Nimesoma mara tatu huu uzi wako nikawa najishauri nikujibu au nisikujibu au nijibu kwa namna gani,lakini nafsi ikasita,nikajisemea nina kitu cha kusema hapa kisha nitatoa msimamo wangu mwishoni.Katika mada zako nyingi za historia ya taifa hili hua nikiangaliama Context naona mada zako zote zinalia kwa uchungu huku zikitoa ujumbe kua Waislamu tunaonewa, nikimaanisha kwamba mada zako karibu zote hua zina chembe chembe za Udini.
Kwamba je haya anayoyasema ni ya uongo au sababu yeye ameeleza yale ambayo hatukuyasikia au hatukupenda kuyasikia ? Nafsi ina maajabu yake sana.
Hivi mathalani mimi nikitetea haki yangu na kueleza sababu ya kukosa haki yangu ni dini yangu,nitakuwa mdini ?
Je haya anayoyasimulia mzee wetu ushawahi kujiuliza kwanini hayakusomeshwa vitabuni mwetu ? Je walifanya makusudi au kwa bahati mbaya ? Kama walifanya kwa bahati mbaya kwanini waliandika Historia bila kuchunga misingi ya kuandika Historia ?
Kila elimu ina takiwa ifate misingi 10,narudia tena kila elimu inatakiwa ifate misingi 10,ukiikosa misingi hiyo kaa ukijua hutaipata elimu hiyo. Misingi hiyo sitaitaja kwa sasa,kama ikibidi huko mbeleni nitaitaja. Maneno haya aliyasema mwanachuoni mkubwa Ali Swabaani.
Kila fani ya kielimu ina namna yake ya ukosoaji ila kwenye asili ndiko majambo hurudishwa.Baadhi ya member hasa mkuu @Pascal Mayalla USER=262438]GUSSIE[/USER] wamejaribu kuchambua mada zako na kuonyesha ni jinsi gani zilivyojaa mahaba ya dini,na upotoshaji wa historia pia hata wasomaji wako ambao mko imani moja wanadiriki kuupinga hata ukweli ili tu kumtetea mwarabu na dini yake. ...mfano kwenye mada aliyoanzisha mkuu pasco akionyesha jinsi warabu walivyowatesa wazawa wa zanzibar watu wengi (isalms) waliukataa ukweli huona na kukubali kumtetea mwarabuu kisa tu ndio alieleta dini hiyo.
Leo hii wewe ukitaka kuikosoa historia ambayo aliiandika mtu fulani basi na wewe rudi kule kule kwa wenye Historia yao kisha uikosoe ili ambayo iko dhidi.
Pia,kuna maneno ya uongo unayasema na haya bila shaka umeandika kwa chuki pia hali ya kuwa unataka kujaribu kuamisha ya kuwa huna chuki,ya kwamba muarabu ana dini,Muarabu hana dini,sababu kwa waarabu kuna wapagani,washirikina na wasio kuwa hao. Hili umelisema lakini ukiombwa ushahidi naamini hata ukipewa miaka mia hutaweza kuthibitisha ya kuwa Uislamu wa waarabu. Kwahiyo unatakiwa ukiandika uandike kwa haki.
Mathalani mnaposema Historia aliyoiandika mzee wetu ina Udini,basi mlitakiwa kuonyesha au kuandika Historia ya kweli ambayo inaonyesha haina Udini huku mkirejea kwa wenye Historia.
Hili na wewe linakuhusu bali hata mimi,na wale pia. Huu uzi wewe ndio umeziruhusu hisia zikuongoze ndio maana umeandika ya uongo mengi na moja wapo ni hilo la kusema Uislamu ni wa waarabu.mzee wangu wewe ni mwandishi na unazifahamu vyema Ethics za mwandishi, moja ya sifa kuu za Mwandishi ni kutokuandika habari fulani kwa kuweka mbele emotions na mahaba yake juu ya kitu anachotaka kutoa taarifa, mwandishi unatakiwa uandike/utoe habari ya kitu hicho ukiwa kwenye Free state, yaani uandike kitu kama kilivyo bila kuweka mahaba yako juu kitu hiko. Kwa hilo mzee wangu naona umefeli kulitekeleza labda lengo lako kuu hua ni kuonyesha jinsi gani ndugu zetu mnavyo kandamizwa.
Hivi mfano wewe ukitaka ukiandika Ukweli labda kuhusu watu wako lakini katika ukweli huo kuna madhila na dhiki kubwa sana zilizo wakuta watu wako,ukweli huu ukitaka kuuwasilisha unauwasilishaje ? Je kwenye huzuni utaweka bashasha ?
Nikupe mfano kidogo, humu JF kuna mwandishi wa makala mbalimbali anaitwa The Bold (@habibu B Anga) ni mwislamu pure! Lakini kamwe akiandika kitu ambacho hua kinagusa imani yake hua anaandika kama kilivyo bila kuweka upendeleo. Ref uzi wa:Adhabu ya kuchinjwa mbele ya kadamanasi Saudia.
