Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Wana JF Heshima kwenu.

Mithali 26:5
Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.

Aidha neno upumbavu limeandikwa zaidi ya mara 46 katika Biblia. Mfano :-

Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.

Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.

Aidha Rais wa kwanza wa TZ; Mwl Nyerere amekuwa akitumia neno hili mara nyingi sana. Huko ndiko Mhe. MKAPA alipojifunzia. (Nimeshindwa kuweka video clip msaada plz)

Mhe. Sugu alipotumia neno mpumbavu pale mjengoni UKAWA walimtetea. Leo kwao limetumika imekuwa nongwa kwenye mitandao. Kweli nyani haoni naniii yake.

Mhe. Mkapa ni Mkristo mzuri mwenye kusoma Neno la Mungu kila wakati. Alichofanya ni kujibu hoja ambayo ameipima na kuiona ni ya kipumbavu ili walioitoa wasijione wana akili.

Nani asiyejua Mhe. Sumaye alibatizwa jina la utani la ZIRO!!! Kwanini mlimuita hivyo na Kipanya alichora katuni nyingi za ZIRO. Mhe. Mkama anamjua sana Mhe. Sumaye. Hivyo amemjibu SAWASAWA na UPUMBAVU wake. Mbona wanawake tunapohubiriwa tusiwe wapumbavu hawasemi wametukanwa???


Hakuna shida hapo, message sent and delivered.

Queen Esther
Kwa kumjuwa sana hivyo na bado akamweka waziri mkuu kwa miaka kumi na huo upumbavu wake, je mpumbavu hapo ni nani??
 
Mkapa anamchukia sana Edward Lowasa kwani baada ya kuwa waziri mkuu alianza kupitia upya mikataba ya madini na alirudisha mgodi wa kiwira kwenye serikali.
Mgodi huo mkapa alijiuzia tsh milioni moja tu na alishindwa kuuendeleza kabisa.

Pia mkapa na magufuli walijiuzia nyumba za serikali kwa bei powa na mchakato uliofubikwa rushwa na usiri mkubwa.

Baada ya Rowasa kuanza kufatilia maswala hayo Kikwete ilifikia hatua ya kumtetea mkapa kwa kusema "MWACHENI MZEE WA WATU APUMZIKE.
NA baadae wakafanikiwa kumtoa madarakani lowasa kwa kumpakazia skendo ya richmond.

Ikumbukwe baada ya Lowassa kutolewa madarakani aliingizwa waziri mkuu Mizengo pinda Ambaye alifanya kazi muda mrefu na mkapa na mkapa ndiye aliyemshawishi Pinda aingie kwenye siasa na kumpendekeza kuwa awe waziri mkuu.

Pia waliingizwa maswaiba wengi wa mkapa CCM kama mangula.

Tofauti na lowassa Japokuwa alipitia kadhia nyingi Pindwa alilindwa sana na JK licha ya baraza la mawaziri aliloliongoza kupitia kafsha nyingi kama.
1. Hongo kwa wabunge kwa wizara ya nisharti na madini ili wapitishe bajeti
2. Operation Tokomeza
3 Ubadhilifu na matumizi mabaya ya fedha kutokana na mkaguzi mkuu wa serikali.
4. Wizi wa fedha za Escrow Ac.
 
Pumbavu yule ambaye jana alikuwa anazomea mafisadi leo anayakumbatia kwa sababu tu ameshikwa masikio na kuaminishwa upumbavu
 
Watu tunakuwa wasahaulifu sana. Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi(SUGU) kwa kumtaja jina, alimuita Waziri Mkuu MPUMBAVU bila ya kuwa na sababu yoyote ya msingi. Mbunge wa Ubungo, John Mnyika akamtukana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumtaja jina kuwa ni DHAIFU.
Inasikitisha sana kuona kauli ya Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Willium Mkapa kuwa baadhi ya wapinzni wanaosema wanataka kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa kutafsiriwa kuwa ni matusi kwa Wapinzani. Hivi ni mtanzania gani hajui Tanzania ilishatoka mikononi mwa Wakoloni?(Ilishakombolewa?)


Mzee Mkapa alitumia maneno sahihi kabisa kwa mtu ambaye anajitoa ufahamu wa ukweli wa jambo. Ni sifa gani ambayo inastahili kwa mtu anayetaka kulikomboa Taifa ambalo tayari lilishakombolewa? Anashindwa kweli kutumia hata maneno kama MABADILIKO na siyo UKOMBOZI?


wapinzani nawaonya msije mkakomalia kauli ya MKAPA na mkaacha kujikita kwenye agenda za msingi. Alichokisema Mkapa ni sahihi kabisa, Tanzania ilishakombolewa na kinachotakiwa ni MABADILIKO ambayo siyo lazima yaletwe na Wapinzani bali chamamchochote chenye MGOMBEA MWADILIFU na anayetokana chama chenye Sera safi na siyo UKOMBOZI.


wote tunaoamini Tanzania ni Taifa huru lazima tuungane na kauli ya MKAPA na pengine kauli hii iwe fundisho kwa wanasiasa wanaotumia maneno yanayowapotosha watanzania.
 
Siasa za tz bwana.. Kama movie, ngoja nivute handbrake niangalie kwa makini
 
Kama wewe ni msomi bila shaka ulikwisha wahi kuitwa kwenye usaili wa aina yoyote ile, je ulipo ulizwa udhaifu wako ni upi uliona tusi au alijimwaga na kuonesha madhaifu yako ili upate ajira? Ukinijibu hapo kuhusu Mnyika kumwambia kikwete ni dhaifu tutakwenda pamoja.

Endelea
 
mkapa anamchukia sana edward lowasa kwani baada ya kuwa waziri mkuu alianza kupitia upya mikataba ya madini na alirudisha mgodi wa kiwira kwenye serikali.
Mgodi huo mkapa alijiuzia tsh milioni moja tu na alishindwa kuuendeleza kabisa.

Pia mkapa na magufuli walijiuzia nyumba za serikali kwa bei powa na mchakato uliofubikwa rushwa na usiri mkubwa.

Baada ya rowasa kuanza kufatilia maswala hayo kikwete ilifikia hatua ya kumtetea mkapa kwa kusema "mwacheni mzee wa watu apumzike.
Na baadae wakafanikiwa kumtoa madarakani lowasa kwa kumpakazia skendo ya richmond

mwaka wa mungu kungea a wa tz. Haya tutasikia mengi na makongoro je?
 
Back
Top Bottom