Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Waliotoa pesa mchango wao unathaminiwa lakini naomba nihoji swali...

Je kabla ya kufatwa na JKN kuombwa pesa... hizo pesa walikua wanazitumiaje katika kutukomboa watanzania....? Ndo tunagundua unaweza ukawa na resources lakini usiwe na akili ya kuzitumia...

Ila JKN anazungumziwa kuliko wengine sababu ndo alikua ni monitor kama nilivyosema awali mawazo yake ndo yalikua chanya na upeo mkubwa wa kujua wakati sahihi wa kufanya jambo fulani sahihi kuliko wengine waliokua katika harakati.... Mfano mzuri ni kama jeshini general haendi vitani lakini strategies zake ndo zinazodetermine matokeo ya vita kwa maana hiyo. Basi aliebeba mtutu akaingia vitani ana mchango lakini hautazungumziwa kama wa yule general alietoa mbinu za kumshinda aduii.

Ndio the same kwa Tanzania kila mtu alikua na mchango katika uhuru wetu kuanzia parties za labour watu kama kina mkwawa kina kinjekitile, wote kambona,bomani, bibi titi... wanazungumziwa kwenye struggle lakini key player aliefanikisha ni nyerere ndo maana historia yake inameza historia za wengine sababu yeye ndo alikua mstari wa mbele kufanikisha jambo... Ila wewe unaforce habari za babu zenu na huyo mzee said ziwe popular na kuonesha bila wao nyerere si kitu.. Kwa pamoja hatutakubali na kamwe hamtoweza kubadilisha misimamo yetu juu ya kile tunachokiamini... Kwanza tunatumai Mungu ameilaz roho yake JKN sehemu pema huko juu mbinguni... Hammaz,
 
Kumbuka uingereza ilikuwa inamandate tu ya kuwepo Tanganyika kwa niaba ya UN,
waingereza walipanga kuondoka na kati ya watu waliofikiria kuwaachia nchi mmojawapo na Msukuma Kidaha makwaia,huyu alipendelewa sana na malkia ili aje kuwa rais wa Tanganyika,

halafu kuna J nyerere,na kama sikosei pia yuko chief Mareale wa moshi huyu sina uhakika sana,
makwaia alipendelewa na wazungu kwani alikuwa kibaraka mzuri,tatizo ilipofika mda hakuwa na chama wala uungwaji mkono miongoni mwa watanganyika,

nyerere yeye alikuwa ameteuliwa kuongoza Tanu na alikuwa na base ya uungwaji mkono,
waliomchangia nauli nyerere kwenda UN ndo hasa waliofanikisha uhuru,kwani baada ya kutoka UN,kilichofuata ni uhuru,
nyerere akawa na mandate ya kuachiwa kuwa PM@badala ya kina makwaia au Mareale
 
Huyo bwana hana tofauti na mchawi
Ameona hakuna mtu aliye na muda wa kusoma vijitabu vyake vya kipumbavu ameamua kukesha jamii forum kupotosha historia ya nchi yetu
Mimi ninadhani badala ya kumponda na kumdhihaki Sheikh Mohamed basi mngekuja na hoja mmbadala kuthibitisha uongo wake kama kweli upo.
 
Mimi ninadhani badala ya kumponda na kumdhihaki Sheikh Mohamed basi mngekuja na hoja mmbadala kuthibitisha uongo wake kama kweli upo.
Huyu Bwana watu wengi wanayopinga sio ukweli au uongo anaosema bali implication yake kwamba watu wa dini fulani walinyonywa na wanaendelea kunyonywa thus kudumazwa...

Sasa sijui ni nani ananufaika na kudumazwa wengine.., matatizo ya sasa ya umasikini, magonjwa na ujinga sidhani kama unachagua dini au imani.., anashindwa kusahau in the end is all about profiteering, umimi na ufisadi (huu hauna dini ni tabia ya mtu) watu wa Imani wafanye kazi zao kwenye mahekalu yao na mikusanyiko yao wenyewe kwa wenyewe na bila kuweka sumu ya kwamba matatizo haya yamesababishwa na mwenzangu, sababu tu ni wa imani tofauti
 
Mimi maoni yangu kwenye hili ni kuwa Sheikh Mohamed anazungumzia historia ya uhuru wetu ambamo ndani yake kulikuwa na mambo mengi yaliyotokea wakati wa mkoloni na pia wakati wa uhuru.

