Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Mzee Mohamed Said acha kupindisha historia, ni Nyerere aliyetuletea uhuru, sio wengine

Mkuu unapopinga Pinga kwa hoja sio porojo. Mohammed Said kaeleza yake sasa wewe lete historia inayoipinga historia yake na yenye kuaminika.
Dos 2020,
Katika historia ya TANU hakuna zaidi ya hii katika chanzo cha African Association hadi kufikia TAA kisha kuundwa kwa TANU yenyewe.

Tatizo kubwa ni kuwa palipitika khiyana na historia hii ikafutwa na kwa muda ikawa imepotea ila ikiishi ndani ya vichwa vya watu waliokuwapo na kushuhudia yote kwa macho yao.

Mmoja wa watu hao alikuwa baba yangu Said Salum, Abdallah Ross (mtoto wa dada yake Adam Sapi Mkwawa ambae baba yake alikuwa Mwingereza, Ross), Mzee Mavemba, Said Kastiko na wengine wengi.

Watoto wa Abdallah Ross tumekuja kujuana ukubwani baada ya kuelezana asili zetu.

Baba yangu kamuona kwa mara ya kwanza Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey na Sikukuu mwaka wa 1952 mwaka niliozaliwa mimi.

Nyumba niliyozaliwa mimi Kipata ilikuwa jirani sana na nyumba ya Ibrahim Hamisi mmoja wa waasisi wa African Association Kipata na Congo na mwanae Abdallah Ibrahim tukifahamiana.

Jirani na kwetu Kipata na Swahili akiishi Hassan Machakaomo na binti yake Bint Hassan yu hai hadi leo na alikuwa shoga wa marehemu mama yangu Baya bint Mohamed.

Hawa akina Machakaomo baba yake Mzee Hassan ni Wazulu waliingia Tanganyika na Herman von Wissman Kamanda wa Majeshi ya Wajerumani pamoja na Chief Mohosh (Affande Plantan) na Sykes Mbuwane kutoka Imhambane kama askari mamluki kuja kupigana na Abushiri bin Salim Al Harith na Chief Mkwawa.

Abdallah Ibrahim wakati nafanya utafiti wa kitabu cha Sykes nilimhoji kuhusu baba yake na ni kutoka kwake kwa mara ya kwanza nasikia jina, ''Daffur,'' aliponiambia kuwa asili yao wao ni Daffur, Sudan.

Mbele kuvuka Mtaa wa Congo katika hiyo hiyo Kipata akiishi Abdallah Matimbwa huyu mzee wetu ameacha kumbukumbu nyingi za nyakati zile ambazo wanae wamezihifadhi hadi hivi sasa.

Nyuma ya nyumba yetu Kirk Street (sasa Mtaa wa Lindi) ilikuwapo nyumba ya Muhsin Mende, Ramadhani Mashado Plantan na nyumba ya Bi. Tatu bint Mzee.

Hawa wote wanachama wa mwanzo wa TANU na wakijuana na Mwalimu Nyerere kwa karibu sana na kote kwenye nyumba hizi mimi nilikusanya historia ya TANU.

Nakala ya gazeti la Zuhra alilokuwa akihariri Mashado Plantan nimeiona hapo nyumbani kwake Mtaa wa Lindi baadae nikakuta nakala za gazeti hili Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana.

Kipata na New Street na huku Mtaa wa Livingstone ndiko alikokuwa akiishi Kleist Sykes na wanae lakini wakati mimi nazaliwa tayari alikuwa keshafariki lakini hapo jirani Mtaa wa Livingstone akiishi mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha bint Mohamed na mkabala wa nyumba yake ndipo ilipokuwa studio ya Mzee Shebe aliyenipiga mimi picha yangu ya kwanza mwaka wa 1952/53 na ninayo hadi leo.

Mzee Shebe akaja kuwa mpiga picha wa TANU na wa Nyerere na kaacha hazina kubwa ya picha za nyakati zile ambazo baadhi nimeziona.

Wanae Mzee Shebe tumekuja kujuana pia baadae sana ukubwani.

Sasa huwa nashangaa anapotokea mtu wala Dar es Salaam ya wakati ule hakuwepo mimi naandika historia ya kwetu yeye ananishambulia na kuniita ati mimi muongo napindisha historia.
 
Tangia muarabu aanze kuja kuuza ndugu zetu ....
Si zaidi Waarabu na Waswahili walikuja kununua watumwa? Waliouza walikuwa machifu na viongozi wa kivita waliouza wafungwa wao?

