TANZIA Mzee Paul Sozigwa, aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Mwalimu Julius Nyerere afariki Dunia

Kumbe wazee humu tumebaki wachache sana...mkiambiwa sisi ni watu wazima huwa mnatukejeli, "mzee uwe wewe. ..wazee walishakufa " nyie mabinti kwa msemo wenu wa sasa... Mungu anawaona.
Aiseee.. MUNGU akuhurumie mzee binti ameuliza swali matokeo yako unatoa povu badala ya kumpa jibu sahihi
 
Yule Mzee Mkongwe na Gwiji la siasa l za Tanzania Mzee Sozigwa amefariki Dunia.Rest in peace Mzee wetu
Poleni wafiwa. Hawa wazee,tutawakumbuka kwa uzalendo wao. Sina uhakika kama ipo taasisi endelevu,inayoweka kumbukumbu sahihi za kiutendaji za hawa wazee wetu. Tuna mengi ya sisi wa sasa na wajao ya kujifunza kutoka kwao! Lengo,tuwe na muendelezo wa yale mema waliyotuachia!
 
Huyu Mzee alikuwa Mzaramo muadilifu sana na muumini mkubwa wa ujamaa inasemwa hata kuliko Mwalimu Nyerere. Kuna wakati gazeti la "Mfanyakazi" zama hizo lilitoa picha yake akiwa anatembea huku soli ya kiatu chake ikawa imechakaa ajabu!
 
Tufafanulie alimpigiaje ,simu wakati miaka kulikuwa hakuna simu za mkononi?
 
Mnyaazi Mungu amrehemu na amchagulie pia panapomstahili...

Si vizuri kumuongelea hapa, ila sijui alitumia vigezo gani mpaka kufikia kusema JK hafai..
Uhafidhina ndio umelifelisha hili taifa kwa kung'ang'ania ujamaa huku misingi ya ujamaa inawashinda.. Nyerere alileta ujamaa hapa halafu akashindwa kuusimamia na bado akawa mbishi kwa kitu ambacho kimemshinda mwishowe impact zake zinatafuna vizazi..
 
Alikoswakoswa kudhulumiwa nyumba na mke Mdogo sijui iliishia wapi?
 
Tufafanulie alimpigiaje ,simu wakati miaka kulikuwa hakuna simu za mkononi?
Mtu ameshakufa unataka kuchimbachimba ya Nini,wewe sema rest in peace halafu ishia zako
 
Hazina ya kumbukumbu na utendaji uliotukuka imeondoka...RIP, comrade, Mzee Paul Sozigwa....
 
RIP Mzee Sozigwa. Msalimie JKN mwambie huku wanakuiba kila siku lakini ngoma yako haichezwi na wanao uliowakabidhi mji. Salamu hizo zimfikie EMS na RMK pia. AMEN!!!!!!!!!!!!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…