Historia inabaki kuwa historia kwani inawezekana kuwa na maeneo mabaya [kama vile wazungu walivyowaua wahindi wekundu marekani na kuchukua ardhi yao]. Ninadhani tukiangalia historia yetu positively utagundua mapungufu mengi ambayo yalikuwa masaza ya wakoloni. Cha kufanya hapa ni kukubali yale ambayo kweli yalitendeka na kuangalia hali halisi ilivyo hivi sasa na kutafuta namna ya kurekebisha.

Suala la Udini ukiliangalia kwa jicho chanya utagundua kuwa lilianzishwa na wakoloni kwani vibali vya kuanzisha shule nyingi walipewa misionary wakati hata kwenye shule za kawaida ingawa zilikuwa chache lakini tatizo lilibakia kuwepo na hili liliwafanya baadhi ya wanafunzi kubadili dini ili waendelee na masomo. Waislamu walijaribu kurekebisha hali hii kwa kufungua shule zao lakini vizingiti vilikuwa vingi sana. Matokeo ya hili ndilo lililofanya wazazi wengi wa kiislamu kuchelea kupeleka watoto wao shule[hata wakipata nafasi] kutokana na hili.

Eneo la pili ni kwamba hata ajira serikalini wakati wa mkoloni hali ilikuwa hivyo hivyo na kwa walioajiriwa walikuwa hawaruhusiwi kujihusisha na siasa kwa kitisho cha kufukuzwa kazi.

Hali hii ilifanya wale wazee wa kiswahili ambao walikuwa wachuuzi na wafanyabiashara wadogo na wasiotegemea ajira ya mdhungu kujitwisha zigo la kugembea uhuru.

Ukifanya utafiti kuanzia Dodoma, Tabora, Mwanza, Musoma, Kilimanjaro, Tanga na Kusini hali ilikuwa hivyo.Hata ujio wa Mwalimu Nyerere ulikuta hali hiyo kwani naye alikutana na vitisho vya wakoloni lakini alikuwa na bahati ya kuwa wazee wa kiswahili hao walimtia moyo na kumhudumia yeye na familia yake kwa kila hali hadi uhuru unapatikana.

Haya yote ninayokueleza kwa ufupi ni historical fact. Baada ya uhuru nini kilitokea????Nadhani hapo ndipo mnapomuona sheikh Mohamed siyo mtu mzuri na mdini.
 
Kitu kimoja , Mzee Mohamed Said amesaidia kuonyesha historia ambayo ilikuwa haikupewa nafasi sana. Udhaifu wake ni kuonyesha ulifanywa , kama waislam. Nafasi ya Nyerere ilikuwa muhimu kutokana na elimu aliyopata kule Edinburg na pamoja ujuzi wa kujua na kufuatilia hali ya kisiasa Tanganyika.

Wakati Nyerere yupo Edinburg - Abdul Sykes, Steven Mhando, Dr. Kyaruzi, DR . Seree , Mwapachu walitengeneza " Memorandum for Political Independence " hili dodoso waliloliwakilisha kwenye ofisi ya Umoja Wa Mataifa, inayohusu Makoloni, iliwaletea shida watu mbalimbali akiwemo, Mwapachu hadi akahamishiwa Ukerewe.

Hivyo Mwapachu, akamwandikia barua Nyerere akiwa Edinburg kuhusiana na hali nyumbani. Utagundua , Nyerere akiwa Edinburg vuguvugu la mabadiliko lilikuwa linaendelea nchini na kukaibuka viongozi mbalimbali kusongesha mapambano.
Saadani Abdu Kandoro, Said Maswanya na Bhoke Munanka kutoka maeneo ya Majimbo ya Ziwa ( Lake Province)

Kwa hiyo ukiangalia historia ya uhuru na mapambano ya Tanganyika , ilipita kwa michango wa watu tofautitofauti wa kada mbalimbali.. Tukitafuta kwenye historia zaidi, tutakuta makundi ya michango ya wafanyakazi, wakulima, wavuvi , wafanyakazi toka vyama mbalimbali na maeneo tofauti tofauti. Na makundi zaidi bado yapo .

