Kwani Ukishajua baadhi yetu misimamo yetu basi huwezi kiwa na shaka tuko upande gani. Hatuko kama wale wanaochukua misimamo kwa kuangalia maslahi ya kisiasa. Hatuna mashaka juu ya uwezo wa Magufuli kumtumbua yeyote inapobidi. Sisi siyo wahamisha magoli.
Sikubaliani na wewe kabisa.
Haki inabaki kuwa haki tu. Na haki ina pande mbili ya kutiwa hatiani au kuachiwa huru.
Kesi yoyote inaanza kama tuhuma.
Kila ufisadi ulianza kama tuhuma na tetesi kwenye vyombo vya habari.
Wewe kama mtu uliyejipambanua kama mpigania haki hutakiwi kukaa kimya mpaka wengine wapige kelele. Ukweli utakapo bainika ndipo uje upige kalele za kupongeza.
Piga kelele za kutaka ukweli ujulikane na haki itendeke.
Hili ni suala nyeti kwa taifa
Haiwezekani liwe linachunguzwa na mamlaka ile ile inayojaribu kwa kila namna kulificha jambo hili.
Nilitegemea uwe umetoa kauli ya kumtaka Rais kuunda tume ya majaji wanaheshimika sana walichunguze jambo hili kwa kina na kuliweka wazi ili kuondoa upotoshaji unaozagaa.
Kwa nini nasema Mh. Rais aunde tume ya k
Majaji kwa sababu jambo hili limeenda mbali zaidi kwa kuwataja watu wengi akiwemo mwanafamilia wa rais mtaafu na Waziri mwenye dhamana ya wizara. Huyo waziri sio kutajwa tu bali ametajwa kama rafiki wa karibu sana wa Rais Magufuli. Hapo haki itaeleweka vipi kwa wananchi bila kuliundia tume maalumu. Tume hiyo ni lazima ifanye kazi yake bila kujali maslahi ya posho zilizoea kutengwa kwa mamilioni kwenye tume zilizokua zinaundwa .Itumie gharama ndogo kutupa ukweli.
Tayari tumeshaambiwa ama kwa kudanganywa au huenda kuna ukweli kuwa Kitwanga na Magufuli ni Rafiki wa ukweli. Sasa hatutaki amuonee au avunje urafiki wake kwa tetesi. Lakini pia hatutaki apuuzie tetesi kwa kulinda urafiki wao. Na hatutaki jambo hili kubwa lifanyike au lichunguzwe kwa siri.
Kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe.
Urafiki, udini,ukanda ,ukabila,ushabiki ,undugu na uchama tuuweke pembeni kwanza.
Wote tumelikuta taifa hili na wote tutaliacha.
Hakuna chama wala dini wala kabila wala mtu mmoja aliyemwomba Mungu na kumshawishi ili aweke rasilimali zote zilizopo kwenye nchi hii. Zote ameziweka kwa mapenzi yake kwenyewe. Hivyo ni vema tukawakataa wote wanaotaka kuzifanya zimewekwa kwa hisani yao.
Cha msingi taifa letu tuliache katika maendeleo ya wote na historia bora yenye ukweli na uadilifu.