Mzee wa CHADEMA Zanzibar aliyezungumzia udini alikuwa anapeleka ujumbe gani?

Mzee wa CHADEMA Zanzibar aliyezungumzia udini alikuwa anapeleka ujumbe gani?

Mzee kasema maneno ya udini kwamba Hussein Mwinyi muislam na Samia Hassan muislam na Mahmoud Kombo, waziri wa mambo ya nje, muislam na Masauni, waziri wa mambo ya ndani Muislam, tena wote Wazanzibari, wajiunge na kujiingiza OIC haraka kabla hajaja rais Mkristo kuweka zengwe.

Kauli hizi zinavunja misingi ya katiba za Tanzania, Zanzibar na CHADEMA ambayo inakataza siasa za udini. Siasa za ubaguzi wa kidini.

Angejivua uongizi wa CHADEMA na kwenda kusema hayo maneno kwenye platform nyingine. CHADEMA hakina ajenda ya udini, kinaunganisha watu wa dini zote na wasio na dini.

Zaidi, Mzee amechochea na kuzipa nguvi dhana za kwamba sasa hivi Wazanzibari wameshika bara na visiwani wanafanya mambo yao kuweka maslahi ya Zanzibar juu ya maslahi ya Tan,ania. Dhana hii ni mbaya sana na inaweza kusababisha mpasuko.
 
Unafanya utani katika jambo lisilo hitaji utani, mkuu 'Benja'. Nilitaka kunyamaza tu, lakini nimeshindwa.

Nisilaumu, pengine wewe hiyo ndiyo njia inayo kusaidia kuondoa maumivu tunayo pewa na hawa waTanzania wenzetu!
Kwa bunduki hatuwawezi kama ni maongezi hawataki, bora tutumie nguvu za giza zitusaidie kwa haraka
 
Mozambique ina waislam 18% only na ni mwanachama tangu 1994
Gabon ina waislam 11.2% na ni mwanachama tangu 1974

Togo only 14% islam ni mwanachama since 1997

Muwe mnachungulia kwanza kabla ya kueneza chuki
OIC = Organisation of Islamic Cooperation.

Hebu tafisiri kwa kiswahili ili tujue tunakosea wapi.
 
Hakuna chuki yeyote hapo. Watu wanahoji tu benefit zake.

So far hao Uganda au Mozambique wamebenefit nini kwenye huo ushirika...!!?
 
Kwa nini hawajitoi miaka 45 baada ya idd amin kutolewa madarakani?!

Hilo wanajuwa wenyewe .... there are a lot of possible reasons. Sitaki kuspeculate hapa.

Tuelezeni faida za kujiunga na OIC ili wote tujue. Maana mpaka sasa hatuji hata hao Uganda wamefaidika nini .... wako hohe hahe tu siku zote.
 
Mozambique ina waislam 18% only na ni mwanachama tangu 1994
Gabon ina waislam 11.2% na ni mwanachama tangu 1974

Togo only 14% islam ni mwanachama since 1997

Muwe mnachungulia kwanza kabla ya kueneza chuki
Sahihisho dogo. Mozambique ni observer. Baadhi ya nchi zilitegemea kupokea misaada mikubwa lakini hili halijatokea hadi sasa. OIC imekuwa zaidi jukwaa la kupiga porojo za kisiasa kuliko kuchochea uchumi na maendeleo. Angalia nchi waasisi kama Nigeria, Mali, Sudan, Tchad n.k. ni vurugu tu hata amani na usalama ni shida.
 
Hilo wanajuwa wenyewe .... there are a lot of possible reasons. Sitaki kuspeculate hapa.

Tuelezeni faida za kujiunga na OIC ili wote tujue. Maana mpaka sasa hatuji hata hao Uganda wamefaidika nini .... wako hohe hahe tu siku zote.
Kwani faida ya kujiunga umoja wa mataifa nini nini,mbona bado mpo hohehahe?
 
OIC = Organisation of Islamic Cooperation.

Hebu tafisiri kwa kiswahili ili tujue tunakosea wapi.
Hilo ni jina tu,
Kuna watu wanaitwa MATATIZO, FIMBO, MAGUFULI, MWANAMVUA, JOHNSON, PEPPER, sasa hapo ukitafsiri kwa maana ndio utapata nini?

Hembu tutafsirie = RED CROSS

Acheni woga, mnaogopa mpaka majina duh,
 
Sahihisho dogo. Mozambique ni observer. Baadhi ya nchi zilitegemea kupokea misaada mikubwa lakini hili halijatokea hadi sasa. OIC imekuwa zaidi jukwaa la kupiga porojo za kisiasa kuliko kuchochea uchumi na maendeleo. Angalia nchi waasisi kama Nigeria, Mali, Sudan, Tchad n.k. ni vurugu tu hata amani na usalama ni shida.
AU,UN, na mitaasisi kibao ya siri siri na ya kugereshea imechochea nini hadi sasa?
Acheni chuki, woga na udini
Mnakataa maendeleo kwa udini tu?
 
Back
Top Bottom