Hii inanipa hamasa kuendelea kutafuta historia ya Tanganyika , ili kuweka mjumuiko mzuri. Kazi hii si ya kitoto au ndogo.. Na wakati tunaendelea na hayo na bado yataendelea sana, isifanye ionekane kuwa ni watu fulani wa madhehebu fulani, kutoka eneo fulani ndio waliochangia uhuru wa Tanganyika
 
Dhibitisha Mfumo Kristo uliopo ndani ya Nchi hii.
Azarel,
Nakujibu kwa kuwa umeniuliza swali kwa adabu na mimi kwa kurejesha heshima kwako nitakujibu swali lako.

Hii mada mwenyewe khasa mtaalamu ni marehemu Sheikh Ilunga Hassan Kapungu.
Sasa kwa kuwa hii ni mada nyeti na nzito sana nitakuomba ufungue uzi mpya ili tujadili.

Lakini kabla hujafungua uzi huo nitakupa darsa kuhusu maisha ya Sheikh Ilunga hadi kufika umauti wake na nini ulikuwa mchango wake katika jamii ya Waislam wa Tanzania.

Darsa hili litakusaidia wewe kuamua kuwa ufungue uzi huo au la.

Ingia hapo chini:

1567604484047.png

Juu wa kwanza kulia ni Sheikh Ilunga Hassan Kapungu na chini wa pili kulia ni Mwandishi 1988
 
Huyu hawezi kujifunza kitu kipya Kwasababu tayari ana sumu inatembea kwenye ubongo wake

Yeye akiona mtu anaitwa lazaro hawezi kumwamini Kwasababu alijazwa chuki na wazee wake naye anaambukiza chuki vijana wake

Hebu Fikiria watu wanaopotosha kwamba kuna mwaka waislam walifanya mtihani wa kuhitimu 71% unajua huyu anamalengo gani

Huyu ni kuigawanya jamii yake ihisi kwamba inaonewa Au inaishi tabaka la pili kumbe ni mzandiki mkubwa

Waislam, wakrsto na dini nyingine wote wamekula keki sawa nchi hii

Ila kwa sababu huyu mzee ana ajenda zake binafsi anapotosha msksudi
Mimi ninadhani badala ya kumponda na kumdhihaki Sheikh Mohamed basi mngekuja na hoja mmbadala kuthibitisha uongo wake kama kweli upo.
 
Mimi maoni yangu kwenye hili ni kuwa Sheikh Mohamed anazungumzia historia ya uhuru wetu ambamo ndani yake kulikuwa na mambo mengi yaliyotokea wakati wa mkoloni na pia wakati wa uhuru.
Historia inabaki kuwa historia kwani inawezekana kuwa na maeneo mabaya [kama vile wazungu walivyowaua wahindi wekundu marekani na kuchukua ardhi yao]. Ninadhani tukiangalia historia yetu positively utagundua mapungufu mengi ambayo yalikuwa masaza ya wakoloni. Cha kufanya hapa ni kukubali yale ambayo kweli yalitendeka na kuangalia hali halisi ilivyo hivi sasa na kutafuta namna ya kurekebisha.

Kuna historical accuracy na kuna allegations red indians kuuliwa hitler kuua Jews its hitorical accuracy na haipingiki ingawa hii haitumiki kama fimbo ya Jews kuwachukia wajerumani. Na pili issue kama hizi za jews ilibidi zitoke from multiple sources sio tu kila mtu alete allegations zake basi zifanywe kuwa hitorical accuracy.

