Mzee mwanakijiji na Humphrey Polepole mbona mpo kimya kuhusu ufisadi wa Lugumi!!?

Mzee mwanakijiji na Humphrey Polepole mbona mpo kimya kuhusu ufisadi wa Lugumi!!?

Kwani Ukishajua baadhi yetu misimamo yetu basi huwezi kiwa na shaka tuko upande gani. Hatuko kama wale wanaochukua misimamo kwa kuangalia maslahi ya kisiasa. Hatuna mashaka juu ya uwezo wa Magufuli kumtumbua yeyote inapobidi. Sisi siyo wahamisha magoli.
haaaaahaaa kakaa nimeipenda nilijua tumepiga udalali hatakuniacha cha tochi hukukijijini...
 
Wanajamvi
Salaam;

Kwa sasa habari kubwa kwenye vyombo vya habari vyote,ni kuhusu ufisadi wa kutisha unaohusisha jeshi la police na baadhi ya viongozi akiwemo waziri wa mambo ya ndani Charles kitwanga na kampuni yake ya INFOSY.

Hawa jamaa niliowataja hapo juu,tangu wakati wa kampeni walijipambanua km wapinga ufisadi wa kweli na waliunga mkono mabadiliko waliyoyaita ya kweli na kuyaacha yale waliyoyaita mabadiliko ya kuzungusha mikono.

Nasikitika tangu kashifa hii ishike kasi,sijawaona kabisa hawa jamaa popote pale wakiongelea hili. Najua wote ni ma-member hapa tena wanaoheshimika,hebu wajitokeze tusikie kauli yao juu ya hili sakata. Bado nafasi za kuteuliwa zipo wasife moyo.
Mzee mwanakijiji nafasi ya msemaji wa ikulu bado inakaimiwa na Gerson msigwa na Bw. Polepole nafasi za ukuu wa wilaya na ubunge wa kuteuliwa bado zipo. Maoni yenu yanaweza kumshawishi mkuu akawaangalia mmempigania sana!

Nawasilisha.
Tangu lini ukamuona mtanzania wa sasa anajipiga risasi?
 
Wanasubiri mwongozo,,, Hawawezi kuanza kuzungumza mpaka kikao cha Lumumba kikae kiwaelekeze nini cha kwenda kusema.
Ni kwa sababu nape jana alikuwa anakagua uwanja wa taifa hivyo hakupata nafasi ya kuwaeleza cha kuongea
Cc[emoji14]olepole
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji lengo langu siyo kujua upande ulipo. Wengine mbali na hilo tungependa tu kuona maoni yako ukilizungumzia pengine inaweza kusaidia kumwamsha yule mliyempigania. Maana nae ktk hili speed imepungua sana...!!
Hao wote ni machumia tumbo tu,wapi ritz,wapi lizaboni
 
Mbona Wenyeviti wote wa UKAWA wamepata ganzi ya kuzungumzia hili jambo! Au masuala ya Ufisadi kwao linatakaswa?
1460642188341.jpg
 
Hao waganga njaa wa fisiemu tuh na ni watumwa wa fisiemu.
 
Basi wewe uwe wa kwanza ili utowe Mfano Kwa Kondoo wenzako.Maana mnalilia kila kunapokuchwa.Hovyooooo
Nasikia siku hizi mnashindia ndege wa porini kutokana na uhaba wa chakula,agwe solowenyo!!!!
 
Nikisema uchaguzi umekwisha mtakubali? Au uchaguzi umeisha tunapozungumza wengine?
Hili la Lugumi halina uhusiano sana na uchaguzi, ila ni vizuri mnaowatetea wakasikia kauli zenu humu kuwa je ni vyema kulizima suala linalowagusa wakubwa waliopo na waliokuwapo madarakani, au la!
 
Nasikia siku hizi mnashindia ndege wa porini kutokana na uhaba wa chakula,agwe solowenyo!!!!
Alee usolowenyu nyenye.
Ndege lazima waliwe wamejaa sana.
Tunawapunguza.Tuna wakaribisha msije Mkaanza kulilia BUREE.
 
Hili la Lugumi halina uhusiano sana na uchaguzi, ila ni vizuri mnaowatetea wakasikia kauli zenu humu kuwa je ni vyema kulizima suala linalowagusa wakubwa waliopo na waliokuwapo madarakani, au la!
Huyo jamaa hawezi kukujibu anarukaruka kama maharage tu kipindi kama hiki ndio utajua wanafiki wakubwa ndani ya nchi hii
 
Kuanzia leo, kila polepole unapoanza kujadili mada yoyote inabidi uwe unaambatanisha na matokeo yako ya shule ili watu wasipoteze muda kutathimini upeo wa ubongo wako.!
 
Back
Top Bottom