(na baadaye pia Waarabu na Waswahili waliuza tena, na mwishoni watu kama Tipu Tipp walienda pia kukamata watu pale Kongo. Lakini je si chanzo cha biashara hii ilikuwa desturi ya kuuza wafungswa wa vita na baadaye mtu yeyote kama chifu alihitaji mali ya kununulia bidhaa? Na hii biashara ilianza tangu karne nyingi? Kabla Waomani kuja Z'bar!
 
Hivi mbonai George Washington ambaye ndiye baba wa Taifa USA alikuwa anavuma sana,? mbona yeye alikuwa anavuma na General Nathanael Greene hajulikani kabisa?
Abunwas,
Mbona unafananisha vitu sivyo?

1567520688398.png
 
Nimepotosha vipi hapo mkuu.. Sawa walikua wanahamasisha.. sasa niambie nini kilitokea adi akafahamika JK ndio kaletaa uhuru.. hawa wengine kiliwakuta nini..?
Da ' Vinci,
Hebu soma hapo chini naamini utapata majibu ya maswali yako:

kolorama said:
Mkuu Nguruvi heshima yako. Kwa uzoefu wangu wa jukwaa hili japo nilikuwa nasoma kama mgeni ila nimekusoma siku nyingi sana. Nakupongeza sana kwa kutoa challenge kwa maalim Mohamed Said ila lazima tukubaliane kuwa historia yetu inamapungufu makubwa na pengine niseme hayajatokea kwa bahati mbaya. Historia inakuwaga na chimbuko ili upate mtiliriko mzuri ila mengi hayajasemwa kwenye historia rasmi na ndo maana maalim yeye kajaribu kuleta yale anayojua, kama Taifa lazima tukubali kuandika historia yetu kwa usahihi kwa manufaa mapana ya jamii yetu.
Kolorama,
Umesema kweli kufutwa kwa majina katika historia ya TANU na
uhuru wa Tanganyika hakukuwa kwa bahati mbaya.

Lile jopo la waandishi wa Chuo Cha Kivukoni walikuwa wanafata
maelekezo waliyopewa vipi waandike historia ile.

Swali la kwanza la kuuliza ni nani huyu aliyetoa maelekezo ya vipi
historia ya TANU iandikwe?

Bila shaka atakuwa kiongozi mwenye nguvu sana ndani na nje ya
chama.

Katika jopo lile nilikuja kujuana na wajumbe wawili na wote makada.
Dr. Mayanja Kiwanuka na Hassan Upeka.

Hassan Upeka ni marehemu.

Huyu ni mtu wa Dar es Salaam na ni mtumishi wa kwanza kuajiriwa
na TANU 1956 alipomaliza darasa la 10 Tabora School.

Upeka alikuwa kachero wa TANU kastaafu miaka ya 1980 akiwa katika
kazi hiyo.

Hakuna kijana wa Dar es Salaam wa umri wangu aliyekuwa hamjui kaka
Upeka kwani akiogopewa kwa ile kazi yake.

Lakini hakupata kumnyayanyasa mtu yoyote kwa wadhifa wake ila nasikia
mara moja moja alikuwa akipita Mnazi Mmoja kuwatisha wauza bangi na
kuwaambia atawaletea polisi ikiwa wataendelea na kazi hiyo.

Vinginevyo alikuwa mtu mtaratibu na mkimya sana.
Labda ni kutokana na mafunzo ya kazi yake.

Upeka akinijua kama bwana mdogo tu lakini alipostaafu tukawa karibu sana.
Wakati huo mimi nishafanya mhadhara wangu wa kwanza Mnazi Mmoja na
kueleza mchango wa Waislam katika kupigania uhuru nikidai wazee wetu
wapewe heshima wanayostahili.

Cassette za mhadhara huu ziliuzwa kama maandazi ya moto.
Kila kibanda cha kuuza inawekwa na watu wamejazana wananisikiliza.

Kipindi hiki nishaandika ile makala ambayo gazeti zima lilikusanywa na
kutolewa katika mzunguko kwa sababu nilimtaja Abdul Sykes kuwa muasisi
wa TANU.

Hili lilikuwa Africa Events likichapwa London.

Makala zangu kuanzia 1990 zikawa maarufu na zikivutia wasomaji wengi.
Africa Events na New African yote magazeti ya London yakinichapa.

Katika hali hii siku moja Upeka aliniomba nende tukae faragha ofisini kwake.
Ofisi yake ilikuwa Mtaa wa Mvita, Karikaoo.

