Uchaguzi 2020 Mzee Shomari: Uchaguzi wa mwaka huu ni kama wa mwaka 1995 ila mwaka huu mgombea wa CHADEMA ameingizwa chaka

Kuna wakati mzee Slaa alikua anakuja na hoja za ufisadi na ushahidi Ukiwa kamili mezani. Zito alikua anakuja na hoja Za ufisadi wa serikali na uthibitisho Ukiwa mezani kabisa. Angalia ishu ya Escrow ya akina Kafulila Unakuta watu wanakuja na vielelezo wazi kabisa.

Richmond iliiangusha serikali kwasababu Watu walikua na ushahidi wa wazi na wananchi wanakubali na serikali inakabwa koo. Sasa wapinzani sasa hivi Wamepwaya sana kwenye hoja zaidi unasikia mazungumzo Kama yakwenye vijiwe vya Kahawa yanazungumzwa na mpaka wagombea urais.

Tuombe Tupate upinzani imara kabisa Kama nyakati zilizopita ili serikali ichangamke. Kukiwa na upinzani wenye hoja, vithibitisho tutarudi enzi za upinzani unaoichachafya serikali na wananchi tunapata burudani ya Siasa na maendeleo juu.
Spika Six na Spika Anna Makinda waliruhusu mijadala bungeni kwa maslahi mapana.
Pammoja wapinzani kuzoa viti vingi 2015 kulinganisha na huko nyuma lakini Spika Ndugai aliwadhibiti 99.9 %hakuwapa nafasi yoyote ya kutupa makombora mazito.
 
Wahenga wanasema usimdharau mtu usiyemjua. Sababu huwezi kujua huyo mtu anajua nini au ana maarifa gani kukuzidi wewe. Mzee Shomari japo ni muuza kahawa anajua mambo mengi. Ni mzee darasa la nne la mkoloni lakini ana uwezo wa kudadavua mambo.

Mwaka 1995 mgombea wa NCCR mageuzi Lyatonga Mrema aliichachafya Ccm kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi. Lakini Ccm ilipo jitafakari na kujirekebisha alijuwa wazi awamu ya pili hawezi tena kuwasumbua Ccm hivyo alikuwa mpole na Ccm ikachukua ushindi.

Ni wazi kabisa CCM mwaka 2015 Lowassa aliwachachafya CCM, lakini ukweli ni kuwa wamejirekebisha na sasa hakuna chama ambacho kinaweza kuwapa presha au jambajamba. Maana ni wazi kuwa CCM itashinda kwa 96% wabunge, madiwani na urais.

Mzee Shomari anasema ni wazi kuwa Tundu Lissu ameingizwa mkenge kuwania nafasi ambayo CHADEMA walijua fika kwa awamu hii hawawezi kuipata hata kwa udi na uvumba.

Lissu ameingizwa mkenge na Mbowe ndio maana hata badala ya kunadi sera na ilani ya chama chake amebaki kuleta siasa za kishamba za uropokaji majukwaani. Mfano mgombea urais unaweza eti utaruhusu wakulima wa korosho kuuza nchi yoyote wanayoitaka! Yaani mkulima wa korosho akauzie Msumbiji, na Tanzania unayoiongoza isipate mapato.

Ni aibu mgombea urais kuzua ufisadi ambao hauna ushahidi, kama kudai uwanja wa ndege Chato na ndege za ATCL zimenunuliwa kifisadi bila kuweka ushahidi. Sisi wapiga kura tulitarajia Lissu aweke nyaraka za ukweli juu ya ufisadi.

Ukweli ni kuwa Mbowe ulijuwa Lissu alitakiwa kugombea Ubunge au udiwani,ila umemuingiza chaka. Na mbaya zaidi umemuacha peke yake afanye kampeni,ndio maana anaropoka hovyo.
hali ukiendelea kubwabwaja utashtukizia Lisu yuko ikulu
 
Ushindi wa zaidi ya 90% unatamkwa sana na wana-ccm wakiongozwa na katibu wao. Inaelekea ushindi umeshapangwa kabisa, kinachosubiriwa ni kutangazwa tu. Kwamba iwe mvua liwe jua, lazima Magufuli atangazwe kwa zaidi ya 90%.

