Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

Elections 2015 Mzee Mkapa: Wanaosema Wanataka Kuikomboa Tanzania ni Wapumbavu na Malofa

CV YA Dr MAGUFULI , NGULI WA SAYANSI NA RAIS MTRAJIWA AWAMU YA 5
Dk. John Pombe Joseph Magufuli, alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato – wakati huo ikiwa Mkoa wa Kagera (sasa Mkoa wa Geita).
Ana Shahada ya Uzamivu ya Kemia (2006 – 2009) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Mwaka 1991 – 1994, alisoma Shahada ya Uzamili (Kemia) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, na baadaye Chuo Kikuu cha Salfordnchini Uingereza.

Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanzaya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1981 – 1982, alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.

Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa.

Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.

Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.

Mafunzo
Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.

Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.

Uzoefu wa kazi
Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Samaki; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).

Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato)

Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.

Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).
Dk. Magufuli amepata tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa.

Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Ameoa na ana watoto kadhaa.
[12:08, 27/08/2015] Ayub Cmn:
Pamoja na kuwa busy na mambo ya kazi za siasa, Uwaziri na Ubunge, Mheshimiwa Magufuli aliweza kusoma na kumaliza PhD yake pale UDSM jambo ambalo ni la kupigiwa mfano tofauti na Mbunge mmoja wa Upinzani aliyeshindwa kumaliza Shahada yake laini (BBA) hapo hapo UDSM miaka nenda rudi.BAADHI YA MACHAPISHO/PUBLICATIONS YA MTEULEMulokozi A. M.; Akwilapo, L.D.: Buchweishaija, J.; Magufuli J. P., and Kyobe, J. ¿Securing the Mechanism of the Decomposition of CaCO3 by the Thermodynamics of the Reaction¿, East and Southern Africa Environmental Chemistry Workshop, pp 71-83, 1st ¿ 5th December 2003, Dar es Salaam 5 Dec 2003
Magufuli, J. P., ¿Funding requirements for the EAC Road network project the East African Community Roads Development partners Consultative meeting 29th ¿ 30th April, 2003 Arusha Tanzania. 30 Apr 2003
Magufuli, J. P., (MP) PIARC First Delegate and Minister for Works of the United Republic of Tanzania.¿ Access to Mobility a basic Social Service, Special Trunk Roads project, Design and Build Tanzania model, XXIInd World Road Congress, 19 ¿ 25 October, 2003 Durban, South Africa. 25 Oct 2003
Mulokozi, A. M., Kyobe, Magufuli, J. P. and R. Whitehead. ¿A New Rate Equation for Solid State Decompositions and its application to the Decomposition of CaCo3. TCS Inaug. Conf. Proc., 11 ¿ 16 July, 1999, p162 ¿ 183. 16 July 1999
Magufuli, J. P., ¿Background of the Mtwara Development Corridor¿ Meeting of the head of States from Malawi, Tanzania, Zambia and Mozambique during the Rounding of the Mtwara Development Corridor, 15 December, 2004, Lilongwe ¿ Malawi.
 
Tumemsamehe; ni shauri ya Viroba!! tunasikia Chinga One kwa viroba na Konyagi hakamatiki!! ndio maana mashavu yameanza kumshuka; yametepeta! inaelekea figo zimeanza kuharibika; chezea konyagi wewe; mpaka yule bwana ashushe mikono ni sheeda!

Jana mzee Mkapa alimwaga radhi, CCM nayo ikamwaga radhi.

Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa, alipopata wasaa wa kuhutubia maelfu ya wanachama wa CCM waliokuwa uwanjani wa Jangwani, alirusha kijembe kwa wapinzani na kusema wanaosema wanatafuta ukombozi ni wapumbavu na malofa.

“Kuna vyama vinajifanya vinataka kuleta ukombozi, ukombozi uliletwa na ASP na TANU, hao wanaojiita vyama vya ukombozi ni wapumbavu, … ni malofa, nchi hii ilikwisha kombolewa na sasa inaendelea kuikomboa kwa kupambana ana umasikini, ujinga na maradhi na ndo kazi imekuwa ikifanywa na serikali zote zilizopita kuanzia ile ya awamu ya kwanza na hii inayokuja itafanywa na serikali ya Dk. Magufuli,” alisema.

Mzee niliyemzoea kwa hoja zenye mashiko na takwimu akageuka mlevi asiyejiheshimu.

Kweli ufalme wa CCM umefitinika.Kati ya mambo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakiitofautisha brand ya CCM na Upinzani ni kule kutumia lugha zenye staha,kuhubiri amani na kuiishi.Jana rasmi CCM imevunja ndoa yake na sifa hizi.

