Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Walioshindwa wote wamehamia chadomo, huwajuwi?

Makapi yamenunuwa nafasi ya kugombea Urais. Uliona wapi dunia hii?

Mchagga anauzza utu wae kwa pesa na hilo Mbowe kalidhihirishia Ulimwengu.

Kama kuna watu wataechaguwa mgombea kama huyo na chama kama hicho, basi nnayakubali maneno ya Mkapa, hao watakuwa ni Wapumbavu na malofa - Mkapa.

I feel pity on you Faiza
 
Na nyie bado mnasikiliza hoja za watu wa kale...!!!! Au hamjui ya kwamba siku hizi ndoa, maisha, ukata, n.k. vinawatia watu stress? kwa hiyo sehemu ya ku-release stress ni kwenye majukwaa ya politics.
 
I feel pity on you Faiza

Is that all? You are note feeling "pity" to your own self? To follow those who do not have even simple principles and ethics?

Today Lowassa is Mr. Clean and Dr. Slaa is Mr. Dirty, is that what you believe?
 
Mkapi alivunja ofisi na kuiba mitihani Makerere au amesahau.
 
Nimeshangazwa Na tafsiri ya ukombozi eti ni kupata Uhuru Mh Mkapa alisema Tanzania ilikwisha pata Uhuru ukawa wanaikomboaje tena? Akawaita wapumbavu asante mkuu. Je Magufuli juzi kasema ataijenga Tanzania upya, Je wewe Na marais wastaafu mlikuwa hamuijengi Tanzania? Na kama mlikuwa mnaijenga nae anataka kufanya nini tena? Nadhani kuikomboa Tanzania iliyopata Uhuru tayari in Upumbavu, Je kuijenga Tanzania mlioijenga nyie wastaafu ni Ujinga au sio mkuu?
 
Is that all? You are note feeling "pity" to your own self? To follow those who do not have even simple principles and ethics?

Today Lowassa is Mr. Clean and Dr. Slaa is Mr. Dirty, is that what you believe?

I never see you support Slaa until today!
I like Slaa a lot,its just as Julius Caesar put it,"There is a tide in the affairs of men,if taken at floods could lead to success" That saying fits settings of the moment,for Lowassa it means its now or never!
 
Wako wapi hao wakombozi aw kweli zaidi ya Dr.Slaa? Hao wengine ni Wasakatonge tu!


Jana mzee Mkapa alimwaga radhi, CCM nayo ikamwaga radhi.

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani wa Jangwani, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.

“Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na TANU, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, … ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuikomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli,” alisema.

Mzee niliyemzoea kwa hoja zenye mashiko na takwimu akageuka mlevi asiyejiheshimu.

Kweli ufalme wa CCM umefitinika.Kati ya mambo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiitofautisha brand ya CCM na Upinzani ni kule kutumia lugha zenye staha,kuhubiri amani na kuiishi.Jana rasmi CCM imevunja ndoa yake na sifa hizi.

Sasa tunaanza kupata picha tukimtazama Makonda, baadae Nape,Wasira,Kamani,Job Ndugai na sasa Mkapa tunaona CCM mpya inayozaliwa; brand ya ngumi,matusi na lugha za mihemko.

Mimi niwaambie tu,busara na hekima ni tunu ila ujinga hafundishwi mtu.Ni suala la kuamua tu!

Magufuli karibu UKAWA,you are a good manager but not a leader.

BURIANI CCM!

 
Last edited by a moderator:
Inasikitisha....yaani Mkapa hajijuwi kuwa yeye ndiyo mjinga? CCM inamtumia kwa kumtoa muhanga wakati huu wa uchaguzi ili watanzania wamshitaki kwa kumuua baba wa taifa. Lazima kieleweke mwaka huu na The Hague lazima aende tu mwaka huu. Kikwete anaona mbali kidogo kwani wiki iliyopita tu alisha anza kubwabwaja kuwa mahakama kuu ya The Hague inawaonea viongozi wa waafrika, hii yote ni kwa sababu anafahamu kuwa siku za Mkapa kunyongwa inakaribia.
 
Uloi nga mâché68;13766079 said:
Wako wapi hao wakombozi aw kweli zaidi ya Dr.Slaa? Hao wengine ni Wasakatonge tu!

Hivi kwa mfano Lowasa ambaye dunia nzima inamgwaya kwa utajiri alionao anaweza kuitwa msaka tonge, au mkombozi!
 
MPUMBAVU ni wewe na wapumbavu wenzako. nchi imepata uhuru wa bendera lakini bado haijakombolewa KIUCHUMI, KISIASA na KIFIKRA. mtapayuka sana mwaka huu na mwisho wa upayukaji wenu ni oktoba 25.
tpaul hakuna haja ya kubishana hapa majibu october ndio mtajua kwanini mzee Mkapa kawaita wapumbavu...
MUNGU IBARIKI TANZANIA, kidumu Chama Cha Mapinduzi:A S 41:
 
Neno Fupi La Leo: Mjinga Na Mpumbavu..