Kwangu mimi mtu kama huyu hakupaswa kuruhusiwa kuandika makala kama zile au kwanza apewe masharti kabla ya kutuma makala zake wahakikishe ameweka na marejeo,kwani Elimu ni amana na amana huwa inarudishwa kwa watu wake,kama kweli watu wanapenda kusoma na kujifunza mambo. Tatizo kubwa la muandishi huyu ni kuwa maandiko yake hayarudishi kwenye asili yaani hana marejeo,pili mambo ya uhalisia anayasimulia kama kama habari za kubuni,mwisho wake anakuwa anapunguza au kuzidisha. Uzi huu naukumbuka na kuna nukta kadhaa nilimkosoa na kuna swali nilimuuliza lakini hakujibu,sijui kama labda huo ndio utaratibu wake au la ! Mimi namdhania kheri.
Kwanza alichokosea yeye ni jambo la kidini kulizungumza kihuni kwa kutaka kutenganisha dini na jambo lile,inaonekana huko anakochukua ambako huwa hatuonyeshi ni kuwa wtu hao hawaijui dini.
Nakumbuka nilimkosoa katika kichwa habari,katika Kiswahili hakuna sentensi "....mbele ya kadamnasi..." kuandika hivi ni kufanya makosa. Tamko "kadamnasi" limejitosheleza kwa lenyewe kwani ni muunganiko wa atamshi mawili nayo ni "kadamu" kwa maana ya mbele ya kitangulia na tamko la pili ni "nasi" kwa maana ya watu,makosa hayo ni sawa na kuandika "......mbele mbele ya watu ....." hakuna Kiswahili cha namna hii.
Angalizo anatakiwa akiwa anazungumzia mambo ya dini basi ahakikishe ana ujuzi na maarifa mapana juu mambo hayo.
Kuna mambo mengine kutokana na umaarufu wake hata kama una hila ya kwapa,huwezi kuuficha ukweli zaidi ya kujibaraguza kwenda na hatua na mirindimo husika. Hapa kuna tegemeana.Lakini mzee hata mimi mwenyewe ni mkatoliki lakini kama nikichangia mada au kundika mada juu ya mauaji yaliyofanywa na kanisa hili siwezi kubisha au kuandika tofauti na ilivyokua kisa ni kanisa langu, siwezikubisha wala kuandika kwa upendeleo kua kanisa katoliki kipindi cha Holocust liliagiza (Papa) wananchi wote wa nchi ya Uholanzi
(Netherlands) wauawe.
Hilo jambo mpaka umelijua wewe ujue watu wengi wamelijua,lakini kuhusu Historia hiyo ya uhuru wengi hawakuwa wakiujia Ukweli,sasa hapa ndipo utakapo jiuliza kama nilivyo gusia huko,je walifanya makusudi kuificha au walikuwa naaarifa machache juu ya uandish wa Historia na kama walikuwa na maarifa machache juu ya kuandika Historia kwanini waliiandika na kuitawanya ?
NB: Yote hayo najaaribu kukuonyesha ni jinsi gani kuna udini kwenye mada zako, lakini lengo langu sijaandika uzi huu ili tujadili udini wala dini yako ila lengo langu hasa kuandika huu uzi ni
Hu ni mtazamo wangu tu,kwangu mimi sijaona udini katika maandiko yangu,na mwisho nitatoa msimamo wangu juu ya maandiko ya mzee wetu.
Mkuu kama nilivyokwisha kukuonyesha jinsi mada zako zilivyo na udini, sasangoja niende kwenye lengo la uzi huu..Mada zako nyingi nilizowahi kusoma kuhusu historia ya uhuru wa Tanganyika, ukiangalia nyuma ya pazia ujumbe ulio jificha unaonyesha kua Mwl. Nyerere hakutakiwa kuwa recognise kama mtu aliye tuletea Uhuru nchini toka kwa wakoloni, Bali kuna wazee wa kiisalmu wa hapo Dar kama Sykes familly n.k ndio wamehangaika zaidi kuleta uhuru.
Mimi nilicho kiona ni kuwa mzee wetu ametuoyesha ya kuwa kumbe kuna watu wengine hawatajwi japokuwa walicheza nafasi kubwa sana katika jambo hilo la uhuru.
Hivi kwani wewe hapo kabla hao wazee alio wazungumzia mzee wetu ulikuwa unawajua ? Kama ulikuwa huwajui kwanini ulikuwa huwajui ? Je tatizo ni lako au tatizo ni la wale walio andika Historia ?
Au jalia tukwamba hao wazee hawakutoa mchango mkubwa kihivyo je ni kwa lipi hawakutajwa ?
Je hawakustahili kutajwa na kwanini ?
Mkuu ni kweli wamechangia kiasi kikubwa kupatika uhuru hapa lakini, ukweliutabaki pale palekua ni J.K.Nyerere the Almighty ndio kaleta uhuru Tanganyika na sio hao wengine bila kuzingatia kigezo cha udini. kwanini nasema hivi?