Lengo ni kutaka kuvunja kwa lazima record ya JK (2005).
Kuna kura za marehemu na ambao hawatapiga kura ndio wanazojivunia.
 
Ni aibu mgombea urais kuzua ufisadi ambao hauna ushahidi, kama kudai uwanja wa ndege Chato na ndege za ATCL zimenunuliwa kifisadi bila kuweka ushahidi. Sisi wapiga kura tulitarajia Lissu aweke nyaraka za ukweli juu ya ufisadi.
Au huelewi maana ya ufisadi ndugu? Naona unatokwa povu tu bure.
Maamuzi ya kujenga uwanja wa ndege wa Chato ulipitishwa na bunge gani?

Tenda ya ujenzi wa uwanja huu ilitangazwa?

Fedha za ujenzi wa uwanja huu zilipitishwa na bunge lipi?

Basi huu ndiyo ufisadi wenyewe. (Nenda kajielimoshe uelewe maana ya UFISADI, mimi sitakuambia).
 
Ahaaa,unachekesha sana boss. Bajeti kuu ikishapitishwa basi ujue hiyo pesa inaweza kutumika kwa shughuli yoyote. Ndio maana kuna pesa za uhuru zinajenga hospital Dodoma.

Kama huo uwanja ulijengw bila kufuata taratibu, kwa nini halmashauri ya mji wa Geita ilibariki ujengwe?
 
Slaa alikuwa anasema ufisadi anaweka naushahidi mezani zitto alikuwa anasema ufisadi anaweka naushahidi mezani Sasa Lisu huu ufisadi wake ambao hauna ushahidi no upi? Kama unabeti vilee
 
Wahenga wanasema usimdharau mtu usiyemjua. Sababu huwezi kujua huyo mtu anajua nini au ana maarifa gani kukuzidi wewe. Mzee Shomari japo ni muuza kahawa anajua mambo mengi. Ni mzee darasa la nne la mkoloni lakini ana uwezo wa kudadavua mambo.

Mwaka 1995 mgombea wa NCCR mageuzi Lyatonga Mrema aliichachafya Ccm kwenye awamu ya kwanza ya uchaguzi. Lakini Ccm ilipo jitafakari na kujirekebisha alijuwa wazi awamu ya pili hawezi tena kuwasumbua Ccm hivyo alikuwa mpole na Ccm ikachukua ushindi.

Ni wazi kabisa CCM mwaka 2015 Lowassa aliwachachafya CCM, lakini ukweli ni kuwa wamejirekebisha na sasa hakuna chama ambacho kinaweza kuwapa presha au jambajamba. Maana ni wazi kuwa CCM itashinda kwa 96% wabunge, madiwani na urais.

Mzee Shomari anasema ni wazi kuwa Tundu Lissu ameingizwa mkenge kuwania nafasi ambayo CHADEMA walijua fika kwa awamu hii hawawezi kuipata hata kwa udi na uvumba.

Lissu ameingizwa mkenge na Mbowe ndio maana hata badala ya kunadi sera na ilani ya chama chake amebaki kuleta siasa za kishamba za uropokaji majukwaani. Mfano mgombea urais unaweza eti utaruhusu wakulima wa korosho kuuza nchi yoyote wanayoitaka! Yaani mkulima wa korosho akauzie Msumbiji, na Tanzania unayoiongoza isipate mapato.

Ni aibu mgombea urais kuzua ufisadi ambao hauna ushahidi, kama kudai uwanja wa ndege Chato na ndege za ATCL zimenunuliwa kifisadi bila kuweka ushahidi. Sisi wapiga kura tulitarajia Lissu aweke nyaraka za ukweli juu ya ufisadi.

Ukweli ni kuwa Mbowe ulijuwa Lissu alitakiwa kugombea Ubunge au udiwani,ila umemuingiza chaka. Na mbaya zaidi umemuacha peke yake afanye kampeni,ndio maana anaropoka hovyo.
mbona hueleweki unakuwa kama CHANGU WA UWANJA WA FISI....
Mbona kauli hii ni yako na si ya hako Kazee uchwara kalikokunywa maji ya bendera
 
Wewe umejua vipi? Huwa unakuja kunywa kahawa kwenye kijiwe chetu? Kwa us..ulionao unatakiwa mtu akunywee alikasusu.
 
