Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi

Mzee Tashrif kafariki leo na kazikwa leo. Waislam wanajua heshima, umuhimu na maana ya mazishi

Yaani Mtu ameshakata roho (Amekufa) halafu anaendelea kupata maumivu kisa hajazikwa???

Maumivu anapataje na hana hisia zozote na nerves zote zimekufa??

Sheikh tuache pls [emoji23]
Unaamini maiti inasikia?
 
Tunarudi palepale Uislam hauendeshwi kwa busara na maoni yako msimamo wa uislam ni mtu akifa azikwe haraka
Wewe unayo hiyari ya kufata tararibu za uislam au ujitoe katika taratibu za uislam hulazimishwi katika hilo kaweke mochwari hata siku 6
Again no counter-points.....ubishi tu. Wewe hata dini ikikuambia mkate mtu kichwa huta question
 
Nimeona kila sehemu watu wanasema kama marehemu kazimia tu inakuaje, inapaswa wajue Waislamu hawaziki mtu bila report ya daktari na vipimo kupita kuthibitisha kifo.
Km amezimia kwenye process ya kuoshwa lazima ashtuke maana kwenye hii process wanafanya vitu ambavyo kwa namna yoyote mtu km hajafa lazima ushtuke.
 
Kaa kimia huna elimu yeyote kuhusu sheria za kiislam na tena mwenyezi mungu amekemea vikali tabia ya kuongea kitu usicho kuwa na elimu nacho.
Suala la kuzika lipo kisheria na sio matakwa ya mtu fulani.
Angalieni hili topolo lingine. Unabisha ujinga bila facts. Mwenzako katoa maoni yako, wewe weka points ku argue sio unatema shudu zilizojaa hasira. Unataka umpige kobazi ya uso?
 
Kwahiyo hadi leo hiyo teknolojia haipo ya kuhifadhi mwili? Vp wanaitumia? Sheria za uislam kwenye Mazishi ziko vile vile wewe usitumie utashi wako.

Mbona hujataka kubadili mtindo wa kuswali?

Huna akili
Oneni hili topolo lingine hapa linatetea utamaduni wa kiarabu kwa kumtukana mmatumbi mwenzake.

Ptuuuu mate usoni. Nimekudharau mwarabu mweusi kutoka kwa mpalange madukani
 
Maoni yako hayazingatiwi katika Uislam.

Sasa ndio umeandika nini? Muongozo wa Mtume hauendi kinyume na Qur-an. Uko wapi wewe na maneno ya Allah;

وَمَآ ءَاتَىٰكُمُ ٱلرَّسُولُ فَخُذُوهُ وَمَا نَهَىٰكُمْ عَنْهُ فَٱنتَهُوا۟

Whatever the Messenger gives you, take it. And whatever he forbids you from, leave it.
(Qur-an 59:7)



Sasa msikilize Mtume;



Sahih al-Bukhari 1315
Narrated Abu Huraira:
The Prophet (ﷺ) said, "Hurry up with the dead body for if it was righteous, you are forwarding it to welfare; and if it was otherwise, then you are putting off an evil thing down your necks."

حَدَّثَنَا عَلِيُّ بْنُ عَبْدِ اللَّهِ، حَدَّثَنَا سُفْيَانُ، قَالَ حَفِظْنَاهُ مِنَ الزُّهْرِيِّ عَنْ سَعِيدِ بْنِ الْمُسَيَّبِ، عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ ـ رضى الله عنه ـ عَنِ النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم قَالَ ‏ "‏ أَسْرِعُوا بِالْجِنَازَةِ، فَإِنْ تَكُ صَالِحَةً فَخَيْرٌ تُقَدِّمُونَهَا ‏{‏إِلَيْهِ‏}‏، وَإِنْ يَكُ سِوَى ذَلِكَ فَشَرٌّ تَضَعُونَهُ عَنْ رِقَابِكُمْ ‏"‏‏.‏

Reference: Sahih al-Bukhari 1315
In-book reference: Book 23, Hadith 72
USC-MSA web (English) reference: Vol. 2, Book 23, Hadith 401
(deprecated numbering scheme)
Report Error | Share | Copy ▼


Jami` at-Tirmidhi 1075
Ali bin Abi Talib narrated that:
The Messenger of Allah said to him: "O Ali! Three are not to be delayed: Salat when it is due, the funeral when it is presented, and (marriage) for the single woman when someone compatible is found."