Suala la Udini ukiliangalia kwa jicho chanya utagundua kuwa lilianzishwa na wakoloni
kwani vibali vya kuanzisha shule nyingi walipewa misionary wakati hata kwenye shule za kawaida ingawa zilikuwa chache lakini tatizo lilibakia kuwepo na hili liliwafanya baadhi ya wanafunzi kubadili dini ili waendelee na masomo. Waislamu walijaribu kurekebisha hali hii kwa kufungua shule zao lakini vizingiti vilikuwa vingi sana. Matokeo ya hili ndilo lililofanya wazazi wengi wa kiislamu kuchelea kupeleka watoto wao shule[hata wakipata nafasi] kutokana na hili.
Wakoloni wameacha masalia mengi tu.., hata hizo dini zote zilizopo zimeletwa, ila sijaona watu wanalalamika kwanini mizimu yao haipewi nafasi tena katika jamii, hii kubaguana ilikuwa ni order of the day hata hao walioleta hii dini walikuwa wanapewa first priority kuliko wazawa ngozi nyeusi / wabantu ambao ndio walikutwa.., ila sins of their and our fathers hatuwezi kuwapiga nazo kizazi cha sasa na cha kesho...

Choice waliofanya hao wazazi its their prelogative.., ila kufanya au kutokufanya kwao maamuzi hayo hakuwapi nafasi kubwa au ndogo katika nchi.., Utanzania is the only ticket no matter imani yako..., ndio maana nasema kwenye taifa la watu wenye Imani nyingi sehemu ya Imani ni kwenye mkusanyiko wao wenye Imani zao.., sio kuleta mambo ya imani yawe incorporated kwenye maisha ya kila siku..., ukizingatia imani hizo ni tofauti..., thus kinachotuunganisha ni utanzania na sio udhehebu au imani zetu za kiroho

Eneo la pili ni kwamba hata ajira serikalini wakati wa mkoloni hali ilikuwa hivyo hivyo na kwa walioajiriwa walikuwa hawaruhusiwi kujihusisha na siasa kwa kitisho cha kufukuzwa kazi.
Hali hii ilifanya wale wazee wa kiswahili ambao walikuwa wachuuzi na wafanyabiashara wadogo na wasiotegemea ajira ya mdhungu kujitwisha zigo la kugembea uhuru.
Ukifanya utafiti kuanzia Dodoma, Tabora, Mwanza, Musoma, Kilimanjaro, Tanga na Kusini hali ilikuwa hivyo.Hata ujio wa Mwalimu Nyerere ulikuta hali hiyo kwani naye alikutana na vitisho vya wakoloni lakini alikuwa na bahati ya kuwa wazee wa kiswahili hao walimtia moyo na kumhudumia yeye na familia yake kwa kila hali hadi uhuru unapatikana.
Haya yote ninayokueleza kwa ufupi ni historical fact. Baada ya uhuru nini kilitokea????Nadhani hapo ndipo mnapomuona sheikh Mohamed siyo mtu mzuri na mdini.
Kunyonywa na kudidimizwa mpaka leo kupo (its the law of the jungle).., kuna watu wanasema uwe chama fulani ili mambo yako yanyooke kuna watu inasemekana wana ukabila.., kuna watu inasemekena wanabagua kutokana na jinsia ya mtu.., either kuwadumaza kina mama au kuwapa wasichostahili kwa hongo ya ngono.., (that's life we live.., unfortunately).., sasa pamoja na hayo mapungufu unataka tuongeze la utofauti wa kiimani ?..., Hell no.., imani ibaki kwenye sehemu zake kwenye mambo ya kiimani na si vinginevyo..., haya mambo ya kidunia tuwaachie wanasiasa, wanadunia na wengineo...
 
Namimi naomba nikuulize unadhani kwanini afahamike JKN kama aliyetuletea uhuru ilihali kulikua na watu walioanza kabla..?
Nani aliyeandika Historia hii ambayo tunasomeshwa ?

Unakataa kwamba katika Elimu hakuna hila ? Kama unakataa,basi utakuwa sio mtafiti wala si msomaji.

