Mohamed Said,
Sidhani kama nimesema Mwalimu alikuwa na chama, bali nimesema Mwalimu alikuwa na mpango wa kuanzisha chama cha kupigania uhuru awali kabisa akiwa chuoni, nina uhakika na hili kwa 100% nikifanikiwa kupata vielelezo vyangu nitakuja navyo maana nimeshindwa kuvipata kwa siku za hivi karibuni.
Kuhusu kuandika Historia, mimi sio Mwanahistoria, bali ni mfuatiliaji tu wa historia, na napenda kusoma/kusikiliza vyanzo mbalimbali na hii husaidia kukwepa historia zenye muelekeo mmoja kama ninazoziona kwako.
Ninaposema "Wenzako" nimepandisha kipande cha video hapo chini. Na hakuna njia nitawatenganisha Watu hawa na hizi makala zako, maana muelekeo ni huo huo, plus kuna clip aliipandisha mshirika wako wa karibu Faiza, ya bw anayesema kwamba Wajerumani walitaka kuhamisha makaburi ya Waislam wakawa wanatokewa na watu wasioonekana na kuchapwa viboko...hekaya kama hizi siwezi kuzitenganisha na makala zako.
Kuhusu historia ya TANU, upo sahihi kabisa, mimi sio mbobezi wa historia, ni mfuatiliaji tu...na hii isiwe fimbo kwako kutushindilia taarifa zenye mlengo wa upande mmoja..yapo niliyoyasikia kuhusu TANU ila kwako unayahepa.
Hayo mengine niliyoeleza kwenye andiko langu umsikilize Mzee Bilal hapa chini.