Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Safuher,
Mimi nimejiuliza sana kwa nini zilifanyika juhudi za kufuta historia ya kweli na kuweka historia ambayo haikuwa sawasawa.

Mtu wa kwanza kukutana na hali hii ya kutaka kubadili historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika ilimkuta Abdul Sykes mwenyewe miaka ya mwanzo ya uhuru pale TANU yenyewe ilipotaka kuandika historia yake na Abdul na Dr. Wilbard Kleruu wakakabidhiwa kazi hii.

Yale aliyokutananayo Abdul aliamua kujitoa lakini Dr. Klerruu alikamilisha kazi ingawa kazi hiyo haikuchapwa kitabu ikabaki mswada katika maktaba ya TANU Mtaa wa Lumumba hadi ilipochukuliwa na kuchapishwa kitabu na Abubakr Olotu baada ya mswada kufanyiwa mabadiliko ya hapa na pale.

Kitabu hiki kinaitwa. ''Historia ya TANU,'' (1971) na hakina tofauti na kitabu cha Chuo Cha CCM Kivukoni, ''Historia ya YANU 1954 -1977.(1981).
nadhani kuna makusudio kwa nini Mungu amekuweka mpaka nyakati hizi mzee wetu.

kuna haja kubwa ya sisi vijana kujifunza kutoka kwenu wazee mlioshuhudia mambo yakitokea chini ya nyayo zenu.,kiko kujifunza mambo haya kwa watu ambao wamesoma tu zile historia ambazo zimeandikwa na wao wakazichukua.

neno Moja kwako mzee wangu endelea kutuelimisha na kutuchimbulia historia kwa hekima hii hii unayoonesha,vijana tuna jambo kubwa la kujifunz kutoka kwenu wazee wetu.

nitazidi kuisoma historia sahihi kutoka kwa watu sahihi.

nimejiuliza pia na kupata majibu ya kuwa waatu wptee wanaokataa kqzi zakobasi wana mrengo mmoja tu ambao ni chuki za kidini.

hawapingi illaa kwa sababu hiyo tu ambayo hata kama ni kweli basi lazima iwekwe kwenye historia.

kuna ubaya gani kukubali kwamba waislamu walichangia kwa asilimia zao katika kuutafuta uhuru wa Nchi hii.
 
@Da'Vinci, Nyerere hakuwepo kwenye mkutano wa Pan Africanism ,Manchester,wakati huo hata hajahitimu Makerere
 
nadhani kuna makusudio kwa nini Mungu amekuweka mpaka nyakati hizi mzee wetu.

kuna haja kubwa ya sisi vijana kujifunza kutoka kwenu wazee mlioshuhudia mambo yakitokea chini ya nyayo zenu.,kiko kujifunza mambo haya kwa watu ambao wamesoma tu zile historia ambazo zimeandikwa na wao wakazichukua.

neno Moja kwako mzee wangu endelea kutuelimisha na kutuchimbulia historia kwa hekima hii hii unayoonesha,vijana tuna jambo kubwa la kujifunz kutoka kwenu wazee wetu.

nitazidi kuisoma historia sahihi kutoka kwa watu sahihi.

nimejiuliza pia na kupata majibu ya kuwa waatu wptee wanaokataa kqzi zakobasi wana mrengo mmoja tu ambao ni chuki za kidini.

hawapingi illaa kwa sababu hiyo tu ambayo hata kama ni kweli basi lazima iwekwe kwenye historia.

kuna ubaya gani kukubali kwamba waislamu walichangia kwa asilimia zao katika kuutafuta uhuru wa Nchi hii.
Safuher,
Umemtaja Allah.

Hakika Allah anafanya mambo jinsi ambavyo shida kwa binadamu hata kufikiria kwa mbali.

Siku moja Ally Sykes alinipigia simu kunambia niende ofisini kwake kuna mtu anataka nikutanenae.

Huyu mtu alikuwa Jim Bailey.