حَدَّثَنَا قُتَيْبَةُ، حَدَّثَنَا عَبْدُ اللَّهِ بْنُ وَهْبٍ، عَنْ سَعِيدِ بْنِ عَبْدِ اللَّهِ الْجُهَنِيِّ، عَنْ مُحَمَّدِ بْنِ عُمَرَ بْنِ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ، عَنْ أَبِيهِ، عَنْ عَلِيِّ بْنِ أَبِي طَالِبٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ لَهُ ‏ "‏ يَا عَلِيُّ ثَلاَثٌ لاَ تُؤَخِّرْهَا الصَّلاَةُ إِذَا آنَتْ وَالْجَنَازَةُ إِذَا حَضَرَتْ وَالأَيِّمُ إِذَا وَجَدْتَ لَهَا كُفْؤًا ‏"‏ ‏.‏ قَالَ أَبُو عِيسَى هَذَا حَدِيثٌ غَرِيبٌ وَمَا أَرَى إِسْنَادَهُ بِمُتَّصِلٍ ‏.‏

Grade:Sahih (Darussalam)
Reference: Jami` at-Tirmidhi 1075
In-book reference: Book 10, Hadith 111
English translation: Vol. 2, Book 5, Hadith 1075



Sababu hii ndio alitupa Mtume? Unajua kama Mtume alikuwa haongei kwa matamanio yake? Allah ambaye ni Mjuzi wa kila kitu, ambaye ndio kamfunulia Sharia atufikishie sisi, anajua zaidi.

Mambo hayapelekwi hivyo. Na dini haipelekwi kwa matamanio. Hata zamani kulikuwa na mbinu za asili za kuhifadhi maiti kwa muda mrefu lakini Sharia imesema azikwe haraka.

Mazishi ni ibada lakini sio ya wajibu kwa watu wote wawepo kuitekeleza. Wakipatikana wachache wakaitekeleza wanawatosheleza wengine wote. Ni Faradh kifaya, wakipatikana baadhi tu wakaitekeleza wengine wote wataondokewa na wajibu. Maiti haiwezi kucheleweshwa kwa sababu ulizotoa.

Maoni yako binafsi hayazingatiwi.

Kuzika mapema ni katika Uislam.

Mwisho nakunasihi ndugu yangu pamoja na kuinasihi nafsi yangu, tusilete matamanio yetu binafsi katika dini. Tuifuate Qur-an na Sunnah juu ya Ufahamu wa Salaf.

Allah aniongoze mimi na wewe katika njia iliyonyooka.

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍۢ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى ٱللَّهُ وَرَسُولُهُۥٓ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ ٱلْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ ٱللَّهَ وَرَسُولَهُۥ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَـٰلًۭا مُّبِينًۭا ٣٦

It is not for a believing man or woman—when Allah and His Messenger decree a matter—to have any other choice in that matter.1 Indeed, whoever disobeys Allah and His Messenger has clearly gone ˹far˺ astray.

(Qur-an 33:36)

adriz Kazakh destroyer Kisai
Huu ni muongozo katika uislamu.Ukiwa muislamu lazima uufuate.
 
Hulazimishwi kufata utaratibu wa kiislam unayo hiyari ya kujitoa katika taratibu za kiislam na ukafata busara zako ukaweka hata mwezi mzima maiti
Duh, yaaani wenzio wanatema points wewe unatema shudu. Embu kama huna cha kuchangia kaa kimya kuliko kudhihirisha ujinga wako hapa
 
Mimi ni muislam lakini katika suala la kuwahisha mazishi niko kinyume na wengi.

Kuzika haraka mtu anapofariki sio muongozo wa quran bali ni maelekezo ya mtume wetu kutokana na wakati wao hakukuwa na teknolojia ya kuhifadhi maiti ili ikae muda mrefu.

Pia kutokana na joto la huko jangwani ikawa ni rahisi maiti kuharibika upesi, lakini pia kutokana na kukosa mawasiliano ya simu wakati huo ikawa sio rahisi kuwapelekea taarifa watu waliopo mbali ili wawahi mazishi, kwa hiyo mtume kwa hekima akasema kati ya mambo yanayotakiwa kufanywa haraka basi mazishi ni mojawapo.

Sasa kwa kuwa nyakati zimebadilika, teknolojia imekua kwa maana maiti inaweza kuhifadhiwa muda mrefu na pia wafiwa pengine wapo mbali na taarifa wamepata kupitia simu au whatsapp, je kuna ubaya gani kuchelewesha mazishi kwa sababu mazishi pia ni ibada mtu akihudhuria anapata thawabu.