Upeka alinifungulia kifua chake kuhusu tatizo alilokutananalo wakati wa
kuandika historia ya TANU.

Akanieleza pia jinsi alivyomsaidia John Iliffe wakati ule mwalimu wa historia
Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kupata nyaraka za TAA na TANU zilizokuwa
TANU Office, Lumumba Street.

Akanieleza pia kuhusu ''notes,'' za Abdul Sykes alizoandika katika mazungumzo
na yeye kuhusu historia ya TANU.

Upeka akanambia kuwa ''notes,'' hizi zilikataliwa na jopo.
Jopo liliamua kuandika historia ya TANU bila kumtaja Abdul Sykes.


grey10.gif
Nilimuomba ruhusu nitumie mazungumzo yetu katika kitabu cha Abdul Sykes

na nitaje jina lake.

Upeka alinikubalia.
Upeka tulibaki marafiki hadi alipofariki mwaka wa 2010.
 
Mohamed Said,
Umetisha mzee wangu unajua vijana wa sasa hawana watu wa kuwasimulia mambo haya wao wanazani kila kitu kipo katika vitabu vyao vya historia vinavyosema babu zetu walikuwa manyani
 
Umetisha mzee wangu unajua vijana wa sasa hawana watu wa kuwasimulia mambo haya wao wanazani kila kitu kipo katika vitabu vyao vya historia vinavyosema babu zetu walikuwa manyani
Wazolee,
Hii ndiyo historia ya TANU niijuayo mie.

Ikiwa kuna watu wana historia nyingine isiyo hii sawa sina uwezo wala mamlaka ya kuizuia lakini muhimu ni kwa wao kustahamili historia hii nayo isikike.
 
Huyo mzee ananuka udini

Kuna kitu ameleta kwa kumnukuu mdini Mwenzake kipindi kile bwana kondo

Ati kuna mwaka wanafunzi wa kiislam walifanya mtihani wa Elimu ya msingi 71%
Na wasio kuwa waislam 29%

Hivi mtanzania mwenye akili timamu anaweza akaamini hizi porojo za Huyu mzee?

Kipindi kile bunge lote lilimdharau kondo sasa huyu Mzee anaendeleza uongo wa mzee kondo

HUJUMA ZA BARAZA LA MITIHANI DHIDI YA WAISLAM - TAARIFA YA MUFTI WA BAKWATA SHEIKH SHAABAN BIN SIMBA KWA VYOMBO VYA HABARI
Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania January 31, 2016 0

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: HUJUMA ZA BARAZA LA MITIHANI DHIDI YA WAISLAM

Kila sifa njema anastahiki Allah, ambaye rehema zake zimeenea katika kila kitu katika ulimwengu bila ya kujali utii ama uasi wa kitu hicho katika amri na sharia zake.

Rehema na amani zimuendee kipenzi chetu mtume Muhammad (S.A.W) kwa kuwa kiigizo chema na rehema kwa walimwengu wote.

Ndugu waandishi kwa muda mrefu waislam wamekuwa wakiilalamikia suala zima la utendaji wa serikali kuwa umekuwa wakibaguzi kwa kuwapendelea wakirsto kwa kuwapa nafasi mbalimbali muhimu serikalini na katika taasisi zake.

Ndugu waandishi na Waislam mnamo tarehe 01/ 05/2012 Baraza la mitihani la Tanzania lilitangaza matokeo ya kidato cha Sita, matokeo hayo yaliwashtua sana wanafunzi waislam waliofanya mtihani wa elimu ya dini ya kiislam (Islamic Knowledge). Takriban asilimia 70 walifeli kwa kupata daraja F, na asilimia 30 ndio waliofaulu tu.

Katika hao waliofaulu walipata alama za juu kabisa nchi nzima ni wanafunzi saba tu ambao wamepata daraja D, kwa matokeo haya somo hili likawa somo la mwisho kwa ufaulu nchi nzima (rejea kitabu cha takwimu cha Baraza la mitihani Tanzania April 2012.

Matokeo haya yaliwashtua wazazi na walimu wa somo hili, baadhi ya wanafunzi waliamua kukata rufaa ya kutokubaliana na matokeo hayo.

Waislam kupitia Taasisi mbali mbali za kiislam walimuandikia katibu mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi kumuomba aunde tume huru kuchunguza matokeo ya somo husika.

Kufuatia malalamiko hayo ya baadhi ya taasisi za dini, baraza la mitihani liliyatazama matokeo hayo na kugundua pia walikosea na hivyo Baraza la mitihani likaidhinisha kutolewa matokeo mapya kwa somo hilo.