Ndugu Zangu,

Nilikuwepo pale Viwanja vya Jangwani. Nilipomsikia Ben Mkapa akiwaita wapinzani ' Wapumbavu na Malofa', basi, nikajua hiyo ndio ingekuwa ' Habari ya Mjini'. Nilikuwa sahihi. Ni kwa vile aliyetamka hayo alikuwa Ben, Rais Mstaafu.

Na hakika, mitaani huko nimekutana na watu wanaohangaika sana hata kuingia kwenye kamusi ya Kiswahili kuona tafsiri ya maneno aliyotamka Ben, kama ni matusi au la!
Katika hili, yaweza pia kusemwa, kuwa Ben amechangia kupromoti lugha ya Kiswahili.

Na hakikatafsiri zaweza kuwa nyingi, na hasa katika wakati huu wa joto la kisiasa linalopanda. Tukianza na Lofa, ina tafsiri ya mtu aliyefilisika,kupungukiwa mtaji na hata mwenye kutembea akipoteza muda. Yaweza pia kutafsiriwa kuwa kufilisika kisiasa. Inategemea na imetamkwa katika muktadha gani. Chimbuko lake ni kwenye kimombo; ' wasting time'- Are you loafing, you better hurry up and do! ....
Naam, mapambano ya kisiasa, na hususan kwenye kampeni za uchaguzi huwa na sura ya mikakati inayyofanana na ya mapambano ya kijeshi. Na kwenye vita kinachopelekea ushindi ni vitu vitatu; Silaha bora, uwezo wa wapiganaji na propaganda.

Huenda si wengi wenye kukumbuka kuwa Ben Mkapa alipata kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje kwenye kipindi ambacho Tanzania ilikuwa vitani dhidi ya Idd Amin.

Ni Ben Mkapa aliyeongoza vita vya propaganda dhidi ya Idd Amin, dunia ikaaminishwa kuwa Tanzania ilikuwa na sababu, uwezo na nia ya kumpiga Idd Amin. Ni kwenye kipindi kile cha vita, na kazi ya fasihi kwenye lugha ya vita ilifanywa na watu wa aina ya Ben Mkapa na Paul Sozigwa na iliyotumika vema kwenye propaganda za kimapambano. Ndio, ikamfanya Idd Amin aonekane si lolote si chochote.
Nini basi tofauti ya Mjinga na Mpumbavu?

Marehemu Mzee Jongo alipata kutamka; " Kusoma sio kuufuta ujinga, bali ni kuupunguza". Kila mwanadamu ana ujinga wa jambo moja au mia moja. Kuwa na ujinga wa jambo si kosa, hata Profesa anaweza asijue namna ya kuchochea kuni za kuchomea hindi bichi likachomeka. Kijana wa darasa la saba anaweza kuwa hodari wa jambo hilo kumshinda Profesa.

Lakini, upumbavu ni ile hali ya mwanadamu kufanya jambo isivyotakiwa huku akiwa na uelewa wa namna ya kufanya inavyotakiwa. Huo ndio upumbavu.

Hoja ya Ben kama ametukana au la, inabaki kuacha uwanja wazi wa tafsiri kwa anayetaka kutafsiri anavyotaka yeye, bila kuacha kuzingatia, kuwa tumo kwenye joto la kisiasa linalopanda. Na ndio utamu wa fasihi pia..!
Ukumbi wenu wajumbe kujadili.

Maggid.

chanzo Mjengwa blog
 
Mkapa anawashtua jamaa zake aliokuwa nao kwenye meza ya ulaji maana anawashangaa wanavyoikimbia himaya ya madikodiko na kwenda kuanza upya utafutaji.Ndio maana anawaona ni wapumbavu na malofa japo sina uhakika kama tulilengwa wote.
 
hii kauli ya huyuu muheshimiwa Ni dhahiri kuwa Siasa imempita kushoto na hata wakati wake wa Uongozi alijikusanya Kusanya ndo akapewa kiti!!

Mtu Makini uliyewahi kuwa Kiongozi mkuu wa taifa hili kuwaita watu wako MALOFA Na WAPUMBAVU ni utovu wa nidhamu ya Utaifa na ujinga wa Mawazo duni na ya kizamani yasiyo kwenda na Wakati!!

nasema yasiokwenda na Wakati kwakuwa siasa yake si sawa na Hii ya KIKWETE, CCM ya mwaka 95 sio ya Mwaka huu 2005!! ebu kaa na Mama Anna Akuliwaze mkitanua Visenti vyenu vya MGODI wa kiwila achana na siasa Mzeeeee!!!

Ukishindwa basi Mrithi kpt KOMBA mzeee labda unaweza ziba pengo lake la kuwarusha Roho wakina Mama wa CCM.....
 
Hapo ndio akiliza ccm zilipofikia baada ya kupo madarakani kwa zaido ya miongo mitatu.
Ni muda muafaka kwa Watanzania walio MALOFA na WAPUMBAVU kufanya maamuzi sahihi kupitia sanduku za kura zilizo lindwa vyema kuung'oa udhalimu
 
Back
Top Bottom