Wana JF Heshima kwenu.
Mithali 26:5
Umjibu mpumbavu sawasawa na upumbavu wake; Asije akawa mwenye hekima machoni pake.
Aidha neno upumbavu limeandikwa zaidi ya mara 46 katika Biblia. Mfano :-
Mithali 14:1 Kila mwanamke aliye na hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu huibomoa kwa mikono yake mwenyewe.
Mithali 9:13 Mwanamke mpumbavu hupiga kelele, Ni mjinga, hajui kitu.
Aidha Rais wa kwanza wa TZ; Mwl Nyerere amekuwa akitumia neno hili mara nyingi sana. Huko ndiko Mhe. MKAPA alipojifunzia. (Nimeshindwa kuweka video clip msaada plz)
Mhe. Sugu alipotumia neno mpumbavu pale mjengoni UKAWA walimtetea. Leo kwao limetumika imekuwa nongwa kwenye mitandao. Kweli nyani haoni naniii yake.
Mhe. Mkapa ni Mkristo mzuri mwenye kusoma Neno la Mungu kila wakati. Alichofanya ni kujibu hoja ambayo ameipima na kuiona ni ya kipumbavu ili walioitoa wasijione wana akili.
Nani asiyejua Mhe. Sumaye alibatizwa jina la utani la ZIRO!!! Kwanini mlimuita hivyo na Kipanya alichora katuni nyingi za ZIRO. Mhe. Mkama anamjua sana Mhe. Sumaye. Hivyo amemjibu SAWASAWA na UPUMBAVU wake. Mbona wanawake tunapohubiriwa tusiwe wapumbavu hawasemi wametukanwa???
Hakuna shida hapo, message sent and delivered.
Queen Esther