Mabadiliko hayo ya matokeo ufaulu kwa wanafunzi wale wale ambao awali walifeli kwa asilimia 70, sasa yakabadilika na ufaulu ukaongezeka kwa zaidi ya asilimia 70.

Kwa namna yoyote ile itakavyokuwa dosari kubwa kama hii ni kashfa kubwa kwa Baraza la mitihani Tanzania na Serikali kwa ujumla.

Na kwa kutilia maanani muundo na historia ya utendaji wa wa baraza la mitihani la Tanzania kama nilivyoanza kuelezea, Waisla wanayokila sababu ya kuamini
kwamba matokeo haya ni uthibitisho tosha wa hujuma ambazo wanafunzi wa kiislam walikuwa wakifanyiwa kwa muda mrefu.

Na hii inatupa picha kwamba dosari hizi zilizotokea kwenye somo la maarifa ya kiislam, haziishii kwenye somo hili, bali uchunguzi ukifanyika kwa masomo yote waliofanya wanafunzi wa kiislam itadhihirika kwamba hila na dhulma kama hizi zinafanyika katika masomo mengine.

Kimsingi kwa dhulma hii waliyoifanya baraza la mitihani dhini ya wanafunzi wa kiislam, Bakwata na waislam wote kwa ujumla wamepoteza imani na baraza la mitihani la Tanzania na hasa katibu mtendaji wake.

Bakwata, linawapongeza na kuwaunga mkono Taasisi zote za kiislam nchini kwa jitihada ya kuligundua hili na hatua walizozichukuwa dhidi ya baraza la mitihani na kuhufahamisha umma wa kiislam juu ya kadhia hii.

Sheikh Ponda Issa Ponda akiomba dua kabla ya kuanza kwa maandamano dhidi ya NECTA
Tunarudia baraza tunawapongeza taasisi zote za kiislam na tunasema katika hili Bakwata tuko nyuma yao kwani kauli yao ndio kauli yetu.


Bakwata, inamshangaa Katibu mtendaji wa Baraza la mitihani (Necta) Dk. Joyce Ndalichako, kwa kauli yake aliyoitoa kupitia vyombo mbali mbali vya habari vya jana tarehe 5/06/2012, akisema hakuna hujuma na mitihani inasahihishwa na walimu wenye sifa,wanachaguliwa na na wakuu wa shule zao, walimu wenye uzoofu na kuna mfumo wa usahihishaji aliohuita “Conveyor Belt”.

Bakwata inasema hapa tatizo la msingi sio mitihani kusahihishwa na walimu wenye sifa,na nani anawachagua walimu hao wenye sifa au huo mfumo wa
usahihishaji, tatizo la msingi hapa ni kufelishwa kwa makusudi kwa wanafunzi wetu wa kiislam katika somo husika, wakati nakala za mitihani yao (Scripts) zinaonyesha wamefaulu.

Bakwata, tunahoji kwanini tatizo hili la huo mfumo (Conveyor Belt) litokee mwaka huu, mbona matokeo ya mwaka jana waislam hawakulalamika na kulikuwa hakuna dosari kama za mwaka huu iweje itokee mwaka huu, wakati mfumo ni ule ule?

Bakwata, tunaamini waislam katika hili tumehujumiwa na waislam hawajaridhishwa na majibu ya Dk. Ndalichako, aliyoyatoa kupitia vyombo vya habari vya hapa nchini.

Hiyo mifumo ya usahihishaji sio maneno matakatifu kwamba haiwezi kuchezewa kutokana hila za binadamu ni mifumo iliyowekwa na binadamu, na binadamu huyohuyo anaweza kuibadilishabadilisha vyovyote anavyotaka.
Sisi kama Bakwata,tunaamini ili kurudisha imani ya waislam dhidi ya Baraza la mitihani tunataka mambo yafuatayo yafanyike,

· Tume huru iundwe la kuchunguza Baraza la mitihani la Tanzania na utendaji wake wa kazi kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita.

· Katibu mkuu wa baraza la mitihani (Necta) ajiuzulu mara moja ili kulinda heshima ya serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzania na Baraza la Mitihani.

· Watendaji wakuu wa kitengo cha mitihani na wanaohusika na mfumo wa kompyuta ya Baraza la mitihani nao wawajibishwe mara moja.

· Hatua za kisheria na kinidhamu zichukuliwe dhidi ya watumishi wa baraza la mitihani watakaothibitika kuhusika na kashfa hii.

