Ndio maana nimeweka hapo kuwa ni maoni yangu binafsi na sio msimamo wa uislam, mimi sio mfuata kila linalosemwa kwa sababu natambua uislam asili yake sio huku kwetu na pia ni karne nyingi zimepita lazima mabadiliko yawepo.
Maelekezo ni kuwa mtu akifa inatakiwa azikwe haraka wakati huo, now lazima nifanye reasoning kwa nini ilisemwa hivi, nagundua ala kumbe wakati huo hakukua na teknolojia kubwa katika uhifadhi wa maiti, mawasiliano, uchukuzi n.k. Lakini uzuri zaidi imesisitizwa tu kuwa mazishi yafanyike haraka, hakuna palipotajwa kuwa yafanyike haraka kwa kiasi gani kwa hiyo kwako wewe masaa mawili unaweza kutafsiri kwamba ni haraka, yule akatafsiri haraka ni masaa sita na mimi nikasema haraka ni siku tatu, hakuna tatizo hapo.
Mimi sio kama wewe unafuata lolote bila kufanya reasoning, chochote kikitamkwa ni lazima kina sababu nyuma yake.