Jim Bailey
ni Mzungu kutoka Afrika ya Kusini mwenye jarida lililojulikana kama Drum ambalo lilikuwa maarufu sana katika miaka ya 1950 hadi 1970 na likisomwa katika nchi zote Afrika ambako Kiingereza kikizungumzwa.

Jim Bailey alikuwa na mswada wa kitabu cha mapicha na captions, '' Tanzania: The Story of Julius Nyerere,'' na alikuwa anataka nimfanyie uhariri na nimtafute mchapaji hapa nchini wa kuchapa kitabu hicho.

Kitabu kilikuwa na picha nyingi za wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika hadi utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi.

Jim Bailey
akaniomba tupate chakula cha mchana pamoja ili tupate wasaa mzuri wa kuzungumza na tumwache Bwana Ally aendelee na shughuli zake.

Tukaenda Kilimanjaro Hotel siku zile katika miaka ya 1990s ndiyo ilikuwa hoteli kubwa ya kutajika Dar es Salaam. Nakumbuka tuliingia Zebra hii ilikuwa restaurant ground floor na walikuwa na buffet.

Bi mkubwa mmoja ndiyo alikuwa in charge pale na aliponiona nimeingia na Mzungu na tumekaa kwenye viti akanifanyia ishara ya kuniita nende kwake.

Akaniuliza kama tumekuja kula nikamjibu akanishauri akasema kuwa ni bora tupande juu kwenye restaurant nyingine kwani kule chakula ni kizuri zaidi.

Basi tukapanda juu.

Tulizungumza mengi na tulipomaliza tukaagana na akanambia kuwa anarudi Johannesburg na tuwasiliane nitakapokamilisha ile kazi ya uhariri.

Katika mswada huu nilikuta picha mbili ambazo zilinisisimua kwani sikupatapo kuziona popote kabla.

Picha ya kwanza ilikuwa ya Julius Nyerere na Sheikh Suleiman Takadir juu ya jukwaa wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika siku za awali za TANU.

Juu ya jukwaa lile alikuwapo pia Mama Maria Nyerere, Bi. Titi Mohamed, Clement Mtamila, Rajab Diwani na John Rupia.

Sheikh Suleiman Takadir baada ya ugomvi wake na Mwalimu Nyerere mwaka wa 1958 akawa mtu ambae kama vile TANU iliweka mkakati kuwa jina lake lisitajwe wala historia yake isizungumzwe popote pale.

Picha ya pili ilikuwa ya Mwalimu Nyerere na Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Tatu bint Mzee na Bi. Titi Mohamed wamepiga Uwanja wa Ndege Dar es Salaam mwaka wa 1955 wakimsindikiza Mwalimu safari ya kwanza UNO mwezi February, 1955.

Picha hizi zimesaidia sana kueleza historia ya TANU khasa katika zile ziku za mwanzo za kujenga chama kabla ya Uchaguzi wa Kura Tatu mwaka wa 1958.

Kazi ya Bailey niliikamilisha na nikamkutanisha na publisher na kitabu kikachapwa.

Miaka mingi ikapita sikupata tena kuonana na Jim Bailey.

Siku moja niko ndani ya ndege nakwenda Manzini kupitia Johannesburg na nikapanga nikimaliza shughuli zangu Swaziland nitakwenda Johannesburg nikamuone Jim Bailey na nia yangu ilikuwa kutembelea kavazi lake la picha maarufu kama Jim Bailey Collection.

Ikawa nimekaa na Mzungu mmoja ndani ya ndege na katika mazungumzo nikamwambia kuwa nitakwenda Johannesburg na hapo nikamtaja Jim Bailey.

Kwa mshangao na mshtuko akaniuliza kama ninamfahamu Jim Bailey.
Akanipa pole akaniambia Jim Bailey alikuwa jirani yake na wamemzika mwezi uliopita.