· Muundo wa baraza la mitihani uzingatie uwiano wa kidini, kitendo cha chombo nyeti kama hiki kujazana watu wa dini moja kunaliondolea baraza la mitihani sura ya kitaifa, kwani takwimu zinaonyesha makatibu wakuu watendaji na manaibu katibu wakuu wamekuwa wakristo na wenyevyiti wa baraza hilo ni wakristo tangu lilipoanzishwa mwaka 1973, mpaka hii leo na takwimu tunazo.

· Pia tunaiyomba Serikali iwape nafasi wanafunzi wote ambao baada ya matokeo yao kubadilishwa wamekuwa na sifa za kujiunga na vyuo vikuu waruhusiwe kuomba mikopo bodi ya mikopo, tunalisema hili kutokana na muda wa kuomba mikopo kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na elimu ya juu kwisha.

Suala la Sensa ya watu na makazi.

Kama tunavyojua kwa mwaka huu wa 2012, kuna zoezi la sense ya watu na makazi ambayo inatarajiwa kufanyika kuanzia mwezi wa nane, 2012, na kutoka na upotoshaji ulioenea kwenye vyombo vya habari hapa nchini, kalenda iliyochapichwa na ofisi ya waziri mkuu, imetoa takwimu zinazoonyesha idadi ya watanzania ni milioni 43 ambapo kwa mujibu wa dini zao wakristo ni asilimia 52, waislam asilimia 32 na dini zingine ni asilimia 16.

Bakwata tunalaani kitendo hiki na tunasema takwimu hizi sio sahihi na zinapotosha wananchi, hii ni kwa sababu katika sense zilizofanyika hivi karibuni ikiwemo sense ya mwaka 2002 kipengele kinachobainisha dini za watanzania kiliondolewa.

Kwakuwa taarifa hizi zinaonekana kwenye kalenda zinazoonyesha zimetayarishwa na ofisi ya waziri mkuu, tunaitaka serikali kurudisha kipengele kinachobainisha dini za watanzania katika sense ya mwaka huu ili ukweli ujulikane na kuondoa kabisa sintofahamu hii.

SUALA LA MGOGORO WA HIVI KARIBUNI ZANZIBAR

Ndugu waandishi wa habri naamini nyinyi nyote kama waandishi wa habari mnajua au mmesikia vurugu zilizohusisha imani za dini zilizotokea visiwani humo na kutokana na taarifa nyingi za vyombao vya habari zilizokuwa zikitolewa tangu mgogogro huu uanze kuna kila dalili za kuchukuliwa hatua za haraka haraka na katika mazingira haya wale wote waliohusika na vurugu hizi wasijulikane tena na watu wasio na hatia wakahusishwa na hali ikawa mbaya zaidi kwa hivy o kutokana na kadhia yote hiyo na yote yaliyosemwa na makundi mbalimbali ya waisla na wasiokuwa waislam Sisi kama Bakwata tunasema yafuatayo:

Kwanza tunalaani kitendo cha uvunjifu wa amani uliotokea Zanzibar na tunaamini waliofanya vurugu zote zile sio waislam bali ni wahuni tu.

Pili tunasema Wazanzibar, wasikilizwe kwa yale ambayo wanayapigia kelele kama malalamiko yao yapo katika muungano Serikali haina budi kuyasikiliza yale yote yanayolalamikiwa na kuyarekebisha, kwani Muungano sio qur- an useme kilichomo humo hakiwezi kurekebishika.

Tatu iundwe tume huru yenye wajumbe kutoka pande zote, makanisa, Serikali na UAMSHO ili zichunguzwe tuhuma hizi kwa undani zaidi maana kwa kweli athari zinaweza zikawa za muda mrefu kwani zinapandikiza kutoaminiana baina ya Wazanzibar hasa wakristo na waislam jambo ambalo halikuwepo hapo kabla na yoyote takae bainika kuwa na hatia sheria ichukue mkondo wake bila ya kujali wadhifa alionao katika chama, dini ama Serikali.

Mwisho tunamuomba Allah atupe Imani ya kweli katika nchi yetu na kama kuna fisadi na adui Allah amdhalilishe hapahapa Duniani, amen.

Wabillah Tawfiq.
Sheikh Issah Bin Shaabani Simba.
Sheikh Mkuu na Muft wa Tanzania
 
Mbona unaleta hii post hapa Hilo baraza lilikuwa linampiga vita ndalichako aondoke wizarani Kwasababu alikuwa anatenda haki

Kuna kundi la watu lilitaka ligeuze necta wawe wanafanya km wanavyotaka

Kikwete kwasababu anajua madhaifu yenu alimpumzisha Ndalichako ili kuondoa lawama. Sasa NECTA iharibu masomo ya dini inanufaika na nini?

