Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Huu ndio unaitwa UDINI. Why Mapadri? Uhuru wa nchi hii haukutafutwa kwa makundi kiasi iandikwe Historia ya Mapadri, Mashehe, Mabudha, Wapemba, Wageni, Wazawa na wengineo.
Mwana...
Umewataja mapadri katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.
Wangelikuwapo ningeliandika historia yao lakini kwa bahati mbaya hawakupo.

Kadhalika hawakuwapo mabudha, Wapemba ila wageni walikuwapo kama Dome Budohi (Kenya) na Denis Phombeah (Nyasaland).

Phombeh kadi yake ya TANU ni no. 5 na Budohi ni no. 6.
Unaweza kusoma historia ya Denis Phombeah hapo chini:

 
Inaelekea wewe ni kizazi baada ya uhuru ila kwa wale ambao walikuwa na akili zao ingawa watoto walishuhudia mengi na anachoandika Mohamed Said kwa yeyote yule alizaliwa miaka ya 40 na 50 na kukulia dar anaelewa.

Mimi ninakumbuka zile enzi ambapo bibi Titi na wenzake walikuwa wanapita nyumba hadi nyumba kuhamasisha akina mama kuingia Tanu.

Na ninamkumbuka mwalimu kipindi kile ambacho alikuwa anakuja mtaa wa sukuma na mafia yalipokuwa makazi ya Yanga kwenye vikao pamoja na wazee wetu. Wacha kupotosha wenzako.
Nimepotosha vipi hapo mkuu. Sawa walikua wanahamasisha, sasa niambie nini kilitokea adi akafahamika JK ndio kaletaa uhuru.. hawa wengine kiliwakuta nini?
 
Nimepotosha vipi hapo mkuu.. Sawa walikua wanahamasisha.. sasa niambie nini kilitokea adi akafahamika JK ndio kaletaa uhuru.. hawa wengine kiliwakuta nini..?
Ninafahamu fika kuwa wewe unataka malumbano kwani nina uhakika unafahamu chachu za uhuru walikuja nazo baba zetu baada ya kutoka WWII.

Hao ndiyo waliokuwa wanahrakati waliokuwa wanahamasisha wazazi wao kuwa wakati wa mabadiliko umefika na ni budi kupigania nchi yetu.Unafahamu kuwa TAA ilikuwepo kabla hata mwalimu kufika mjini Dar?

Mimi sikulaumu sana maana historia ya nchi hii imeandikwa kisiasa zaidi kuliko uhalisia na ndiyo maana watu maarufu kama kina mzee Chamwenyewe na wengine wengi hivi leo huwezi kuwakuta kwenye machapisho hayo. Na kwa wale kina mama ambao wengine waliridhia hata kupewa talaka na waume zao kwa sababu ya kutumia muda mwingi kwenye siasa hawajulikani.
 
Abunwasi,
Mm sijataka kuanzisha malumbano.. swali la msingi ni ilitokea nini hao wengine wakashindwa kua recognised kama waliotuletea uhuru.. bali ni wapigania uhuru..
 
Namimi naomba nikuulize unadhani kwanini afahamike JKN kama aliyetuletea uhuru ilihali kulikua na watu walioanza kabla..?
Da 'Vinci, mwanangu una hoja dhaifu mno yani umeniangusha kwa ili bandiko lako man yaani unataka kuniambia kwamba since 1920 hakuna watu ambao walikuwa wanapambania uhuru its seem that watu walikuwa wamerelax alafu mzed baba Nyerere ndo akaje iyo 1947 akaanzisha harakati za mapambano kiukweli mzee hujawatemdea ukweli wapigania uhuru wa tanganyika mzee yaani daaah Da vinc nimeshusha baadhi ya nyota zako una hoja dhaifu mno mno mzee mohamed alicho andika ndo ukweli halisi kabisa.

Hata siku moja usije ukajidanyanga kwamba eti Nyerere ndo aliaznisha harakati za uhuru no wapo walishakomaa sana uko kitambo before ya KJN ila historia zao zimefutwa tu mzee ili kmtukuza na kumkuza uyu JKN lakini Ukweli si kwamba yeye ndo pekee alipigania uhuru jamaa harakati alizikutia kati watu wshauawa sana washakatwa sana viungo washapotezwa sana na wasiojulikana wa kipindi icho ivyo @Da vinc pls kama historia inakuwa haiko vizuri kichwani pls ni vyema pia kusoma na kuuliza pia ili kuapata maarifa.
 