Kila ninapoziangalia picha hizi zinanikumbusha Jim Bailey lakini naamini yeye kaingia kaburini akiwa hajui umuhimu wa picha zile mbili alizozileta Tanzania kutoka Afrika Kusini kwenye Jim Bailey Collection.

Jim Bailey
alianiambia kuwa alihudhuria sherehe za uhuru wa Tanganyika 1961 na Zuberi Mtemvu ndiye aliyemuazima gari yake kutembelea mpaka siku aliporudi Johannesburg.

1567712990859.png


1567712926999.png


1567712166382.png
 
Lete ushahidi...
Da'Vinci,
Nadhani post yangu moja nimeweka jana imekupita hukuiona nikisema ukitaka kujua zaidi kuhusu Mwalimu Nyerere soma kitabu cha Thomas Molony, ''Nyerere: The Early Years, '' James Curey (2014).

Ushahidi wangu ndiyo huo na kukufahamisha tu ni kuwa Thomas Molony tunafahamiana vyema na katika kitabu hicho kanitaja kama rejea.

Nilikuwapo New Africa Hotel siku alipozindua kitabu chake na tulipata muda wa kuzungumza ingawa haukuwa muda mrefu.

1567721178348.png

.
 
lukubuzo Samsis,

Luku...
Saigon tulianza kama Everton na jezi zetu rangi ya blue kama Everton ya Uingereza.
Tumezinunua Dar es Salaam Music and Sports Independence Avenue na no. tumetilisha kwa Fakrudin.

Umenikumbusha mbali sana udogo wangu.
Nyumbani mama anagomba natumia muda mwingi kucheza mpira kuliko kusoma.

Tuko Mnazi Mmoja mechi kali nikiangalia kushoto kwangu namuona "Guy" Gharib kulia namuona Jumanne Masimenti pembeni namuona Kodo nyuma nasikia sauti ya Chico Centre Back wetu yeye mpirani alikuwa akihamasisha kwa Kiingereza, ''On him..'' ''Score...'' nakumbuka kama jana hii ni 1966 sote ni watoto.

Nikivaa jezi no. 7.
Tulikuwa na coach...

Mpira unakwenda kwa kasi sana na coach anapiga kelele nje za kututia moto tuzidishe mashambulizi ...
Leo sisi ni wazee na hao niliowataja wametangulia mbele ya haki...

Leo bint yangu kanihimiza nifanye mazoezi asubuhi...
Sasa tuje katika haya maneno yako hapo chini:

"M.Said aka mzee wa sago saigon ni mrongo kwa kujitungia ufongo ili apate sapoti ya kidini huko madrasa na misikitini. Huyu mtu ni hatari ana ajenda ya ugaidi nyuma yake wakian farid wa uamsho,serikali lazima itolee macho kwa huyu gaid aliyejificha kwa mgongo wa dini.''

Nilikuwa nimekupuuza kwa maneno yako ya kipuuzi kuna wafuatiliaji wa darsa ninazotoa hapa hawa hawaandiki hapa wao ni wasomaji tu lakini wanawasiliana na mimi wengi wao wanajiita wanafunzi wangu,

Hawa baadhi toka jana usiku wamekuwa wakiniletea ujumbe kuwa nizungumze kuhusu hili sula la ugaidi ili tuepushe nyuzi tunazojadili hapa kuvurugwa na kuharibiwa na watu mfano wa wewe.

Kwanza nataka nikufahamishe kuwa serikali haikuhitaji wewe kuwapa taarifa zangu kwani mimi nafahamika kwingi khasa kwenye vyuo vikuu ambavyo vinasomesha African History na hii inatokana na uandishi wangu wa historia ya Tanganyika inayokwenda nyuma miaka 100.

Kitabu nilichoandika ni katika rejea muhimu na baadhi ya vyuo hivi nimealikwa kuazungumza.

Orodha ya magaidi wote dunia nzima iko Marekani na wao wameisambaza ulimwengu mzima pamoja na Tanzania.
Haya Wamarekani wamefanya baada ya 9/11.