Hakuna hujuma yeyeto NECTA ni wanaharakati kina ponda waliokuwa wanatafuta umaarufu uchwara kwa wafuasi wasiojielewa.

Je, baada ya kuondoka ndalichako nini kilitokea?

Mkuu, acha roho mbaya kwasababu kiuhalisia hakuna Muislam anayeonewa hizo ni ngojera mnatengeneza.

Mohamed Said,
 
Mbona unaleta hii post hapa Hilo baraza lilikuwa linampiga vita ndalichako aondoke wizarani Kwasababu alikuwa anatenda haki

Kuna kundi la watu lilitaka ligeuze necta wawe wanafanya km wanavyotaka

Kikwete Kwasababu anajua madhaifu yenu alimpumzisha ndalichako ili kuondoa lawama
Sasa NECTA iharibu masomo ya dini inanufaika na nini?

Hakuna hujuma yeyeto NECTA ni wanaharakati kina ponda waliokuwa wanatafuta umaarufu uchwara kwa wafuasi wasiojielewa.

Je Baada ya kuondoka ndalichako nini kilitokea?

Mkuu acha roho mbaya ya kishetani hiyo
Chuki zako na kundi lako ni kazi bure Kwasababu kiuhalisia hakuna muislam anayeonewa hizo ni ngojera mnatengeneza
Mikocheni ...
Si muhimu kwetu wewe au yeyote yule aamimi haya niyawekayo hapa.

Muhimu kwetu ni kule kujulikana kuwa lipo tatizo ndani ya jamii yetu.

Dhulma kama anaedhulumiwa hajui basi jua hakuna dhulma.

Pale anaedhulumiwa akajua kuwa anadhulumiwa hili ndilo muhimu.
 
Imeandikwa wapi hii historia
Nyerere siyo Yesu wala Nyerere siyo Muhammad.

Jamii lazima ielezwe miongoni mwa waliyochagiza mapigano ya uhuru ni akina nani mbali na Nyerere. Chama kilichodai uhuru kilianzishwa kabla ya Nyerere kuwemo ndani ya hicho chama. Basi ni lazima jamii ielezwe hao waanzilishi ni akina nani, juhudi zipi walizifanya na wapi walipokwama.

Nyerere mpaka anakikuta chama ina maana chama kiliishi. Lazima kutakuwepo na watu waliyojitolea kwa hali na mali mpaka chama kiliishi na Nyerere kukikuta. Ni lazima tuelezwe hao watu ni akina nani na mchango wao uthaminiwe na historia iwa enzi kama anavyoenziwa Nyerere kwa sababu wametoa mchango kulipigania hili Taifa.

Baada ya hapo ni lazima tuelezwe Nyerere alipatikana vipi na ni vipi aliweza kukitanua chama na kupambana dhidi ya wakoloni na nchi kuwa huru. Ajabu sehemu hii peke yake ndiyo imetunukiwa tunu ya dhahabu. Kama ni Samaki basi limezungumziwa tumbo hali ya kuwa kichwa na mkia vimeachwa, na huu si ukamilifu wa Samaki.

Nyerere hakupambana peke yake na wakoloni bali chama kilipambana pamoja naye dhidi ya wakoloni. Na ndiyo maana ya chama, na ndiyo maana ya team work. Kuleta historia ya mtu moja kanakwamba ndiyo Jemedari (one man army) wa kila kitu ni kuifanyia uhalifu historia na kuifanyia uhalifu hiyo jamii. Ni lazima tuelezwe kinaga ubaga hayo yote yalikuwaje.

Unawaeleza nini watu waliyotoa mali zao au majasho yao mpaka Chama Nyerere kukikuta? Unawaeleza nini watu waliyopambana pamoja na Nyerere dhidi ya wakoloni? Leo hii waonekane wapuuzi?credit zote ziende kwa mtu mmoja! Thats unfair.

Hakuna mjadala kwamba watu wa pwani walikuwa mstari wa mbele kwenye kudai uhuru wa nchi. Miongoni mwao hao wakazi ni wazee wa MS walikuwemo. Mzee @MohammedSaid alipotujia na kadhia ya historia ya uhuru wa nchi ukiwataja wengine mbali na Nyerere alituwekea na uthibitisho wa kile anachokizungumza.