Sasa tunaanza kupata picha tukimtazama Makonda, baadae Nape,Wasira,Kamani,Job Ndugai na sasa Mkapa tunaona CCM mpya inayozaliwa; brand ya ngumi,matusi na lugha za mihemko.

Mimi niwaambie tu,busara na hekima ni tunu ila ujinga hafundishwi mtu.Ni suala la kuamua tu!

Magufuli karibu UKAWA,you are a good manager but not a leader.

BURIANI CCM!

Last edited by a moderator:
kunya anye kuku...akinya bata kaharisha sio??? mtasubiri saana ...endeleeni kuweka vikwazo vya kijinga wakati wenzenu wapo busy ....kumwaga sera ...nyie mko busy kulalamika mmetukanwa wakati muda umebaki mchache...endeleeni kulalamika ...lazma mkae oktoba 2015 #hapakazitu
 
Ndugu Zangu,

Nilikuwepo pale Viwanja vya Jangwani. Nilipomsikia Ben Mkapa akiwaita wapinzani ' Wapumbavu na Malofa', basi, nikajua hiyo ndio ingekuwa ' Habari ya Mjini'. Nilikuwa sahihi. Ni kwa vile aliyetamka hayo alikuwa Ben, Rais Mstaafu.
Na hakika, mitaani huko nimekutana na watu wanaohangaika sana hata kuingia kwenye kamusi ya Kiswahili kuona tafsiri ya maneno aliyotamka Ben, kama ni matusi au la!
Katika hili, yaweza pia kusemwa, kuwa Ben amechangia kupromoti lugha ya Kiswahili.
Na hakikatafsiri zaweza kuwa nyingi, na hasa katika wakati huu wa joto la kisiasa linalopanda. Tukianza na Lofa, ina tafsiri ya mtu aliyefilisika,kupungukiwa mtaji na hata mwenye kutembea akipoteza muda. Yaweza pia kutafsiriwa kuwa kufilisika kisiasa. Inategemea na imetamkwa katika muktadha gani. Chimbuko lake ni kwenye kimombo; ' wasting time'- Are you loafing, you better hurry up and do! ....
Naam, mapambano ya kisiasa, na hususan kwenye kampeni za uchaguzi huwa na sura ya mikakati inayyofanana na ya mapambano ya kijeshi. Na kwenye vita kinachopelekea ushindi ni vitu vitatu; Silaha bora, uwezo wa wapiganaji na propaganda.
Huenda si wengi wenye kukumbuka kuwa Ben Mkapa alipata kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje kwenye kipindi ambacho Tanzania ilikuwa vitani dhidi ya Idd Amin.
Ni Ben Mkapa aliyeongoza vita vya propaganda dhidi ya Idd Amin, dunia ikaaminishwa kuwa Tanzania ilikuwa na sababu, uwezo na nia ya kumpiga Idd Amin. Ni kwenye kipindi kile cha vita, na kazi ya fasihi kwenye lugha ya vita ilifanywa na watu wa aina ya Ben Mkapa na Paul Sozigwa na iliyotumika vema kwenye propaganda za kimapambano. Ndio, ikamfanya Idd Amin aonekane si lolote si chochote.
Nini basi tofauti ya Mjinga na Mpumbavu?
Marehemu Mzee Jongo alipata kutamka; ” Kusoma sio kuufuta ujinga, bali ni kuupunguza”. Kila mwanadamu ana ujinga wa jambo moja au mia moja. Kuwa na ujinga wa jambo si kosa, hata Profesa anaweza asijue namna ya kuchochea kuni za kuchomea hindi bichi likachomeka. Kijana wa darasa la saba anaweza kuwa hodari wa jambo hilo kumshinda Profesa.
Lakini, upumbavu ni ile hali ya mwanadamu kufanya jambo isivyotakiwa huku akiwa na uelewa wa namna ya kufanya inavyotakiwa. Huo ndio upumbavu.

Hoja ya Ben kama ametukana au la, inabaki kuacha uwanja wazi wa tafsiri kwa anayetaka kutafsiri anavyotaka yeye, bila kuacha kuzingatia, kuwa tumo kwenye joto la kisiasa linalopanda. Na ndio utamu wa fasihi pia..!
Ukumbi wenu wajumbe kujadili.
 