Hawa magaidi watakamatwa popote duniani watakapoonekana.

Sasa nikufahamishe kuwa kuanzia mwaka wa 1998 nimekuwa kwa kipindi cha miaka 8 nikisafiri Afrika ya Mashariki kwa vipindi vifupi vifupi nikiingia Kenya na Uganda kwa likizo za shule ambako wanangu walikuwa wanasoma.

Nimesafiri kwenda Afrika ya Kusini, Swaziland, Nigeria, Ethiopia, Egypt, Germany, Holland, Switzerland, Dubai, Oman na Saudi Arabia na Marekani na nchi nyingine naingia zaidi ya mara moja.

Ili uingie nchi ya kigeni unahitaji visa na kuna nchi kabla ya kugongewa visa nchi hizi wanapeleka taarifa zako Marekani na kwengineko kutaka kujua kama umo katika orodha ya magaidi.

Naamini hili sasa umelifahamu.

Ama nimesikitika sana umewataja masheikh waliotuhumiwa kwa ugaidi ambao wako rumande sasa mwaka wa sita na ushahidi bado haujaweza kuletwa mahakamani wahukumiwe.

Umeniumiza sana roho yangu.

Hapa ningependa kukufahamisha kuwa hakuna hata Mtanzania mmoja ambae amepata kuhukumiwa kwa kosa la ugaidi.

Nakusihi sana ndugu yangu uache hizi fitna na upuuzi huu.

Najua unachomwa na historia hii niliyoandika kuhusu mchango wa Waislam katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika lakini huu ndiyo ukweli ikiwa wazee wako hawakushiriki wala si jambo kubwa hivyo la kukuhangaisha wewe kwani isingewezekana kila mtu awemo.

Huna sababu ya kutukana watu kwa hili.
Sasa isiwe kwa kuwa nakushindeni kwa hoja mnakimbilia ''udini,'' ''ugaidi'' na maneno mengine ya kipuuzi.

Nakuwekea hapo chini mhadhara niliotoa Chuo Kikuu Cha Ibadan, Nigeria kuhusu ugaidi soma ili unifahamu zaidi isiwe unanijua kwa Saigon Club peke yake:

 
Mohamed Said,
Napenda sana unavyojenga hoja na kupresent mtiririko wa sentense, Hakika historia izungumzwe jinsi ilivyokuwa bila kuweka kificho, walio wengi mambo haya tumeyafahamu baada ya kumaliza vyuo, lakini kupitia kwako na kuendelea kusoma ukweli wa jambo hili binafsi nakupa pongezi za dhati kwa kutuelimisha Watanzania ambao hatukujua ukweli juu ya historia sahihi ya nchi yetu katika harakati za kupigania uhuru wa nchi ya Tanzania. Big up Mahamed Said kwa uandihi wako bora.
 
Napenda sana unavyojenga hoja na kupresent mtiririko wa sentense, Hakika historia izungumzwe jinsi ilivyokuwa bila kuweka kificho, walio wengi mambo haya tumeyafahamu baada ya kumaliza vyuo, lakini kupitia kwako na kuendelea kusoma ukweli wa jambo hili binafsi nakupa pongezi za dhati kwa kutuelimisha Watanzania ambao hatukujua ukweli juu ya historia sahihi ya nchi yetu katika harakati za kupigania uhuru wa nchi ya Tanzania. Big up Mahamed Said kwa uandihi wako bora.
mkuu huyu mzee wetu ana experiencr kubwa sana na mashambulizi ya maneno ya watu.

umemuona mtoa mada yuko wai si kakimbiaa?
hyo ni kutokana na ujibuji wake ambao unamtosheleza mtu na akapata kuishiwa na maswali.

kibaya zaidi(kwa wanaopinga) huyu mzee wetu ameishi nyakati hizo tunazozisoma sisi kwa hyo ana lundo na ushhidi.

wakati huo wanaompinga ni watu ambao wameisoma tu historiaaa
 
Hivi kuna mtu tajir duniani anayeweza kusema au kusemewa na watu kuwa utajiri wake kaupata yeye mwenyewe bila ya kuwa na ushirikiano na watu.

