Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

watu kama sumaye sijui motive yake ni nini. kama ni madaraka ya juu kabisa alikuwa nayo kwa miaka 10 akiwa msaididzi namba moja wa mkapa. kuhamia ukawa sijui anafikiri atapata nafasi gani ya juu zaidi ya kuwatumikia wananchi zaidi ya aaliyokuwa miaka ile 10

mwenzake anajulikana. motive ni kupiga zaidi hela na kulipa visasi

Hata yeye amesema hatafuti nafasi yoyote.
 
Wanajamvi jana wakati ccm inazindua kampeni yake katika uwanja wa jangwani,Rais mstaafu wa awamu ya tatu ,wakati amepewa nafasi ya kumwaga sera za chama chake,Aliishia kusema WAPINZANI NI WAPUMBAVU NA MALOFA WAKUBWA.Pamoja na mkapa kukosa busara,vilevile alionyesha ni kwa jinsi gani ni MPUMBAVU NA LOFA ZAIDI YA WAPINZANI aliowatukana.Lofa na mpumbavu ni nani kati ya mkapa na wapinzani?....Ni mkapa kwa sababu:-

1.Inasemekana kuwa mkewe mkapa kabla ya kuolewa na mkapa alikuwa ni mke wa mramba,Ambapo alizaa na mramba mtoto mmoja halafu mkapa akachukua makombo ya mramba.Hapohapo mkapa akamteuwa mramba kuwa mkuu wa mkoa badaye waziri wa fedha.Nani ni lofa na mpumbavu kama siyo yeye.

2.Mwaka 1991 mkapa akiwa waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa alizuia wajerumani watatu wasikamatwe na jeshi la polisi baada ya wajerumani hao kumtumia mbwa kumlawiti msichana wa kitanzania katika fukwe za oysterbay dsm,huku akijua kuwa kitendo hicho siyo makosa yanayoangukia mkataba wa vienna.Inasemekana alihongwa dutchmark 2,400 tu.Nani ni lofa kati ya mkapa na wapinzani?.

3.Mwaka 1996 mkapa alipatikana na kashfa ya rushwa ya shilingi milioni 900,zinazosemekana alihongwa na wafanyabiashara wa minofu ya samaki wa mwanza.Mpaka sasa mkapa hakuwahi kukanusha tuhuma hizi.Rais mzima kuhongwa ni ulofa na upumbavu au siyo?.

4.Kuna tetesi kuwa mkapa aliongwa na makaburu shilingi milioni 700 ili awauzie bank ya NBC.Awali ilijulikana kana kuwa fedha hizo zilikuwa kama mkopo ili watanzania wasijue lkn baadaye mkopo huo haukulipwa na mkapa.Nani ni mpumbavu na lofa kati ya mkapa na wapinzani?.

5.Wakati wa utawala wa mkapa ndiyo wakati tulioshuhudia ufisadi mkubwa kuliko wakati wote wa utawala wa nchi yetu tangia tupate uhuru.MEREMETA,DEEP GREEN,EPA,DCP,KIWIRA,NSSF,KILIMANJARO HOTEL,SUKARI NK.



Ni vyema mkapa akatambua kuwa watanzania wengi tunajua madhambi yake ila muda wa kumwondolea kinga umefika.Asifikiri kwamba hakamatiki!...Asifikiri kuwa hatumuwezi.Na asifikiri kuwa sisi ni wapumbavu na malofa kama yeye.Mkapa atambue kuwa hata nyumba aliyomjengea hawara yake wa kanada ,ambaye alikuwa mke wa mtu hatujui.Mkapa atambue kuwa vifo vya watanzania wenzetu waliokuwa viongozi wetu tunajua alishiriki na muda wa kutueleza umefika.Mkapa atueleze kifo cha kolimba,nkulu,mwaikambo,omar ally juma,kombe,mpiana malicela,nyerere vilitokeaje na nani alihusika na kwa maslahi ya nani.
 
Stupid gang of devils
This time we will know the truth about the the death of the father of our nation. Wait the game is begining!! ICC /hague

Meku hilo tusi ni kali mno....aisee nakiri sijawahi kuliskia mahali....stupid gang of devils!!!?... hatari mno
 
Wapumbavu na malofa siku zote ni rahisi sana kujiuza hata utu wao kwa thamani ndogo sana.

Leo wapumbavu na malofa kwa kununuliwa tu, wale waliowaita mafisadi wamegeuka malaika.

