Uchaguzi 2020 Mzee Shomari: Uchaguzi wa mwaka huu ni kama wa mwaka 1995 ila mwaka huu mgombea wa CHADEMA ameingizwa chaka

Lisu kapewa hiyo nafasi kama sehemu ya matibabu yake na sio kwakua ana sifa za kugombea Urais na kushinda.

Chadema waliona wakimpa nafasi agombee anaweza pata nafuu kidogo, na kweli bwana ukimuona lisu kwa sasa ana recover.

Tupo tunauguza mgonjwa na sio mpinzani halisi kwa nafasi ya Urais.
 
Tumekaa miaka 5 no siasa, na Leo watu wana uitikio wa Aina Ile kwa upinzani then yy anaongea madudu gani?
 
We jamaa hamna kitu kabisa. Nani aliyekwambia mkulima akiuza popote nchi inakosa mapato.?

Unaelewa mapato yanakusanywa vipi?

Kajipange kwanza.
 
Wewe ndio umeingizwa chaka,
mzee shomari nimemuona kwenye zomea zomea ya kagera..hamtaki jiwe hata kidogo..maana zao la kahawa limemshinda jiwe, pamoja na kukaa madarakani miaka yote mitano mbaya zaidi anasahau kuwa aliahidi 2015 amechemsha sasa ana ahidi tena kuhusu kahawa 2020.
 
Miradi ya CCM ni miradi ya 10% ni miradi ya kifisadi mtupu
 
Hii ni 2020 mwaka wa maajabu bora ukae kimya na usubirie matokeo.

Hakuna mtremko hapo mbele kuna kona kali na mlima mkali
 
Andaa mwili; watakuja kukusulubu muda mfupi ujao
 

Kwa mtu anayejuwa siasa anafahamu fika nani atashinda huu uchaguzi sababu ianafahamika kuwa kuna mgombea anapofanya mkutano inabidi kasi ma ofisini zisimame na watu wanatishiwa kuwa kutakuwa na kuandikisha majina. Watu wanasombwa na malori, wasanii wakubwa ambao wanaweza kujaza watu bila ya kuwepo mkutano wowote ndiyo wanaotumika. Hivi hapo bila hizo juhudi kutakuwa na watu kweli kwenye mkutano wa CCM kama hawatalazimisha wafanyakazi hawatasomba watu na malori hawatakiwepo wasanii. Ukijibu hilo swali ndo utafahamu kama mgombea gani atashinda.

Pili maisha ya watanzania sasa hivi ni magumu sana siyo mjini siyo kijijini wanachohitaji ni mtu wankuwaambia ni kwanini maisha yao yamekuwa magumu basi na hilo ndilo linalofanywa na Lissu. Sioni kwa namna gani CCM wanaona uchaguzi huu ni rahisi.

Hakuna kipindi uchaguzi umewahi kuwa mgumu kama safari hii, ukiangalia uchaguzi wa mwaka 1995 upinzani ulikuwa haujajulikana na pia hakukuwa na utandawazi kama leo ambapo mtu anahutubia Tunduma ujumbe unafika nchi nzima. Lakini pia Mrema alikuwa siyo mpinzani wa kweli kwahiyo hakuwa anaaminika maana na pia uelewa wake ulikuwa mdogo sana.

Mwaka 2015 mgombea alikuwa hana uwezo wa kuongea na kishawishi wapiga kura watu wengi walikuwa wanajitokeza lakini hawashawishiki sababu alikuwa hawezi kuongea zaidi ya dk 5 hivyo hawakuweza kushawishika hata baada ya kufika kwenye mikutano.

Lissu ana uwezo mkubwa wa kushawishi anaelewa mambo mengi sana na anauwezo mkubwa was kujenga hoja na kujibu hoja pia hivyo ana ushawishi mkubwa sana. Sifa nyingine ni mpinzani wankweli na pia CHADEMA wamekuja na sera nzuri ambayo ina jibu matatizo ya umasikini wa wananchi wakati nchi yetu ni tajiri. Suluhu ni serikali za majimbo ili kuweza kusimamia vizuri rasilimali za nchi.

Hizo ndiyo sababu zitakazo mfanya mgombea wa CHADEMA kufanya vizuri na kishangaza watu wengi
 
Muuaji mkubwa wa upinzani ni Mbowe kwani ndiye aliyekuwa kiongozi rasmi wa kambi ya upinzani; ameivuruga CHADEMA mpaka sasa imekuwa chama cha wababaishaji tu.
 

Kuhusu kununua Ndege na kujenga uwanja kifisadi ni kweli sababu mwaka 2017 imetungwa sheria kuwa mikataba yote mikubwa itakuwa inapelekwa bungeni sasa kwanini mikataba ya Ndege haijapelekwa bungeni na kwanini ATCL haijakaguliwa tangu Ndege zinunuliwe.

Kuhusu uwanja wa chato kwanini umejengwa bila kuwepo na business plan mtu anaamka tu na kujenga uwanja kijijini kwake hata tenda haijulikani ilitangazwa lini huo siyo ufisadi nini basi maana manunuzi ya umma ya sheria zake na yanafanyika kwa uwazi kunapokuwa na usiri ndiyo ufisadi wenyewe unavyofanyika.

Tundu Lissu aendeleze moto huo huo kila mtanzania ada hamu kwamba sasa ufisadi unafanywa na nani. Watanzania wana kumbuka Prof Assad alipoonesha upotevu wa trillion 1.5 akaondolewa kazini kila mtu anajuwa kwanini aliondolewa sasa watanzania wataamuwa tarehe 28/10
 
Wale waliomwingiza chaka kugombea wakati huu nawapa 'hi five' ili ashindwe, agalagazwe vibaya, amalize zamu yake na aondoke zake, atuachie chadema tuijenge upya. Hatuwezi kuwa na kiongozi mropokaji namna hiyo.
 
Mimi ninacho kumbukumbuka hata wajinga wanazeeka.. vilevile
 
Acheni siasa kwenye uchumi, nani kasema bidhaa ikiuzwa nje nchi inakosa mapato, kila nchi ya dunia hii inajaribu kubalance books of payment, huwezi kuagiza bidhaa nje kama huuzi nje, na kumbuka kila kitu tunaagiza kwa asilimia kubwa.
Nimeongelea huo upotoshaji mengine sihusiki nayo na sina comment
 
Ingia field, kuna upinzani? Kama hata wabunge wa upinzani hawana pesa ya kampeni. Nini kinafuata?
Nini maana ya upinzani?
Je, upinzani ni vyama au watu?
Ninachojua, a real battle btn Magu & Lissu, Magu kufikisha even 50% ni ngumu kwake. Ila kwa kuwa dola imeamua kum-favour, basi hata kwa magumashi wameamua lazima atangazwe kwa zaidi ya 90%.
 
Kongole mzee shomari. Ushindi 96%,kwa CCM this time. Tuwaletee maendeleo watanzania.
 
Nini maana ya upinzani?
Je, upinzani ni vyama au watu?
Ninachojua, a real battle btn Magu & Lissu, Magu kufikisha even 50% ni ngumu kwake. Ila kwa kuwa dola imeamua kum-favour, basi hata kwa magumashi wameamua lazima atangazwe kwa zaidi ya 90%.
Lissu kufikisha 50% ya kura alizopata lowasa itakuwa ngumu Sana.
 
Yaani anajazwa upepo na Watu wa mitandaoni ID Kumi kumi
bila kujua hawa ni Vibendera tu
ngoja Atakiona
 
Sawa kuna mantiki gani kusema wakulima wa korosho wauzie nchi za nje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…