Ndugu Zangu,

Nilikuwepo pale Viwanja vya Jangwani. Nilipomsikia Ben Mkapa akiwaita wapinzani ' Wapumbavu na Malofa', basi, nikajua hiyo ndio ingekuwa ' Habari ya Mjini'. Nilikuwa sahihi. Ni kwa vile aliyetamka hayo alikuwa Ben, Rais Mstaafu.
Na hakika, mitaani huko nimekutana na watu wanaohangaika sana hata kuingia kwenye kamusi ya Kiswahili kuona tafsiri ya maneno aliyotamka Ben, kama ni matusi au la!
Katika hili, yaweza pia kusemwa, kuwa Ben amechangia kupromoti lugha ya Kiswahili.
Na hakikatafsiri zaweza kuwa nyingi, na hasa katika wakati huu wa joto la kisiasa linalopanda. Tukianza na Lofa, ina tafsiri ya mtu aliyefilisika,kupungukiwa mtaji na hata mwenye kutembea akipoteza muda. Yaweza pia kutafsiriwa kuwa kufilisika kisiasa. Inategemea na imetamkwa katika muktadha gani. Chimbuko lake ni kwenye kimombo; ' wasting time'- Are you loafing, you better hurry up and do! ....
Naam, mapambano ya kisiasa, na hususan kwenye kampeni za uchaguzi huwa na sura ya mikakati inayyofanana na ya mapambano ya kijeshi. Na kwenye vita kinachopelekea ushindi ni vitu vitatu; Silaha bora, uwezo wa wapiganaji na propaganda.
Huenda si wengi wenye kukumbuka kuwa Ben Mkapa alipata kuwa Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje kwenye kipindi ambacho Tanzania ilikuwa vitani dhidi ya Idd Amin.
Ni Ben Mkapa aliyeongoza vita vya propaganda dhidi ya Idd Amin, dunia ikaaminishwa kuwa Tanzania ilikuwa na sababu, uwezo na nia ya kumpiga Idd Amin. Ni kwenye kipindi kile cha vita, na kazi ya fasihi kwenye lugha ya vita ilifanywa na watu wa aina ya Ben Mkapa na Paul Sozigwa na iliyotumika vema kwenye propaganda za kimapambano. Ndio, ikamfanya Idd Amin aonekane si lolote si chochote.
Nini basi tofauti ya Mjinga na Mpumbavu?
Marehemu Mzee Jongo alipata kutamka; " Kusoma sio kuufuta ujinga, bali ni kuupunguza". Kila mwanadamu ana ujinga wa jambo moja au mia moja. Kuwa na ujinga wa jambo si kosa, hata Profesa anaweza asijue namna ya kuchochea kuni za kuchomea hindi bichi likachomeka. Kijana wa darasa la saba anaweza kuwa hodari wa jambo hilo kumshinda Profesa.
Lakini, upumbavu ni ile hali ya mwanadamu kufanya jambo isivyotakiwa huku akiwa na uelewa wa namna ya kufanya inavyotakiwa. Huo ndio upumbavu.

Hoja ya Ben kama ametukana au la, inabaki kuacha uwanja wazi wa tafsiri kwa anayetaka kutafsiri anavyotaka yeye, bila kuacha kuzingatia, kuwa tumo kwenye joto la kisiasa linalopanda. Na ndio utamu wa fasihi pia..!
Ukumbi wenu wajumbe kujadili.

Asante kwa upumbavu wako
 
Yule kijana anaeonekana kama mzee wa miaka 90 jana kasema anachukuwa wanawake zenu akawalishe bata ngurdoto na nyie mnachekelea tu. Kisha wanunua wanaume sasa mambo laini kabisa, mna kauli ya kumzuwia?

CCM mna bahati sana kupata hata mtu wa kuwazika. Kukosa wa kukuzika is a bad anticipation. Furahini UKAWA watawakamua mavi ya ngama fresh kabisa na kuwazika ipasavyo Oct 25
 
CCM mna bahati sana kupata hata mtu wa kuwazika. Kukosa wa kukuzika is a bad anticipation. Furahini UKAWA watawakamua mavi ya ngama fresh kabisa na kuwazika ipasavyo Oct 25

Vipi bibie, upo safari ya ngurdoto. Msisahau kututumia picha za huko.
 