Mm sijataka kuanzisha malumbano.. swali la msingi ni ilitokea nini hao wengine wakashindwa kua recognised kama waliotuletea uhuru.. bali ni wapigania uhuru..
Hivi mbonai George Washington ambaye ndiye baba wa Taifa USA alikuwa anavuma sana,? mbona yeye alikuwa anavuma na General Nathanael Greene hajulikani kabisa?
 
Kabla ya hilo kundi kudai uhuru watu walikuwa wanafurahia kunyonywa..., Tangia muarabu aanze kuja kuuza ndugu zetu kama watumwa watu walikuwa wananungunika na kugombana kutoka katika hali ya Unyonyaji.., Mjerumani alivyokuja wapo kina Mkwakwa n.k.

Sasa kusema kwamba hilo kundi ndio lilikuwa na wazo la kudai uhuru na Nyerere alikuwa tu pugu anashika chaki.., basi hilo kundi lisingemfuata Nyerere bali lingemfuata jamaa yoyote pale mtaani...,
Inaelekea hata hujui usemalo. Na hao waarabu ambao unasema walikuwa wanawauza ndugu zako kama watumwa. Je, hao watumwa walikuwa wanawapata wapi?

Ni machifu wetu wenyewe ndiyo walikuwa wanakamata hao watumwa aidha mateka wa vita au vinginevyo ndiyo walikuwa wanabadilishana na bidhaa ambazo waarabu walikuwa wanaziuza na waarabu hao nao kuwauza kwa wanunuzi ambao nao walikuwa maajenti wa wazungu.
 
Mkuu wewe ni mwepesi sana kujibishana na mzee Mohamed, huyo ni level nyingine we endelea kutuletea habari za kutunga za kina tesla. Narudia tena mzee said humuwezi sio level yako.
Daaah mi mwenyewe mshikaji nimeshangaa sana leo yaani jamaa kaja na hoja dhaifu mno, mno, mno kupitiliza. Nina mashaka mawili, either jamaa acc yake imedukuliwa ama jamaa pasword zake kampa demu wake nando anayeandika hii nyuzi huu sio uqezo wa Da Vinc ata kidogo.

napinga kabisa yaani unawezaje kusema eti nyerere ndo kaleta uhuru peke yake wakati uko nyuma kuna wana walishakatwa sana mikono ,miguu na wajeruman na waingereeza hawa wana walijaribu kupinga na dno walianziaha izo harakati sema yule mzanaki kwa kupenda kwake sifa aliona awafute wenzie ili kwenye historia abaki yeye peke yake kama ambavyo unaona Kajamaa kalijaribu kuifuta historia ya KAMBONA na SOkOINE ABDU JUMBE ila wadau wakagoma kabisa na ndo mapka leo mnaona tunziona historia za hao wadau kwenye vitabu na kwenye written documents kifupi uyo ticha hakupenda watu wenye kumchallenge yaani yeye alikuwa napenda watu wa dizaini ya kabudi wale wa kusema ndio mzee ka kila kitu ila wale waliokuwa wakijielewa jamaa wengi kawaua na kzofuta histoeia zao mazima


Da vinc kuna mengi huyajui ambayo yako nje ya uwezo wa akili yako kufikiria ni vyema kujifunza na kuuliza hii itakusaidia sijapenda ..ili bandiko lako ni la ajabu mno kuwahi kuandikwa na mtu ninaye muheshimu kama wewe
 
Mohamed Said,
Na miaka 8 baadaye uhuru ukapatikana.

Haiingi akilini kusema JKN aliiletea Tanzania Uhuru peke yake isipokuwa kama kiongozi wa kikundi/chama cha wapigania uhuru credit zikaenda kwake.

Na ni kweli kwani yy ndiye aliyekuwa mstari wa mbele kunegotiate na Waingereza, na hata baada ya hapo ni yy ndiye aliyeonekana kupigania nchi nyinginezo za kusini mwa africa pia kujikomboa. Hivyo historia imebaki ikimmulika yeye zaidi.
 