Kisomi ili umguse @MohammedSaid kwanza pinga maneno/maandiko yake kwa hoja na wala usituletee hisia zako. Everyone is entitled to his or her own opinions but not to his or her own facts. Tunahitaji facts, usitujie na mtazamo wako.
 
Namimi naomba nikuulize unadhani kwanini afahamike JKN kama aliyetuletea uhuru ilihali kulikua na watu walioanza kabla..?
We should ask you the same question. Kwa nini hiyo hali iwe hivyo?
 
Harakati zimeanza tangu enzi za kina Mkwawa, baada ya wazungu kugawana Africa katika Mkutano wa Berlin, ndipo sasa machifu wa Kiafrika kina Mirambo, Mkwawa, Nyungu ya Mawe etc wakashika silaha kumg'oa mkoloni.
 
harakati zimeanza tangu enzi za kina mkwawa,baada ya wazungu kugawana africa katika mkutano wa berlin,ndiposaa machifu wa kiafrika kina mirambo,mkwawa,nyungu ya mawe etc wakashika silaha kumg'oa mkoloni

Elongata,
 
...Sasa huwa nashangaa anapotokea mtu wala Dar es Salaam ya wakati ule hakuwepo mimi naandika historia ya kwetu yeye ananishambulia na kuniita ati mimi muongo napindisha historia.
Kwa mara ya kwanza kabisa umekuwa mkweli kwa nafsi yako kwamba unaandika historia ya kwenu na wazee wako na hapo hata mimi nakuunga mkono, una haki ya kushangaa.

Tatizo linakuja pale unapoanza kudai unaandika historia ya kwetu na wazee wetu halafu huishii hapo unaenda mbele zaidi na kudai unaandika historia ya Tanganyika! Hapo sikuungi mkono katika juhudi zako za kujaribu kuipindisha historia yetu.

Tanganyika haikuwa na kabila la Wazulu wala kabila la Wamanyema na kwa bahati tupo ambao tulisoma kitabu kinaitwa Watanganyika kilichoorodhesha makabila ya Tanganyika kabla na baada ya uhuru.

Ukoo wa Sykes na ukoo wa babu yako hawakuwa Watanganyika katika hizo nyakati unazodai kuanzishwa kwa vuguvugu la kudai uhuru. Unadanganya pia unapodai kuwa wao ndio mwaka 1929 walianzisha chama cha TAA.

Chama cha TAA hakikuwa chama cha kudai uhuru na kilianzishwa na aliyekuwa Gavana wa Tanganyika wakati huo ili kuwaunganisha wazawa waliokuwa wafanyakazi wa serikali. Lengo la kuanzishwa kwa TAA ilikuwa ni kuwapa fursa hawa wafanyakazi wapate sehemu ya kustarehe na kubadilishana mawazo baada ya kazi.

Hata nyumba waliyokuwa wakikutania walipewa na huyo huyo Gavana wa kikoloni na Rais wake wa kwanza aliitwa Cecil Matola.

Bila shaka mpaka hapo wasomaji wataanza kujiuliza mbona Cecil Matola, Myao na mwalimu aliyekuwa na ushawishi mkubwa hadi kuchaguliwa kuiongoza TAA humtaji? Mbona hii hadithi yako inawataja wengine tu hapo juu na kumsahau muasisi na Rais wa kwanza kabisa wa TAA aliyeiongoza hadi kufariki kwake? Je ni kwa sababu hakuwa Mzulu? Je ni kwa sababu hakuwa Mmanyema? Au ni kwa sababu alikuwa Mtanganyika mzawa!

Naona hilo tuliache na hebu sasa tuje kwenye kuzaliwa kwa TANU mwaka 1954. Nani alileta wazo kwamba sasa muda muafaka umefika kwa chama cha TAA kubadilisha malengo yake na kuwa chama cha kudai uhuru? Ni nani alisimamia na kuongoza mabadiliko hayo na kuchaguliwa kuwa Rais wake wa kwanza? Ni nani aliweza kuwaunganisha Watanganyika wote bila kujali rangi, jinsia, kanda, kabila wala dini kuunga mkono harakati za TANU?

Kwaherini, nawatakia mjadala mwema...!
 
Mzizi wa Mbuyu,

Ndiyo inavyoishia baada ya kuweka ushahidi baada ya ushahidi ghadhabu zinapanda na matusi kutolewa.

Huwezi tena kujadili wala kuiambia akili yako kuwa huenda kweli lipo tatizo katika nchi yetu.

Akili imekimbia na nafasi yake imejazwa na ghadhabu.