Swali ulilo uliza,ulitakiwa sasa urudi kuwauliza walioandika Historia hiyo hali ya kuwa umekutana Historia dhidi ya hiyo tunayosomeshwa.

Naendelea. .....
 
Sio ali mwinyi pekee sio abdul syke au mwapachu waliokua na mchango katika ukombozi wa tanzania tunakubai walikuepo na wengine wengii tuuh lakini historia haiez kuandika kila mtu au mchango wa kila mtu sababu watu wazalendo walikua ni wengii, mfano inasemekana kulikua na matawi zaidi ya 30 ya TAA sasa historia haiez kuchambua na kueleza kila member katika kila tawi kama unavyotaraji wewe... .. ila tunatizama key players katika kufanikisha ile adhima iliyokuwa ikikusudiwa ndio tunamsikia JKN aliekua kifua mbele....
Mizy...
Sijasema kuwa historia iandike kila mtu nilichoandika mimi ni historia ya African Association 1929 hadi kufikia TANU 1954.

Hii si historia ya kila mtu.

Sasa nakuwekea hapo chini kipande cha makala ya Daisy Sykes kutoka kumbukumbu aliyoandika katika miaka 50 ya kifo cha baba yake Abdul Sykes.

Nitakuachia mwenyewe utafakari historia ya TANU na wapi ilikotokea na kama unaona ni sawa kwa historia hii kufutika:

''Juma moja kabla ya kifo chake nilimuuliza baba swali ambalo jibu alilijua lakini katika hulka yake ya kawaida ya kutopenda kujikweza hakutaka achukue sifa zote kwa ule ukweli na matokeo yake.

Wakati ule nilikuwa mwanafunzi Chuo Kikuu Cha Afrika ya Mashariki Dar - es- Salaam na mwalimu wangu wa Historia Dr. John Iliffe kwa kutambua kuwa natoka familia ya Sykes waasisi wa mwamko wa siasa katika Tanganyika na mchango wa wazee wangu katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika alinitaka niandike mafanikio ya Watanganyika wa kizazi kile pamoja na historia ya babu yangu Abdallah Kleist Sykes. Dk. John Iliffe alinitia moyo nifanye utafiti na kuandika historia hii na nilikubali kufanya hivyo.

Nilikuwa na swali kuhusu nani khasa walikuwapo katika mkutano na kushiriki wa kuibadili TAA kuwa TANU.

Baba akashauri kuwa tuombe miadi na Rais wa Tanzania Mwalimu Nyerere ili anipe ukweli niliokuwa nautafuta na kusadikisha mambo mengine yanayohusiana na historia hiyo.

Hivyo tukaenda Msasani kuonana na Mwalimu Jumamosi moja asubuhi.

Kama ilivyotegemewa Mwalimu alifurahi sana kutuona maana ilikuwa muda mrefu watu hawa waliokuwa marafiki wakubwa sana kupata kuonana.

Mwalimu alitoa ushirikiano mkubwa sana kwangu kupata ukweli kutoka kwake katika yale niliyotaka kujua kutoka kwake.

Hii ndiyo ilikuwa siku yao ya mwisho kuonana.''

Hii makala nimeitafsiri kutoka Kiingereza na ina utamu wa aina yake ukiisoma kama alivyoiandika mwenyewe.

Yapo mengi mazuri katika makala hii na ikiwa hujaridhika na hayo hapo juu nieleze nikuwekee vipande vingine In Shaa Allah.
 
Mohamed Said,

Lakini mzee wangu Mohamed Said huyo sheikh Ilunga tabia yake ilikuwa mbaya na alikuwa mfano mbaya kabisa tofauti kabisa na ninavyowafahamu waislamu ninaoishi nao mitaani kwetu na hata makazini.

Kuna video zake kadhaa kwenye youtube ameonekana na kusikika akiwahimiza waislamu waue mapadri, kardinali na maaskofu, eti kulipiza kisasi cha sheikh aliyeuawa na polisi kule Kenya. Nilimshangaa sana na kumdharau kabisa. Eti polisi wakiua mtu Kenya basi inahalalisha watanzania kuua wenzao kwamba wanalipiza kisasi? Kisasi kipi? Kardinali au askofu au hata paroko wa Tanzania anahusikaje na polisi wa Kenya, kuna ushahidi gani kuwa ndiye aliyewatuma hao polisi wamuue huyo sheikh?