Nliwah kusema mapema sana suala la UKAWA kujipanga na kuangalia sana wanaohamia UKAWA toka CCM wengi walisema mimi ni chizi kama ambavyo jija langu lilivyo. Nliwaambia Muogope sana CHIZI ANAYEJITAMBUA KULIKO MTU MWENYE AKILI ASIYEJITAMBUA KUWA ALIPEWA AKILI HALAFU HATUMII.
Juzi hapa nlisema kuwa MKAPA aliwaita UKAWA/WAPINZANI ni WAPUMBAVU NA MALOFA. nikataka kusikia watajibu nini nashukuru kwa ASILIMIA 95 WALIKUBALI. Nikaanza tena kuwa na hofu. OGOPA SANA WAPUMBAVU NA MALOFA Wanaojikubali kuwa ni kweli ni wapumbavu na laofa kuliko wale wanaokataa. LEO naleta mambo kadhaa ya kuangalia kwa makini sana UKAWA.
1. UKAWA inaweza kuvunjika mara baada ya UCHAGUZI au hata kuwa na migogoro Mingi sana Tunapoelekea kwenye Uchaguzi. sababu kuu ni kuna wana UKAWA wanaohujumu chama kwa kiasi kkubwa wakiwa wanafanya kazi kwa maelezo toka CCM usalama wa taifa
2. Kuna watu waliokuja UKAWA kwa kutafuta MADARAKA/ hasira za CCM. kulikuwa hakuna haja kumpokea na kumpa nafasi ya Kugombea Ubunge(nisahihishwe kama si kweli) mtu kama Said Nkumba kwa sababu Nkumba alikuwa ni mmoja wa tu wenye upeo mdogo sana wa kufikiria na kuamua mambo muhimu, akina nkumba wengi bado wapo CDM.Waangaliwe watu kama Akina Tambwe Hiza hawa si wanasiasa ni wanamaslah... Tambwe Hiza alikuwa wapi miaka yote hii aje kuibukia leo Mkutano wa Ukawa? Ni rahisi tu.. CCM walimtema tambwe hiza baada ya Kumtumia sana na baadaye akakosa matumizi. huyu alichoka sana kimaisha... sasa anarudi kupitia Ukawa na kuna siku atarudi tena CCM kiukweli hana mchango wowote kwa Harakati hizi za Ukombozi awe ni mtu wa kawaida tu.
3. UKAWA jipangeni kuzungumzia ADHA WALIZO NAZO WANANCHI msijishahau mkaingia kwnye siasa chafu za CCM. huko CCM watawashinda kwa kuwa wana uzoefu mkubwa wa siasa chafu kwa kutumiw watu wake mbumbumbu wasiojilewa. inabid mjitofautishe nao. ni muhimu sana kujitofautisha na CCM. maana wanawavuta muelekee uelekeo wao kwa kutaka kuwatoa kwenye mambo ya muhimu ya wananchi.
4. Haya majimbo mawili ambayo hamjayatolea maamuzi mpaka sasa yatawathiri hasa jimbo la segerea ambalo ningeshauri abaki nalo Mtatiro huyo dada mngemtafutia kazi nyingne but jimbo la segerea haliwezi hata kidogo.
5. Mmejipanga vipi ikiwa CCM WATAIBA KURA NA KUJITANGAZA WASHINDI? hapa ndipo mtakapopoteza wanachama wengi sana ikiwa hamtakuwa makini katka hili. na baada ya hapa UPINZANI utakufa maana hakutakuwa na WATU WENYE KUAMINI TENA UPINZANI. WENGI wataacha SIASA au kurudi CCM.

haya mtayakataa, mtayapinga kwa ukali na kebehi na kunidhihaki. tuombe uzima maana mtakuja kuyakumbuka.
 
UKAWA ni moto wa mabua
Ni suala la uwezo binafsi wa mtumiaji. kuna mahala huko vijijini wakina mama hutumia moto wa Mabua kupikia. Wewe ukiona moto wa mabua hauwezi kuleta ufanisi au hasara jua uwezo wako wa kujiongeza ni mdogo!!
 
zuzu, chizi... mharoooooooo
 
zuzu, chizi... mharoooooooo
Huu uliotoa ni utabiri wa kweli. Mwisho wa Chadema umefika. Wamekaribisha nyoka wakidhani watabaki salama. Wamsubiri Mzee Mako wa chandimu aje awachane kama alivyoanza kumchana Sumuye
 
Watalumbana hao cdm sana. Na wasishangae huyo mgombea wao akajitoa na kusingizia kuwa madaktari wamemshauri asijihusishe na siasa kwa ajili ya afya yake. Huyu babu tunamjua sis ni msaninii. Kama anasema kuwa hawezi kuhama ccm na baadae kidogo anhama na kusema ccm si baba wala mama yake. Huyo mnamwamini. Hongera Mzee wetu Marandoo na wengine ambao kwa macho yao wanadhani mko nao kumbe mnatafuta info na kuzifanyia kazi. Mwisho wa cdm na ukawa umewadia hata kabla ya uchaguzi mkuu
 
Back
Top Bottom