Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Mizy,Shukrani ziende kwa waanzilishi wa harakatii ila tunamthamini alietufikisha tulipokua tunahitaji (FREEDOM) ..
Tunakubali sawa japokuwa JKN sio muhasisi wa harakati ila amepokea kijiti na kukifikisha sehemu ambapo wahasisi walishindwaa kukifikisha na hapo ndo utambuzi, heshima na uweledi wa JKN unatofautika na watu wengine waliokuwepo kweny harakati.... .
Hakuna anaeweza kukataa mchango wa Mwalimu Nyerere katika historia ya uhuru.
Lakini historia hii ilipooza sana pale ilipokuwa imefunika wazalendo wengine katika kupigania uhuru.
Leo historia hii inanoga unapoisoma na kujua kuwa kulikuwa na mazungumzo kuhusu Nyerere kuingizwa katika uongozi wa TAA nyumbani kwa Hamza Mwapachu Nansio, Ukerewe mapema mwaka wa 1953 na waliokuwa katika mazungumzo hayo walikuwa Hamza Mwapachu mwanyeji wao na wengine walikuwa Abdul Sykes aliyekuwa Katibu na Kaimu Rais wa TAA aliyefuatana na Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Msomaji atajiuliza huyu Hamza Mwapachu aikuwa na nguvu kiasi gani kiasi kuwa watu wafunge safari kutoka Dar es Salaam kumfuata Nansio kusikiliza fikra zake?
Msomaji atajiuliza Abdul Sykes alikuwa nani na atajua nafasi yake na ya baba yake katika siasa za kikoloni nk. nk.
Kwa namna hii historia ya Tanganyika itakuwa inafahamika vizuri.
Kutaka kuwa historia hii atajwe Nyerere peke yake hii ni sawa na nchi kuihujumu historia yake.