. Mfano mgombea urais unaweza eti utaruhusu wakulima wa korosho kuuza nchi yoyote wanayoitaka! Yaani mkulima wa korosho akauzie Msumbiji, na Tanzania unayoiongoza isipate mapato.

Ni aibu mgombea urais kuzua ufisadi ambao hauna ushahidi, kama kudai uwanja wa ndege Chato na ndege za ATCL zimenunuliwa kifisadi bila kuweka ushahidi. Sisi wapiga kura tulitarajia Lissu aweke nyaraka za ukweli juu ya ufisadi.
Kwani mkulima hawezi kuuza korosho zake msumbiji? Ni mfumo tu. Na akiuza msumbiji haina maana kuwa serikali itakosa mapato - ni utaratibu tu. Anafika mpakani analipa kodi sahihi.
Juu ya ufisadi, anachodai lisu ni mikataba ya ununuzi wa ndege; tuna sheria ya manunuzi, je ilifuatwa? Kama haikufuatwa, kwa nini, nini kinafichwa? Uwanja wa Chato hivyo hivyo, kampuni iliyojenga iliteuliwa katika mchakato wa wazi? - kama si hivyo kwa nini?
Majibu kwa lisu ni rahisi - ni kumweleza kuwa sheria ya manunuzi ya uma ilifuatwa - basi
 
Huyo mzee naona amezeeka zaidi akili kuliko mwili.

Mtu yeyote mwenye akili anajua kabisa uchaguzi wa safari hii hakuna mgombea atakayeshinda kwa zaidi ya 70%.

Duniani kote, kama kuna uchaguzi wa kidemokrasia, hakuna ambaye huwa anashinda kwa zaidi ya 80. Ni kwenye tawala za kidikteta tu ndiko ambako Rais huweza kupata ushindi wa zaidi ya 90%, ambayo kwa ujumla ama huwa ni matokeo ya wizi wa kura au hutokana na kutangaza matokeo tofauti na kuwa zilizopigwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna wakati mzee Slaa alikua anakuja na hoja za ufisadi na ushahidi Ukiwa kamili mezani. Zito alikua anakuja na hoja Za ufisadi wa serikali na uthibitisho Ukiwa mezani kabisa. Angalia ishu ya Escrow ya akina Kafulila Unakuta watu wanakuja na vielelezo wazi kabisa.

Richmond iliiangusha serikali kwasababu Watu walikua na ushahidi wa wazi na wananchi wanakubali na serikali inakabwa koo. Sasa wapinzani sasa hivi Wamepwaya sana kwenye hoja zaidi unasikia mazungumzo Kama yakwenye vijiwe vya Kahawa yanazungumzwa na mpaka wagombea urais.

Tuombe Tupate upinzani imara kabisa Kama nyakati zilizopita ili serikali ichangamke. Kukiwa na upinzani wenye hoja, vithibitisho tutarudi enzi za upinzani unaoichachafya serikali na wananchi tunapata burudani ya Siasa na maendeleo juu.
unataka uthibitisho na ushahidi gani zaidi ya report za CAG?
 
NA WEWE UKAKUBALI KABISA KUINGIZWA CHAKA NA MZEE SHOMARI?
KWANI MZEE SHOMARY ALIONA UCHAGUZI WA MWAKA 1995 WAGOMBEA WAKIKATWA KWA MADAI YA KUTOKUJAZA FOMU VIZURI KAMA MWAKA HUU?
 
Na
Kwa hiyo unamdharau? Mbona Lissu anadegree lakini anaropoka pumba? Hivi unaweza kuruhusu korosho na mazao ya biashara yakauzwe nje?
Natumai wewe ndiye mzee Shomari mwenyewe,maana hoja ya mazao umekomalia kwelikweli.Ni ndoto yetu Sisi wakulima na wafanyabiashara wa mazao kuuza nje ya nchi ili tupate faida na fedha za kigeni.
 
Back
Top Bottom