Najisikia vibaya sana kwa mtu ninayemheshimu kama Maalim Mohamed Said kumshabikia au kuunga mkono vitendo na kauli za Sheikh Ilunga zilizokuwa na nia ovu ya kusababisha shari.
 
Hammaz,

Hammaz,
Tatizo ninaloliona kukukabili wewe ni kule kutoijua historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kwa ukamilifu wake.

Miaka michache iliyopita hapa JF niliweka bandiko lililoeleza kuwa hotuba ya Mwalimu Nyerere UNO mwaka wa 1955 ilikuwa katika mafaili ya TAA toka 1950 na waandishi wa hotuba ile wanatoka katika TAA Political Subcommitee ambao wajumbe wake ni: Sheikh Hassan bin Ameir, Abdul Sykes, Dr. Vedasto Kyaruzi, Hamza Mwapachu, Said Chaurembo, John Rupia na Steven Mhando.

Wako wasomaji walighadhibika sana na kuniita mimi muongo.
Tofauti yangu na wao ni kuwa mimi nimezisoma Nyaraka za Sykes zote na nimena mengi.

Sasa nataka nikusaidie wewe nikutoa huko kwenye ujinga wa kutojua historia ya kweli ya Tanganyika.

Ingia hapo chini:

Lakini mzee wangu Mohamed Said huyo sheikh Ilunga tabia yake ilikuwa mbaya na alikuwa mfano mbaya kabisa tofauti kabisa na ninavyowafahamu waislamu ninaoishi nao mitaani kwetu na hata makazini . Kuna video zake kadhaa kwenye youtube ameonekana na kusikika akiwahimiza waislamu waue mapadri, kardinali na maaskofu, eti kulipiza kisasi cha sheikh aliyeuawa na polisi kule Kenya. Nilimshangaa sana na kumdharau kabisa. Eti polisi wakiua mtu Kenya basi inahalalisha watanzania kuua wenzao kwamba wanalipiza kisasi? Kisasi kipi? Kardinali au askofu au hata paroko wa Tanzania anahusikaje na polisi wa Kenya, kuna ushahidi gani kuwa ndiye aliyewatuma hao polisi wamuue huyo sheikh?
Najisikia vibaya sana kwa mtu ninayemheshimu kama Maalim Mohamed Said kumshabikia au kuunga mkono vitendo na kauli za Sheikh Ilunga zilizokuwa na nia ovu ya kusababisha shari.
Ralph...
Kwa nini unasema mimi namshabikia Sheikh Ilunga?
 
Nani aliyeandika Historia hii ambayo tunasomeshwa ?

Unakataa kwamba katika Elimu hakuna hila ? Kama unakataa,basi utakuwa sio mtafiti wala si msomaji.

Swali ulilo uliza,ulitakiwa sasa urudi kuwauliza walioandika Historia hiyo hali ya kuwa umekutana Historia dhidi ya hiyo tunayosomeshwa.

Naendelea. .....
Zurri,
Kuna kitabu kilichoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni kinaitwa Historia ya TANU 1954 - 1977 ingia hapo chini kupata historia yake:

Ralph...
Kwa nini unasema mimi namshabikia Sheikh Ilunga?
Niwie radhi kama sijakuelewa vizuri lakini katika post yako kumhusu naona umemjaza masifa kedekede! Nami tangu siku nilipoona video zake katika youtube za kuhimiza watu kuua wengine roho yangu ilikataa kabisa kupatana na chochote kinachomhusu!
Lakini nitafurahi na kufarijika sana ukitamka mwenyewe kuwa hukubaliani na mahubiri ya marehemu Sheikh Ilunga yanayowataka waislamu waue kardinali, maaskofu na maparoko kulipiza kisasi.
 
Back
Top Bottom