Da ' Vinci,
Ahsante sana kwa kuniandikia.
Hakika mimi nimeandika historia ya Waislam jinsi walivyokuwa mstari wa mbele katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika wala sikatai na wala sijuti kwa kufanya hivyo.

Wengi wameumizwa na historia hii kwa kuwa hawakuwa wanaijua, historia waliokuwa wanaijua ni ile historia rasmi ambayo ndiyo iliyokuwa imepasishwa na kusomeshwa kuanzia shule za msingi hadi Chuo Kikuu.

Hii ndiyo historia niliyoikuta mimi ikisomeshwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam nilipokuwa mwanafunzi na nilikuwa nawashangaza hadi walimu wangu ninapowaambia kuwa historia hiyo ina upungufu mkubwa.

Laiti mimi nisingeliaandika kitabu cha ''Maisha na Nyakati za Abdul Sykes...'' historia hii ilikuwa imeshafutika na kupotea kabisa na hakuna jamii katika ulimwengu huu ambayo inaweza kukubali au kuvumilia kuona historia yake inafutwa.

Hakuna mahali popote ambapo mimi nimedogosha mchango wa Julius Nyerere katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika na laiti ningelikuwa mjinga nikafanya hivyo ningekiua kitabu changu kwani wasomaji wangenipuuza.

Nilichofanya mimi ni kueleza kuwa ikiwa ni historia ya TANU basi haiwezekani kuanza na Julius Nyerere 1954 itabidi turudi nyuma hadi 1924 na tusome mswada wa Kleist Sykes alioandika kabla ya kifo chake 1949 akieleza historia ya African Association yeye akiwa mmoja wa waasisi wa chama hicho (mswada huu mwaka wa 1973 ukawa moja ya sura ya kitabu kilichohaririwa na John Iliffe, ''Modern Tanzanians).

Katika mtiririko wa historia hii kuna wazalendo wengi kama Hassan Suleiman na Ali Juma Ponda, Hamza Kibwana Mwapachu na wale madaktari watano - Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Wilbard Mwanjisi, Dr. Michael Lugazia na Dr. Luciano Tsere.

Pamoja na hawa ndipo wanapoingia Abdul Sykes na mdogo wake Ally katika historia ya TAA, TANU na harakati za kudai uhuru na ndipo pia nilipotumia nyaraka waliazokuwanazo kuanzia miaka ya 1920 zinazoeleza na kuthibitisha historia yao katika kuunda TANU na mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kwa nini historia hii ilifutwa swali hili nitakuachia wewe ulijibu.
Naamini hujusikii vibaya kwa kuandikwa historia hii.

Ama kuhusu manung'uniko ya Waislam yapo na si mimi peke yangu ambae nimeandika kuhusu tatizo hili.

Somo hili limeandikwa na Bergen (1981), Sivalon (1992) na Njozi (2002) ingawa kitabu cha Njozi kimepigwa marufuku.

Kwa nini kitabu cha Njozi kimepigwa marufuku badala ya serikali kujibu yaliyosemwa hili swali pia nakuachia wewe ulijibu.

Tatizo la udini tunalo nchini na serikali inalijua na Waislam hawajajificha katika kulieleza tatizo hili na linafahamika.

Ikiwa wewe huamini kuwa lipo kwangu ni sawa pia.
Kughitilafiana kwa binadamu katika fikra hili haliepukiki.

Sina tatizo na kutambuliwa kwa Nyerere kama shujaa wa uhuru wa Tanganyika na narudia tena kusema kuwa laiti ningelikuwa mjinga na kudogosha mchango wa Mwalimu Nyerere katika historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika kitabu changu kingelikufa mapema sana.

Kitabu kimepokelewa vyema kote katika Vyuo Vikuu wanakosemesha African History na baadhi ya vyuo hivi wamenialika kuzungumza katika vyuo vyao kwa mnasaba wa kitabu hiki nilichoandika.

Kitabu kimepata ''review,'' tatu ndani ya Cambridge Journal of African History na kimechapwa kama ''series'' katika, The East African Magazine (Nairobi) na katika baadhi ya magazeti hapa nyumbani.

