Mwinyi hakusema "katiba ivunjwe", alisema katiba "ifikiriwe kubadilishwa" kipengele cha ukomo wa raisi ili Magu aendelee,--- hayo yalikuwa ni maoni ya Mwinyi kama Rais mstaafu, kama raia mwenye haki zote za kutoa maoni kama jinsi wewe unavyotoa hapa.
Katiba inaweza kubadilishwa na imeshafanyika hivyo mara kadhaa kukidhi haja ya wakati, Katiba sio Qur'an au Biblia, katiba ni sheria zilizotungwa na Bunge, hoja ni hii; ni Bunge gani lingekaa kwa wakati ule/ huu kubadilisha hiyo katiba, kimsingi Mwinyi alikuwa anamfurahisha Magu (kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa) ili kumtengenezea njia Hussein.
Hata kama ingewezekana katiba ibadilishwe mimi binafsi sikubaliani na mawazo ya Mwinyi ambayo yasingeweza kutekelezeka.