Haya ni maoni yangu binafsi kwa sababu kuna Uislam na Uarabu, kun mambo inabidi kuyafuata kama Uislam unavyosema lakini pia kuna masuala ya utamaduni wa kiarabu ambao huku kwetu hauko applicable sio mbaya kama tutaacha huo utamaduni bila kuathiri dhima ya Uislam.
Ni muislam soma suratul nnajim inasema hivi "Haiwi anachokisema Muhammad isipokua ni wahyi kwenu"hvyo usidharau Sunna za Mtume S.A.W kaka,halafu mambo manne ya haraka kwa muislam mojawapo akifa azikwe haraka sana na Kuna hadithi nadhani inasema maiti akifa azikwe km kheri akakutane nayo na Shari pia akakutane nayo
Halafu kuzika ni faradhi ila sio lazima uwepo au usiwepo atazikwa tu
Suala la kuweka maiti inaweza kua zuri au baya pia
Ila aliyekufa amekufa hata akikaa mwaka Ndo kafa huyu
baby zu
 
Sio hvo tu marehemu anapakwa shedo lipstick...jaman ifike muda Mungu TUMUOGOPE haya mapokeo ya Dunia yatatupeleka pabaya siku ya kiama
Sasa ndo umeongea nini hapa? Wewe ukimpenda na kumthamini mtu akishakufa unaacha kumpenda na kumthamini? Nimekudharau ndugu ALUWATAN
 
Angalieni hili topolo lingine. Unabisha ujinga bila facts. Mwenzako katoa maoni yako, wewe weka points ku argue sio unatema shudu zilizojaa hasira. Unataka umpige kobazi ya uso?
Umeshaambiwa kuwa Uislam haungozwi kwa fact kutoka kwenye kichwa cha mtu bali unaongozwa kwa Qruan.
Qruan imesha toa miongozo yote kuanzia kuishi ,kuoa, kuzika ,suala la kuzikwa lipo kisheria ndani ya Quruan na sio mawazo ya mtu binafisi.
 
Aah kumbe ni biashara hapo sawa
 
Muslims wako smart sana kwenye mambo yao. Haitumiki busara ya mtu bali miongozo ya vitabu.

Uislaam umetoa miongizo namna ya kumuhudumia maiti baada yamtu kufariki mpaka mazishi.

Ukristu ni vurugu mechi kila mtu anafanya limfaalo yeye. Hakuna maelekezo wala miongozo ya kufuata .

Mtu akifariki ni maamuzi yenu marehemu azikwe ama akae tu hata mwaka.

Ndio maana wakristo utakuta marehemu kafa ana wiki mbili manjemba hayashtuki wala nini.

Wakristu akifariki maskini anaweza kuzikwa siku hiyo kuondia bugudha.

Akifariki tajiri hatua ya kwanza inaundwa kamati ya msiba na kutengeneza majukumu.

1. Kutengeneza sare za msiba
2. Kukodi mziki mzuri mzito wa kuburudisha waombolezaji
3. Kuandaa usafiri marehemu akazikiwe kwao kakonko
4. Kuandaa vyakula na vinywaji kwa muda usio eleweka kama sio walokeole hapa msiba utageuka kilabu ya pombe.

Wakristu wenzangu sijui tunakwama wapi?
Umeandika pumba tupu wewe pimbi
 
Mkiambiwa msome dini yenu muielewe maana yake ni kuepusha rai za kibinadamu zinazoweza kuleta hasara, Sasa huoni tu hapa unapuyanga tu kwa akili zako binafsi wakati ushaambiwa kabisa mkitaka kupata ukweli juu ya jambo lolote basi rejeeni katika Quran na Sunna. Dini sio maoni ya kila mtu ila ni muongozo kamili na muongozo huo unapatikana kwenye Quran na Sunna, Sasa haya sijui technology unayatoa katika lipi kwenye hiyo miongozo? Quran ishaweka sawa toka kuumbwa kwa Dunia mpaka mwisho wake hakuna kitu hakina jibu lake. Unachotakiwa kujua tu ni kwamba wewe ni maamuma unahitaji kusoma dini yako uijue.
Badala uweke counter-point, unaandika kujinasibu namna wewe unaijua dini. Hopeless
 
Uislam hauendeshwi kwa mawazo na busara zako, uislam unaendeshwa kwa kufata Quran na Sunnah

Katika uislam mambo matatu yanatakiwa yafanywe haraka.
1.Mtu anapohitaji kuoa aozeshwe haraka
2.Mtu anapotaka kuslim asilimishwe haraka
3.Mtu anapo fariki azikwe haraka.

Huo ndo uislam kila kitu kimefundishwa katika uislam had staili ya Kutembea, kula&Kunywa, kuvaa, kulala, kuamka, kiiila kitu kimefundishwa na huo ndo unatakiwa uwe mwenendo wa waislam na siyo burasa zako na maoni yako.
Nashukuru Kwa nondo zako bro
Na mtume anasema Uislam ulikuja mgeni na utaondoka ukiwa mgeni pia yaani hakuna anaejua zaidi ya aliyeuleta tu ,sisi tunafata miongozo Quran na Sunnah
 
Back
Top Bottom