Kitabu hiki kinatambulika kama ''corrective history,'' yaani imesahihisha historia ambayo kwa bahati mbaya ilikuwa na makosa.

Wako waliopendezwa na kitabu changu na ndiyo maana sasa tunakwenda toleo la tatu Kiingereza na la nne Kiswahili.

Halikadhalika wako ambao hawakupendezwa na kitabu changu wangependa historia ibaki kama ilivyokuwa zamani kwa kufuta historia za wazalendo wengine katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ibakie historia ya Mwalimu Nyerere peke yake.

Muhali wa hili ni kuwa wale waliokuwa na Mwalimu Nyerere katikaTANU mimi ni wazee wangu kutoihifadhi historia yao ni kujidhulumu mimi mwenyewe na kizazi changu.

Unaweza kuisoma historia ya babu yangu Salum Abdallah katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika hapo chini:



Hata wewe ungelitoka katika mifupa ya wazee kama wangu usingestahamili kuona historia yao inafutwa.
Swallow Abdul Sykes alipokuwa antique Mchango Wa kupigania uhuru Alicia kama musical aunt mdanganyika!vipi hao madaktar 5 wore no waislam!kwa tusingumzie utanganyika Wa nyerere bali tuungalie Mchango wake kwa mtazamo Wa ukatoriki?
 
ankai,
Yes, Leicester City ilikuwepo miaka mingi ikipambana kuwania ubingwa, lakini ni mpaka alipoiongoza Claudio Ranieri ndio ilitawazwa kuwa mabingwa wa EPL. Kwa maneno yaliyonyooka, Claudio Ranieri ndio ameipa Leicester City ubingwa kwa uongozi wake.
 
Sidhani kama kuna mahali mzee Mohamed anapotosha, anachofanya mzee huyo ni kuifungua historia yote kama ilivyo.

Ndiyo maana anatambua mchango wa watu wa dini nyingine walioshiriki kikamilifu kudai uhuru, akiwemo Dr Vedasto Kyaruzi, John Rupia, Kasela Bantu, Paul Bomani, Julius Nyerere nk.

Lakini kuna ukweli mchungu ambao wengi wetu tunaukwepa.

Kwamba zama za kudai uhuru kulikuwa na mahusiano ya karibu baina ya umishionari na Serikali za kikoloni, kwahiyo kwakuwa harakati zenyewe zimeasisiwa maeneo yenye waislam wengi, ilikuwa lazima kuwatenga baadhi ya watu waliokuwa karibu na wamishionari ili harakati za uhuru zibaki salama.

Hivyo, utaona alichokuja kufanya mwalimu ni kiviunganisha vyama vilivyoasisiwa zamani na ambavyo vyote vilikuwa na nia moja ya kuikomboa Tanganyika. Kwa kauli mbiu yake ya "Umoja ni nguvu, utengano ni udhaifu"

Kwa sababu hiyo, ingawa mwalimu ametoa mchango wake, lakini nyuma yake kulikuwa na kundi kubwa la watu ambalo historia inalazimishwa ili wasahaulike
 
Utumwa ilikuwa ni biashara ya kimataifa, biashara hii haikufanywa Tanganyika pekee, wala watumwa hawakuwa wafrika pekee, nchi nyingi Duniani zimezalisha watumwa ikiwemo nchi za Ulaya.

Vinginevyo waarabu walinunua watumwa Afrka na kwenda kuwauza barani Ulaya na Amerika ambako ndipo kulikokuwa na soko kubwa
Kabla ya hilo kundi kudai uhuru watu walikuwa wanafurahia kunyonywa..., Tangia muarabu aanze kuja kuuza ndugu zetu kama watumwa watu walikuwa wananungunika na kugombana kutoka katika hali ya Unyonyaji.., Mjerumani alivyokuja wapo kina Mkwakwa n.k.