Amma kwa hakika wapumbavu hawaishiwi na vituko.
 
Salaam.

Kampeni za uchaguzi zimefunguliwa na sasa Kumekucha Tanzania!

Nipende kuwapongeza wanaCCM kwa kufungua rasmi kampeni yao hapo jana (23.08.2015) lakini kwa namna mpya ya kejeli, vijembe, matusi(vilivyokataliwa na tume) kutawala ufunguzi huo. Nilishtushwa na kauli za viongozi wa CCM kama vile Mh. Benjamin W. Mkapa kutukana hadharani. Mengi yamesemwa ikiwa ni pamoja na kusema "upumbavu na ulofa" si tusi. Nabaki najiuliza hata kama si tusi hakuna maneno makali ya kutumia tofauti na hayo, hasa kwa Rais mstaafu? Nakumbuka Mh. Tundu Lissu aliwahi kutamka maneno hayo Bungeni(haikuwa hekima), kwa kuwa alikosea basi ndiyo inahalalisha matumizi yake? leo inaonekana kama mtindo!

Wazungu wanasema 'Great minds discuss ideas, average minds discuss events and small minds discuss people" Nilitegemea kwa kikosi kile pengine kutoa maneno ya busara na kutofanya kuwa kijiwe cha chuki kwa waliokatwa.(wakiwakejeli wakiokatwa, na baadhi ya waliokatwa walio ndani ya CCM kumalizia hasira zao pale kwa kuwa walikatwa)!

Wengi wa viongozi hawa hawajui maisha halisi ya mtanzania wa chini(Kama wanajua wanajua kwa namna kufikirika tu), leo hii hawa ni watu wa kufanyiwa hivi

Kauli kama "Wapigwe tu...",

"Wapinzani(Waliokwenda Upinzani) ni wapumbavu na malofa",

"Mil. 10 ni fedha ya mboga tu",

"Mkishindwa kulipa nauli mpige mbizi",

"Tutashinda tu hata kama kwa goli la mkono" na aina nyingine nyingi ya matusi, kejeli na dharau vinamdhalilisha mwanananchi!

Ninahitaji Kiongozi anayesimamia sheria, inaposemwa mwisho wa mkutano ni saa kumi na mbili jion(saa 12:00), basi na iwe hivyo lakini si saa 1231!

Ninahitaji kiongozi mwenye busara katika matamshi ya maneno na mwenye kuulinda ulimi wake!

Nahitaji kiongozi mwenye kunadi ilani yake, sera zake kwa umakini na namna nitakayoelewa na si kuponda upande mwingine(wa pili) kwasababu ya umasikini wa hoja anazoshindwa kutoa.


Tatizo wengi wa viongozi wanadhani "immunity" waliyonayo inawakinga na UHAI wao! Wananchi pia wana 'threshold' yao ya uvumilivu na hasira. Niwakumbushe tu kuwa kulikuwa na viongozi makini sana 'Nchi za watu' waliouawa tena wakiwa na Ulinzi wa kutosha kwa sababu ya kauli mbovu tu pamoja na umakini wao. Tena kwa sisi na vijana wetu(waliokwenda jeshi) na hawana ajira(ninyi mwawaita vibaka), watakaowa-assassinate, mmoja baada ya mwingine ndipo mtakapotambua 'maskini jeuri' wa nchi hii.

Wengi wanadhani bado wanaweza kupumbaza watu kwa vyombo vya habari vya ndani(Local Media) lakini niseme Afrika Mashariki sasa inaona Afrika na Dunia nzima sasa inaona kinachoendelea Tanzania(ikitazama Viongozi wakubwa wakitukana hadhari, wakistaajabu aibu kubwa ya viongozi kujiandaa kusimama kuponda upande wa pili bila ya wao kuwa na hoja).

Kwa sasa ilani ya CCM imekuwa ni UKAWA, Hoja zao ni UKAWA. Bila UKAWA CCM haitaweza kuwepo!

Hivyo basi mimi na upumbavu, ulofa wangu nikiwa 'kibaka' na 'mnywa viroba' nitaisubiri Oktoba 25, 2015 kwa Mapenzi ya MUNGU kuonyesha ubora wangu na kichinjio changu.
 
Jana mzee Mkapa alimwaga radhi, CCM nayo ikamwaga radhi.

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani wa Jangwani, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.

“Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na Tanu, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, … ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuiomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli,” alisema.

Mzee niliyemzoea kwa hoja zenye mashiko na takwimu akageuka mlevi asiyejiheshimu.

Kweli ufalme wa CCM umefitinika.Kati ya mambo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiitofautisha brand ya CCM na Upinzani ni kule kutumia lugha zenye staha,kuhubiri amani na kuiishi.Jana rasmi CCM imevunja ndoa yake na sifa hizi.

Sasa tunaanza kupata picha tukimtazama Makonda, baadae Nape,Wasira,Kamani,Job Ndugai na sasa Mkapa tunaona CCM mpya inayozaliwa; brand ya ngumi,matusi na lugha za mihemko.

Mimi niwaambie tu,busara na hekima ni tunu ila ujinga hafundishwi mtu.Ni suala la kuamua tu!

Magufuli karibu UKAWA,you are a good manager but not a leader.

BURIANI CCM!


Mithali.18:18/Hagai. 2:21-22
 
Last edited by a moderator:
Watu tunakuwa wasahaulifu sana. Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(SUGU) kwa kumtaja jina, alimuita Waziri Mkuu MPUMBAVU bila ya kuwa na sababu yoyote ya msingi. Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akamtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumtaja jina kuwa ni DHAIFU.

Inasikitisha sana kuona kauli ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Willium Mkapa kuwa baadhi ya wapinzni wanaosema wanataka kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa kutafsiriwa kuwa ni matusi kwa Wapinzani. Hivi ni mtanzania gani hajui Tanzania ilishatoka mikononi mwa Wakoloni?(Ilishakombolewa?)

Mzee Mkapa alitumia maneno sahihi kabisa kwa mtu ambaye anajitoa ufahamu wa ukweli wa jambo. Ni sifa gani ambayo inastahili kwa mtu anayetaka kulikomboa Taifa ambalo tayari lilishakombolewa? Anashindwa kweli kutumia hata maneno kama MABADILIKO na siyo UKOMBOZI?

wapinzani nawaonya msije mkakomalia kauli ya MKAPA na mkaacha kujikita kwenye agenda za msingi. Alichokisema Mkapa ni sahihi kabisa, Tanzania ilishakombolewa na kinachotakiwa ni MABADILIKO ambayo siyo lazima yaletwe na Wapinzani bali chamamchochote chenye MGOMBEA MWADILIFU na anayetokana chama chenye Sera safi na siyo UKOMBOZI.

wote tunaoamini Tanzania ni Taifa huru lazima tuungane na kauli ya MKAPA na pengine kauli hii iwe fundisho kwa wanasiasa wanaotumia maneno yanayowapotosha watanzania.
 
Malofa na wapumbavu hawaishiwi na vituko.

Kituko cha mwaka, yule mliyemuita fisadi leo yuko juu kwenye chama cha wapumbavu kuliko Katibu Mkuu wake.

Hivi Katibu mkuu wa malofa kaishia wapi?
 
CCM mmeamua kutukana wapiga kura mmezidi kumuharibia magufuli.
hichi kibri mlichonacho ndiyokimefika mwisho.
 
Mkapa kuwaita watu wanaotaka mabadiliko ni wapumbavu na malofa ni mwendelezo wa kauli za dharau zinaendelea kutololewa na viongozi wa ccm hata Magufuli aliwahi kuwaambia wananchi wa kigamboni asiye kuwa sh.mia mbili apige mbizi'
watanzania watambue kipindi ccm kuondoka madarakani lazima wachanganyikiwe wapumbavu na malofa tutawaonyesha kwenye sanduku la kura .
#UKAWA wala hatuna haja kuwajibu hawa wajinga ambao Mungu ameshapiga upofu sasa muda wa kumwaga sera zetu kwa wananchi.
 
Usiseme sisi wananchi - sema wewe na mkeo na wapumbavu wenzako/ na malofa ndio mtapiga hizo kura, mwenzako bado nasubiri sera za vyama vingine ili nitoe uamuzi muafaka... kuna vyama vingi sana havijazindua kampeni na wananchi kibao bado wanasubiri kuviskiliza.
Heeeee, Heeee ni tuna masikitiko makubwa kwa kauli ya MATUSI aliyotoa Mh. Rais mstaafu Ben Mkapa jana katika uzinduzi wa kampeni kwa chama tawala (CCM). Alisema wapinzani ni WAPUMBAVU na akarudia ni WAPUMBAVU SANA.

