sblandes
JF-Expert Member
- Apr 25, 2010
- 6,632
- 4,737
Spika Six na Spika Anna Makinda waliruhusu mijadala bungeni kwa maslahi mapana.Kuna wakati mzee Slaa alikua anakuja na hoja za ufisadi na ushahidi Ukiwa kamili mezani. Zito alikua anakuja na hoja Za ufisadi wa serikali na uthibitisho Ukiwa mezani kabisa. Angalia ishu ya Escrow ya akina Kafulila Unakuta watu wanakuja na vielelezo wazi kabisa.
Richmond iliiangusha serikali kwasababu Watu walikua na ushahidi wa wazi na wananchi wanakubali na serikali inakabwa koo. Sasa wapinzani sasa hivi Wamepwaya sana kwenye hoja zaidi unasikia mazungumzo Kama yakwenye vijiwe vya Kahawa yanazungumzwa na mpaka wagombea urais.
Tuombe Tupate upinzani imara kabisa Kama nyakati zilizopita ili serikali ichangamke. Kukiwa na upinzani wenye hoja, vithibitisho tutarudi enzi za upinzani unaoichachafya serikali na wananchi tunapata burudani ya Siasa na maendeleo juu.
Pammoja wapinzani kuzoa viti vingi 2015 kulinganisha na huko nyuma lakini Spika Ndugai aliwadhibiti 99.9 %hakuwapa nafasi yoyote ya kutupa makombora mazito.