Sasa kusema kwamba hilo kundi ndio lilikuwa na wazo la kudai uhuru na Nyerere alikuwa tu pugu anashika chaki.., basi hilo kundi lisingemfuata Nyerere bali lingemfuata jamaa yoyote pale mtaani...,
 
Inaelekea hata hujui usemalo. Na hao waarabu ambao unasema walikuwa wanawauza ndugu zako kama watumwa. Jee hao watumwa walikuwa wanawapata wapi??? Ni machifu wetu wenyewe ndiyo walikuwa wanakamata hao watumwa aidha mateka wa vita au vinginevyo ndiyo walikuwa wanabadilishana na bidhaa ambazo waarabu walikuwa wanaziuza na waarabu hao nao kuwauza kwa wanunuzi ambao nao walikuwa maajenti wa wazungu.

Utumwa ilikuwa ni biashara ya kimataifa, biashara hii haikufanywa Tanganyika pekee, wala watumwa hawakuwa wafrika pekee, nchi nyingi Duniani zimezalisha watumwa ikiwemo nchi za Ulaya.
Vinginevyo waarabu walinunua watumwa Afrka na kwenda kuwauza barani Ulaya na Amerika ambako ndipo kulikokuwa na soko kubwa
Nani alikuwa mfanyabiashara wa watumwa maarufu katika Arab Slave Trade AKA East African Slave Trade.

Abunwasi unaamini watumwa wote walikuwa mateka and who was behind hao machifu ? Na ni machifu gani walitajirika sana kwa hii biashara kuwazidi hawa ma-sultani

All in all my point is katika kudai uhuru huwezi kusema Nyerere alikutana na wadau fulani ndio wakamfundisha kudai uhuru tangia enzi za kale watu wanaohisi kunyonywa wamekuwa wakidai uhuru wao.
 
Msisitizo wangu mkubwa ni kuwa hata Waafrika hasa machifu walihusika sana kwenye biashara ya utumwa.
 
Mohamed Said,
Niwe muwazi sana katika hili na tuvumiliane katika kutoa hoja zetu ila kiukweli wapo baadhi ya watu hupenda yafuatayo :-

1: recognition: mi nafikiri kuwa ipo siku ya kwenda kanisani au msikitini kuswali na ukitoka hapo unafanya mambo yasiyo ya dini. Hivyo kuanza kutaja watu wenye dini ya kiislam katika harakati za kupata uhuru basi huu ni ubaguzi kwani hata sasa serikali ina waislam na wakristo lakini katika shughuli za kijamii hatuhusishi dini. Ni sawa na zanzibar, ndugu okelo ameipa uhuru kwa njia ya mobilisation na kutokn na mambo haya haya ya kibaguzi, hazungumziwi kisa sio muislam.

2: suala la kutafuta uhuru usingeweza kupatikana nchini tanganyika kwa kipindi kile hadi kumfuata mwlm nyerere, ilitokana na waliokuwa wanataka kupigania uhuru hawakuwa wasomi, ambao ndio hao wengi wao asilimia kubwa walikuwa ni waislam na hivyo ombwe la kwenda kuonana na wazungu ni lazima uwe msomi.

Pia waliomchangia nyerere kwenda huko na mengineyo mengi aliyoyafanya hadi akashtakiwa kwa uchochezi, na mahakama ya tanganyika ilisema kuwa nyerere alikuwa na Akili sana, na akipigwa faini na watanganyika wengi walimchangia hela Bila kujali wa dini gani lakini huwez sikia kwa mtu ambae anazungumzia masuala ya dini katika kuleta uhuru.

Mi nadhani kama mwandishi anataka kuzungumzia suala la muungano, achaneni masuala ya dini maana hakuna dini iliyohusika katika kufanikisha uhuru wetu ila walioshirikiana wote ni watanzania na si dini imetumika. Huu mgogoro unawez kutufanya tuhamasike katika masuala ya dini kwa kigezo tu kuwa dini flani imeleta uhuru.

Labda mfano kwa sasa kwa kazi anazofanya mkuu wetu wa nchi, tunawez sema kuwa ni ukristo ndo umefanya haya yote? Tujiaminishe kwa Hilo? Maana wapo baadhi ya waislam wamepewa nchi na ni tofauti ya maendeleo tofauti na awamu hii?

Kwa kifupi watu walioleta au kupigania uhuru ni ndugu zetu na tuwataje majina yao na si kwa dini zao, mengineyo in uchochezi na ni ujinga usio na kifani.
 
Back
Top Bottom