Acha kuukimbia ukweli, kutokana na historia ilivyo ya hapa Tanzania na hayo yasemwayo vyote vinahusiana..
Shida ni kukaririshwa ndo kinacho wasumbua watu...
 
Napenda sana unavyojenga hoja na kupresent mtiririko wa sentense, Hakika historia izungumzwe jinsi ilivyokuwa bila kuweka kificho, walio wengi mambo haya tumeyafahamu baada ya kumaliza vyuo, lakini kupitia kwako na kuendelea kusoma ukweli wa jambo hili binafsi nakupa pongezi za dhati kwa kutuelimisha Watanzania ambao hatukujua ukweli juu ya historia sahihi ya nchi yetu katika harakati za kupigania uhuru wa nchi ya Tanzania. Big up Mahamed Said kwa uandihi wako bora.
Mpekuzi 17,
Ahsante sana.
 
Huu ndio unaitwa UDINI. Why Mapadri? Uhuru wa nchi hii haukutafutwa kwa makundi kiasi iandikwe Historia ya Mapadri, Mashehe, Mabudha, Wapemba, Wageni, Wazawa na wengineo.

hivi kuna dini inaitwa wapemba, wageni, wazawa ???
 
Mohamed Said,
Maandiko yako Mzee Said huwa yanaishia kuonyesha kwamba Mwalimu "alibebwa" tu na TAA, kwamba hawa Waasisi wa TAA, kina Syke na Wenzake walimfanyia Mwalimu favour tu.

Ambacho huiambii Jamii ni kwamba Mwalimu alianzia wapi? umebakia kuonyesha kana kwamba Mwalimu yeye aliibuka tu ghafla.

Huna haja ya kuongelea mambo ya upande mmoja kama huna taarifa za kutosha za upande mwingine, matokeo yake unaishia kulisha Watu historia inayokosa mizania.

Hivi nikikuuliza swali, kati ya Mwalimu na TAA/Sykes brothers ni nani alimuhitaji mwingine zaidi?

Maandiko yako yameegemea kuonyesha kana kwamba Mwalimu hakuwa na nguvu yoyote na alihitaji sana mbeleko za kina Sykes, sijawahi kuona kwenye maandiko yako ukionyesha potential ya Mwalimu, ambayo kiukweli wale Wazee waliiona, na ukweli ni kwamba Mwalimu alikuwa nayo.

Kwa Mtu yeyote makini akisoma maandiko yako na hata kuwasikiliza "wenzako" kadhaa atagundua kwamba Mwalimu alikuwa na nguvu kubwa ambayo sio wewe au wenzako hao wapo tayari kuweka wazi, kwa makusudi au labda kwa kutofahamu sijui.

Wengi wenu naona mnaishia kulalamika tu na kuonyesha kwamba Mwalimu asingefanya chochote bila TAA/Sykes brothers/Waisilamu, mambo wanayotaja "tulimkaribisha kwenye nyumba hii...alitumia gari langu..nilimpa pesa kadhaa n.k" mwisho wa siku hamsemi huyu mliyemfanyia hayo yote yeye alikua na nini?.

Hutaki kusema ukweli kwamba Mwalimu alianza harakati tangu akiwa anasoma, huwezi kusema kama Mwalimu alitaka kuanzisha Chama ila alisikiliza ushauri wa kusitisha hiyo mipango na kuja kuungana na waliopo tayari, miongoni mwao ni kama hao TAA.

