Mzee wa Jambia: Ukimtoa Mayele Yanga ubora unapungua kwa 50%

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Kupitia kipindi cha michezo cha efm, Wilson Oruma amekaririww akisema kwa kikosi cha Yanga ya sasa ukimtoa Fiston Kalala Mayele basi ubora wa Yanga unapungua kwa 50%

Akaongeza zaidi, Mayele pekee yake kwa ubora wake anaibeba Yanga kwa asilimia 50%. Hivyo ili Yanga iwe vizuri inahitaji ubora wa Mayele.

Alikuwa akiyazungumza hayo kuelekea mchezo wa kesho wa Marumo Vs Yanga ambapo wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika watashuka dimbani wakijaribu kutafuta matokeo ya kuwawezesha kutinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Je unakubaliana na maoni ya Wilson Oruma " Mzee wa Jambia"
 
Mimi kwa mtazamo wangu Oruma kazingua, Yanga ya sasa inacheza zaidi kitimu kuliko kumtegemea zaidi mtu mmoja mmoja.

Namkumbusha aangalie mchango mkubwa wa kipa, Diarra ambaye aina yake ya kucheza imeisaidia sana timu kwa utulivu wake.

Pia aangalie mchango wa Mwamnyeto ambaye nae kajitahidi sana kuboresha kiwango chake.

Wapi Ibrahim Bacca?
 
Majizo kwenye vituo vyake vya habari hasa vipindi vya michezo, ameokota watu mapoyoyo wanatafuta attention tu... Hawana akili hawana exposure, wao kilasiku ni kuichambua Yanga na Simba hata kama hazichezi watalazimisha wajadili...
 
Ni makanjanja.
 
Kupitia kipindi cha michezo cha efm, Wilson Oruma amekaririww akisema kwa kikosi cha Yanga ya sasa ukimtoa Fiston Kalala Mayele basi ubora wa Yanga unapungua kwa 50%

Akaongeza zaidi, Mayele pekee yake kwa ubora wake anaibeba Yanga kwa asilimia 50%. Hivyo ili Yanga iwe vizuri inahitaji ubora wa Mayele.

Alikuwa akiyazungumza hayo kuelekea mchezo wa kesho wa Marumo Vs Yanga ambapo wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika watashuka dimbani wakijaribu kutafuta matokeo ya kuwawezesha kutinga fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza.

Je unakubaliana na maoni ya Wilson Oruma " Mzee wa Jambia"
Katika timu kila mchezaji ana umuhimu wake na majukumu yake. Timu ina beki kazi yake kuzuia timu isifungwe, ina viungo ambao wanaunganisha timu na kuna washambuliaji wamesajiliwa kufunga. Kwa kauli hiyo anabeza nafasi nyingine na kumsifia mtu mmoja.

Hii Yanga hata magoli imefungwa machache, magoli manne tu kwenye mechi sita za makundi za kombe la shirikisho na mtoano haijafungwa kwa maana ya mechi mbili za robo na moja ya nusu fainali. Makundi ilifungwa magoli tisa Mayele kafunga matatu kati ya hayo. Sasa atasemaje Mayele ubora wake ni nusu ya timu. Tujaribu tu kukubali ubora wa Yanga hata kidogo.
 
Mimi kwa mtazamo wangu Oruma kazingua, Yanga ya sasa inacheza zaidi kitimu kuliko kumtegemea zaidi mtu mmoja mmoja.

Namkumbusha aangalie mchango mkubwa wa kipa, Diarra ambaye aina yake ya kucheza imeisaidia sana timu kwa utulivu wake.

Pia aangalie mchango wa Mwamnyeto ambaye nae kajitahidi sana kuboresha kiwango chake.

Wapi Ibrahim Bacca?
Kaka usisahau kumtaja Dickson Job
 
Hilo jina lenyewe la huyo mchambuzi ndiyo nalisikia leo. Hivyo siwezi kumhukumu.

Inawezekana ndiyo zile sampuli za akina Bin Kazumari.
 
Mkuu huyu ndio yule aliyesema "shughuli Yao imeishia hapa" baada ya Yanga kutoa sare na Club Africain uwanja wa taifa
 
Ukimtoa haaland ubora was man city unapungua kwa 70%

Ukimtoa vini jr ubora wa Madrid unapungua kwa asilimia 40

Jamaa akachambue mchele tu
 
Kuna wachambuzi wengine hawajui nini maana ya %! Kwahiyo muacheni tu anaropoka ili mkono uingie kinywani
 
Back
Top Bottom