Ninapomfikisha mtu katika hali hii kwa hoja zangu, ushahidi na maneno ya upole mimi inakuwa kazi yangu nimeikamilisha.

Sina sababu tena ya kujadili chochote na yeye kwani siwezi kujibu lugha za kifedhuli.

Kama kusoma nimekwisha msomesha.
 
harakati zimeanza tangu enzi za kina mkwawa,baada ya wazungu kugawana africa katika mkutano wa berlin,ndiposaa machifu wa kiafrika kina mirambo,mkwawa,nyungu ya mawe etc wakashika silaha kumg'oa mkoloni
Then mbona wanalazimisha kua Islams ndio walianza kupigania uhuru?
 
Mag3,

Aliyemtaja Cecil Matola ni Kleist Sykes kwenye mswada wa kitabu chake alichoandika kabla ya kufariki kwake 1949.

Kumtaja Cecil Matola kama Rais Muasisi wa African Association Kleist akiwa Katibu muasisi na mkutano wa kuasisi chama ulifanyika nyumbani kwake Cecil Matola Mtaa wa Masasi.

Nyumba hii ikaja kununuliwa baadae na John Rupia na ipo hadi leo.

Mswada huu ukaandikwa kama seminar paper na mjukuu wa Kleist, Aisha Abdul Sykes 1968 wakati mwanafunzi University of East Africa, Dar es Salaam akisoma History and Education.

Hii paper iko Department of History na inapatikana University of Dar es Salaam Library East Africana.

Mwaka wa 1973 hii seminar paper ikatiwa kwenye kitabu alichohariri John Iliffe, "Modern Tanzanians," "Kleist Sykes The Townsman."

Hii nimekuwekea kukufahamisha kuwa historia ya wazee wetu ndiyo historia ya Tanganyika.

Mimi nikapokea alipoacha dada yangu Aisha Abdul Sykes nikamwandika Kleist katika "The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika," (1998)kwa anuani hii: "Kleist Sykes (1894 -1949) Man of Ideas."

Harvard na Oxford University Press New York wakaniomba nimwandike tena Kleist katika Dictionary of African Biography (DAB)(2011).

Mtafute Cecil Matola katika Name Index ya kitabu cha Abdul Sykes utamuona.

Ipe historia hii ya babu zangu jina lolote upendalo mimi sina tatizo lakini hawa ndiyo waliounda African Association (1929), Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (1933)na TANU 1954.

Haya yalifanyika baada ya kifo cha Cecil Matola 1933 na nafasi yake kuchukuliwa na Mzee bin Sudi.

Huyu Mzee bin Sudi alikuwa Mmanyema.

Msukumo wa vyama hivi ndivyo vilivyokuja kuunda TANU.

Hakuna anaeweza kunifutia historia hii.

Sasa Mag 3 ingia hapo chini umsome babu yangu Salum Abdallah Mwekapopo:

 
Mohamed Said,

Shukrani ziende kwa waanzilishi wa harakatii ila tunamthamini alietufikisha tulipokua tunahitaji (FREEDOM) ..
Tunakubali sawa japokuwa JKN sio muhasisi wa harakati ila amepokea kijiti na kukifikisha sehemu ambapo wahasisi walishindwaa kukifikisha na hapo ndo utambuzi, heshima na uweledi wa JKN unatofautika na watu wengine waliokuwepo kweny harakati.... .
 
Yes, Leicester City ilikuwepo miaka mingi ikipambana kuwania ubingwa, lakini ni mpaka alipoiongoza Claudio Ranieri ndio ilitawazwa kuwa mabingwa wa EPL. Kwa maneno yaliyonyooka, Claudio Ranieri ndio ameipa Leicester City ubingwa kwa uongozi wake.
Vipi marehemu Vichai Srivaddhanaprabha hapewi sifa yake na je historia haimtambui mchango wake katika ubingwa wa Leicester city!?

Mie nilivyomuelewa mzee Mohamed said hampingi nyerere ila anaweka historia sawa inayojaribiwa kufichwa kizazi kwa kizazi.
 
harakati zimeanza tangu enzi za kina mkwawa,baada ya wazungu kugawana africa katika mkutano wa berlin,ndiposaa machifu wa kiafrika kina mirambo,mkwawa,nyungu ya mawe etc wakashika silaha kumg'oa mkoloni
Historia za kina mkwawa ziko wazi.

Na ndio anachokitaka mzee Mohamed said, kuwa historia ya kina Sykes na wanaharakati wengine iwe wazi, mchango wao utambulike
 
Back
Top Bottom