Kawaida katika wengi lazima wawepo wawakilishi kwanini umtaje yeye Nyerere pekee kwani kule alipewa uhuru baada ya kupigana au aliupora au alipewa tu baada ya muda kufika ? Hii hata lugha inakataa kukata na kumuweka yeye pekee.
Hili sio lengo bali ni matokeo,kwani lengo la sisi kuumbwa ni kumuabudu Mola pekee,haya mengine yanayotokea ni sehemu ya maisha wala hutokuja kuulizwa kwanini hukupigania uhuru wala kwanini wewe ulipigania uhuru.Kila mtu akizaliwa hapa duniani huja na kusudi (Purpose) aliloletwa kulitimiza, kwa mantiki hiyo Mwalimu aliletwa kwa kusudi la kuikomboa Tanganyika kutoka kwenye mikono ya
Huu ni uongo,mkubwa sana,je kusudi huwa unalijua kabla au baada ?
Hii sio hoja bali ni malalamiko,huu ni uwakilishi ambao ulikuwa na sababu.Mwalimu nyerere kazaliwa 1922 lakini mwaka 1945 akiwa ana miaka 23 tu aliweza kuhudhuria mkutano wa 5 wa Pan African Congress jijini Manchester hivyo basi waweza kuona ni jinsi gani alivyikua ashajua kusudinla yeye kuja dunianina kuanza kulifanyia kazi. mkuu hatima ya uhuruwa Tanzania ilikua mikononi mwa mwalimu, na kama inavyojulikana "You can escape your Destiny, Nobody can take away your Destiny"
Mfano kidogo ili kuenea kwa imani ya kiislamu duniani allah ilibidi amletee Mtume maswahaba ambao walimsaidia pakubwa kusambaza uislam kwenye maeneo ya makafiri, vilievile ili YESU kueneza wokovu duniani ilibidi awe na wanafunzi na mitume wa kusambaza Habari za wokuvu ulimwengu mzima, kupitia wanafunzi wake Yesu aliweza kutimiza kusudi lake la kueneza wokuvu, Mwisho wa siku tunasema Yesu katuleta wokuvu mpaka kwetu huku ndani ndani ( ila hatusemi mitume wanatakiwa ndio wtambulike kama walioleta wokovu duniani bali Yesu) Mkuu hata wewe hadi kufika hapo ulipo kuna watu walisimama nawe hadi kua wewe uliyoko sasa hivi, ila hatusemi kwamba wale wiloku-push kipindi cha nyuma ndio wanaotakiwa kufahamika kama wanaoandika makala humu jF bali mzee Mohamed Said.
Hapa uko sahihi kabisa lakini wale wote walio kuwa bega kwa bega na mitume tunawajua na michango yao inajulikana tangu mwanzo mpaka kiyama kinasimama na tunawaombea dua kila kukicha,je hao waliomsaidia Nyerere mbona hawatajwi,mpaka mzee wetu alipokuja kuelezea upande wa pili au wewe uliwasoma hao hapo kabla ?
Kutetea hila na uongi wa watu wa ovu kuna ujasiri na kujitoa akili.
Kwa mantiki hiyo namaanisha kwamba ili kutimiza kusudi fulani ulilopewa na Mungu basi Mungu hukuandalia watu ambao watafanya kazi bega kwa bega ili kutimiza kusudi lako (mfano mzuri ni wazazi/walezi). hivi mkuu unatambua kua kuna watu hua wamezaliwa kusudi lao la kuzaliwa likiwa ni kuja kumsaidia mtu fulani aje kutimiza kusudi lake alopewa na Mungu,mfano mzuri ni Yohana mbatizaji. kusudi lake hata kwenye vitabu vinasema alikuja kuandaa njia/kusudi la Masihi Kristo....Hivyo hivyo kwa Mwalimu wetu Kuna watu wengi sana waliletwa hapa Tanganyika kuja kutimiza kusudi hilo. Ili kutimiza kusudi lake la kuiletea nchi yetu uhuru ilibidi watu wengi washirikiane nae. hatimaye aliweza kufanikiwa kuleta uhuru, hivyo basi hakuna suala la udini wala nini The Godman Nyerere atabakia kutambuliwa kama shujaa aliyeleta uhuru Tanganyika haijalishi ni wangapi walishirikiana nae.
Sasa haya ndio mahaba niue na aya yako ya mwisho imesisitiza hilo.
Sisi huwa tunasema hivi "Kitengeneze kiti chako kwanza kabla ya kukitia nakshi"
Niombe radhi kwa yoyote ambae andiko langu limemuudhi kwa namna moja au nyingine.
Ciao
- Da'Vinci
Mimi binafsi nimekupa udhuru sababu umetumia hisia sana kuliko ukweli na maarifa. Hisia zako nimekuachia mwenyewe.
MSIMAMO WANGU.
Waislamu tukiona tunakuwa wadhaifu sana na kuhisi tunaonewa basi tukae tukijua kwamba sisi ndio sababu basi lazima turudi nyuma na kujitathmini upya.
Kama kuna lolote ambalo nimekosea basi ni kwa udhaifu wangu.