Kitu kingine kinachoonekana dhahiri kupitia maandiko yako na maelezo ya 'wenzako' ni kwamba hawa Waanzilishi 'wenu' wa harakati hizi hawakuwa haswa wanahitaji uhuru wa nchi, zaidi ni kama walitaka uhuru wa kidini, na zaidi walihitaji dini ya kiislamu ndio iwe kipaumbele.

Hii hoja mnayosema kwamba mlimuhitaji Mwalimu kwa sababu ni Mkristu na Waingereza wangemsikiliza ni hoja dhaifu sana na ni aibu kwa Mtu yeyote makini kuitumia, hivi ni mataifa mangapi ambayo Waingereza walitawala na yalikuwa ya kiislamu tena kwa 100%? sasa ni kwa vipi uislamu wa Tanganyika kwao ungekuwa ni big deal?

Nilichomsikia 'Mwenzako' mmoja wa Tabora anasema wawakilishi wao walipoenda Umoja wa Mataifa kuomba uhuru walifurushwa kwa sababau walienda kama kikundi cha kidini, na hizi ndio zilikuwa harakati kubwa za hawa wanaojinadi kama Wapigania uhuru...na hawakukataliwa kwa sababu ya dini yao bali uwakilishi wao uliegemea kwa dini moja...sasa kusema Mwalimu alipokelewa ili kurahisiha tu mambo sio hoja ya msingi kabisa, zaidi ni kuonyesha Wazee wetu hawa hawakuwa haswa wanajua cha kufanya.

Mwalimu alikuwa very strong, ni dhahiri wengi wa Wazee hao wa TAA walimgwaya, tofauti kabisa na maelezo yako yaliyojikita kuonyesha kana kwamba Mwalimu alikuwa Mnyonge.

TAA na Sykes walimuhitaji Mwalimu kuliko yeye alivyowahitaji wao, Mwalimu alikuwa ana nafasi ya kuchagua afanye harakati na TAA au la, aanzishe harakati zake au ajiunge na harakati nyingine zozote zilizokuwepo...naweza kusema Mwalimu alikuwa ni lulu.

Kuanzisha harakati ni jambo moja, na kujua nini cha kufanya ni jambo lingine. Mwalimu alikuwa master plan, na ukweli ni kwamba yeye ndiye aliyesisimua harakati za TAA na baadae TANU kuelekea uhuru.
 
May Day,
May Day,
Sijapata kuandika popote kuwa Mwalimu Nyerere ''alibebwa,'' kama papo tafadhali onyesha wa sijasema kuwa Abdul Sykes alimfanyia Mwalimu ''favour.''

Nilichoandika ni kuwa Abdul na mdogo wake Ally, Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir kwa kuwataja wachache walimsaidia Nyerere kwa mengi katika harakati za kupigania uhuru na hawa ni wale waliokuwa Dar es Salaam ukienda nje ya Dar es Salaam utakutana na Ali Migeyo, Salum Mpunga, Haruna Taratibu, Omari Suleiman, Paul Bomani, majina ni mengi sana lakini yote hayakuwapo katika historia hadi nilipoyaandika.

Nilichoeleza na kwa kuwa kilifutwa katika historia rasmi ni kuwa Kleist Sykes alikuwa Katibu muasisi wa African Asociation chama alichoasisi na watu hawa wafuatao: Cecil Matola kama President, Mzee in Sudi, Ibrahim Hamisi, Zibe Kidasi, Rawson Watts, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima na Mzee bin Sudi na haya majina yapo kwenye mswada wa kitabu alichoandika yeye mwenyewe kwa mkono wake kabla hajafariki mwaka wa 1949.

Mswada huu sasa ni sura katika kitabu kama nllivyokwisha eleza mara nyingi.

Pengine kama si kwa yeye kuandika mswada ule historia ya African Association yote ingepotea.

Sasa wewe badala ya kuwauliza waandishi wa historia ya uhuru kwa nini historia hii kuandikwa kusababisha kuwa na historia yenye upungufu mkubwa, umeshikila kuniuliza mimi maswali ambayo laiti ungesoma kitabu ungepata majibu yako yote.