Sasa kwa masharti yaliyotolewa na tume ya uchaguzi ya kutotoa kauli za kuudhi wala kashfa huyu naye mbona alikiuka?

Mzee Mkapa iga mfano kwa Rais mstaafu mwenzio Mzee Mwinyi alivyotoa hotuba ya busara.

Kwa wadhifa wako hukupaswa kutukana kabisa, kwa hapo Mh umekididimiza chama.

Sasa sisi wananchi ni jukumu letu tarehe 25 Octoba,2015 kuondokana na watu wa chama kile kile miaka yoooote toka uhuru ambao hawana lugha nzuri kwa kizazi kijacho.


Jamaaaaaaniii eeeee akili kumkichwa, Oct, 25
 
Rudia kusoma ulichoandika...kama utaona kila kitu kiko sawa, anza kutangulia mirembe, la kama kuna upungufu basi urekebishe!
 
Malofa na wapumbavu hawaishiwi na vituko.

Kituko cha mwaka, yule mliyemuita fisadi leo yuko juu kwenye chama cha wapumbavu kuliko Katibu Mkuu wake.

Hivi Katibu mkuu wa malofa kaishia wapi?

Umetoka eda mara hii...... Fanyeni kampeni safi acheni mijitusi haiwasaidii
 
Malofa na wapumbavu hawaishiwi na vituko.

Kituko cha mwaka, yule mliyemuita fisadi leo yuko juu kwenye chama cha wapumbavu kuliko Katibu Mkuu wake.

Hivi Katibu mkuu wa malofa kaishia wapi?

Mwisho wa yote october 25, aibu yako au aibu yangu. TATU BILA!
 
Enyi wapumbavu na Malofa, jiandaeni kuhama nchi baada ya uchaguzi, vinginevyo, jela

Hakika naiona Tanzania mpya baada ya uchaguzi wa Oktoba. Tanzania ijayo itakuwa mahala pabaya sana kuishi kwa wapumbavu na malofa.

1. Kutakuwa na jela maalum kwa malofa na wapumbavu ambao siku zote wamekuwa wakituibia Watanzania. Mafisadi, majizi na mahujumu uchumi.

2. Tanzania ijayo itaweka usawa baina ya wananchi. Hiyo itawanyima fursa mafisadi ambao wamekuwa wakitumia umaskini wetu kujitajirisha.

3. Tanzania ijayo itakuwa ya viwanda. Wananchi wengi watakuwa busy na kazi hivyo itakuwa ngumu kwa wapumbavu na malofa kuwatumia Watanzania kama chambo kwenye maandamano.

4. Elimu itakuwa bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari. Yale mafisadi yaliyotuibia yakajenga mashule yao yakawa yanatoza ada kubwa sasa hali itakuwa mbaya. Heshima ya shule za serikali itarudi tena.

5. Enyi mafisadi, katika Tanzania ijayo, ili chama kiwe cha siasa lazima kiwe na sura ya kitaifa. Chama ambacho viongozi wake wakuu wanatoka kanda moja tu hakitapata nafasi ya kugombea

6. Enyi wauza unga, Tanzania ijayo viwanja vya ndege na bandari vitakuwa havipitiki. Biashara yenu itaingia kirusi na hivyo hakutakuwa na fedha za kufadhili mafisadi kwenda Ikulu.

7. Enyi malofa na wapumbavu, CCM kimezaliwa upya baada ya malofa, wapumbavu na wachawi kuhama chama. Waliobaki tunaserebuka na kucheza.

8. Enyi mafisadi na malofa, mmekuwa mkihujumu sana hospitali za serikali kwa kujenga mafoka kando ya hospitali hizo. Mmekuwa mkihamisha dawa za serikali na kuuza kwenye maduka binafsi. Tanzania ijayo hakutakuwa na mwanya huo. Heshima ya hospitali za serikali itarudi tena.


Ujumbe huu uwafikie wafuatao.
...


1. JAKAYA MRISHO KIKWETE


2.ANNA TIBAIJUKA


3.ABDURAHMAN KINANA


4.BENJAMIN MKAPA

na wote wanaohusika.....
 
Wanaodanganya watanzania kuwakomboa wakati tulishakombolewa na CCM
Unaposema hakutaja chama, hao wanaotaka kuwakomboa watanzania wako vyama gani? If a = b and b = c, then a = c.
 
Back
Top Bottom