6 Pack
JF-Expert Member
- Apr 17, 2022
- 2,819
- 5,996
Habari zenu wana JF wenzangu, ama baada ya salam ningependa sasa nijielekeze kwenye mada husika.
Kwa wale mliofatilia kipindi cha mashujaa wetu huko Dodoma, bila shaka mmemuona mzee huyu mwenye umri wa miaka 102, akiwa anadunda kwa ukakamavu wa hali ya juu tena kwa kujiamini.
Mzee huyu amenifurahisha pale alipoonekana kujua kila analolifanya bila kupoteza kumbukumbu yoyote. Tofauti kidogo na mzee wetu mzee Ally Hassani Mwinyi ambae husahau hata majina ya watoto wake. Huyu amekumbuka mpaka kupiga saluti katika ngao ile ya mashujaa.
Mungu aendelee kumpa umri mrefu mzee huyu na mashujaa wetu wengine walio hai. Ningeishauri serikali ikampa tunzo ya heshima mzee huyu, na ikiwapendeza watafute mtaa mmoja huko jijini Dodoma katika makao makuu ya nchi na waupe mtaa huo jina la mzee huyu ili kumuenzi kwa mchango wake mkubwa kwa taifa letu.
Nawasilisha.