Kuwa mimi sina taarifa za kutosha za Nyerere si kweli.

Labda iwe kwa mengine yake lakini kama ni kuhusu TAA na TANU Nyaraka za Sykes zina mengi kuhusu Mwalimu toka siku ya kwanza mwaka wa 1952 alipojulishwa kwa Abdul Sykes na Joseph Kasella Bantu.

Si haya tu nawajua hadi wale ambao walimpokea Mwalimu Nyerere na nimeona kwa macho yangu hadi ''guest wing,'' nyumba ya vyumba viwili yaani nyuma ndani ya nyumba nyumbani kwa Abdul Sykes, Mwalimu alipoishi kwa muda baada ya kujiuzulu kazi ya ualimu Pugu.

Nyuma hii nikiijua toka udogo wangu nikiingia mlango wa mbele na kutokea mlango wa uani.

Waliompokea Mwalimu mimi ni wazee wangu na hakuna popote katika mazungumzo na wazee hawa kuwa Mwalimu alifika kwao na mpango wa kuanzisha chama cha siasa Dar es Salaam.

Mipango yote ya siasa aliikuta pale nyumbani kwa Abdul Sykes tena Abdul akiwa Kaimu President na Secretary wa TAA akiwa pia mjumbe wa TAA Political Subcommittee ambao wajumbe wake walikuwa Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, John Rupia, Hamza Mwapachu, Dr. Vedasto Kyaruzi, Steven Mhando na Abdul Sykes mwenyewe.

Majina yote haya nimeyasoma katika Nyaraka za Sykes na kitu ambacho mimi kimenigusa sana ni kule kuona kuwa baba yao hawa akina Sykes kawaachia wanae kumbukumbu nyingi za AA halikadhalika wanae pia wamehifadhi kumbukumza alizoacha baba yao pamoja na zao zikianzia wakati wako vitani Burma WW II na zina maelezo yao kuhusu kuunda TANU na kudai uhuru wa Tanganyika.

Ikiwa Mwalimu alikuwa na chama cha siasa au chochote kile nje ya TAA hiyo ni historia nzuri ukaiandika ili uweke sawa ''mizania,'' chembelecho.

Kuna maswali umeniuliza mimi hayo nitayanyamazia sitakujibu kwa ajili ya kuchungua murua wangu na wa wazee wangu.

Ushauri wangu kwako ni huu, jitahidi uandike historia ya Mwalimu.

Baada ya kutoka kitabu cha Abdul Sykes kuna walioona itakuwa vyema Mwalimu na Nyerere na yeye aleleze historia yake.

Kutokana na maradhi Mwalimu hakuweza kufanya hili lakini hivi niandikapo kuna jopo linaloongozwa na Prof. Shivji wanafanya kazi hii na wamenihoji mara kadhaa na nimewapa picha kutoka Maktaba ya Sykes na nyaraka.

Tusubiri kitabu hiki kitoke.

Kuhusu ''hao wenzangu,'' mimi siwajui wala katika historia ya uhuru wa Tanganyika sijasikia kuwa kulikuwa na ''chama cha kidini kilichokwenda UNO.''

Kwa maneno kama haya ni wazi kuwa huna moja ulijualo katika historia ya TANU.
 
May Day,
Unasema maandiko ya Mzee Allama Mohamed Said lakini huweki nukuu hata moja ya hayo maandiko.

Naona umeleta yako unaswma ya @Allama Mohamed Said.

Tuwekee nukuu zake kama ushahidi zilizokufanya uandike hayo. Simpo.
 
Ahsante kwa pongezi.. Kwakweli mzee wetu ajikague upya aangalie Wapi walipokosea wao wenyewe na falsafa za dini yao.
Lililokuuma "dini yao" au wazee waliosahauliwa kwenye historia ya kivukoni na kuja kukumbukwa na Allama@Mohamed Said?
 
Back
Top Bottom