do not underestimate the power of stupid people in large groups', Ninaimani Mkapa aliyakumbuka haya kabla ya kuita watu ni wapumbavu na malofa!
 
Mtu mwenye akili timamu hawezi kuuza rasilimali za taifa kwa milioni mia7.
 
Mpumbavu na Lofa ni yule aliyeuza Benki kwa bei ya kutupa!
 
Hizo in dalili za utawala uliochoka kumbuka hata gadafi alifikia hatua ya kuwaita wananchi wake panya
 
Ndugu zangu watanzania,

Katika hali ya ubabe wa viongozi wa CCM na kwa kuwa wanaogopa kama wakitoka madarakani huenda wakafikishwa katika mahakama ya AICC au the Hague.

Kwa mara ya kwanza Kikwete alisikika akilalamika kwa nini mahakama ya AICC inawashughulikia viongozi wa nchi za Africa tu?! Mbona hajaona hata kesi moja inayomuhusu kiongozi wa nchi za Ulaya?!

Lakini katika kutilia mkazo kauli hiyo Rais wa Awamu ya tatu katika serikali ya Jamhuri ya Muungano Ndugu Benjamini W. Mkapa ambaye na yeye ana kashfa nyingi za kujilimbikizia mali. Ndiyo katika kuona hali ya kupelekwa AICC haiepukiki ameamua kufyatuka (sijui alikuwa kisha weka spirit kichwani?) na kuwaita wale wote wanaopigania raslimali za nchi kutumiwa na wanachi ni WAPUMBAVU NA MALOFA.

Nijuavyo mimi;

MALOFA ni watu wasiojua hali yao ya baadae kimaisha itakuwaje kwa upande wa KULA, KUNYWA, MAVAZI na HUDUMA ZA KIJAMII KWA UJUMLA.

WAPUMBAVU ni watu wanayeshindwa kuelewa jambo hata akielezwa, juha, zuzu, jura, nyange, baghami, bahau, hambe, maarasi, zebe, mbumbumbu.

ASUBUHI NJEMA

WAPUMBAVU NA MALOFA WENZANGU.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…