Mzee wa upako: Haina maana Samia Suluhu anafurahia kifo cha Magufuli, ni ramani ya Mungu. Adai Magufuli alimwambia 'alideep' Urais

Mzee wa upako: Haina maana Samia Suluhu anafurahia kifo cha Magufuli, ni ramani ya Mungu. Adai Magufuli alimwambia 'alideep' Urais

Ni kawaida hiyo, madaraka kama Rais Mungu huwapa watu aliowachagua na haiwi bahati mbaya bali kwa. Sababu maalumu..

Ndio maana huwaotesha watu,ukiangalia watu wengi Sana walitabiri miaka mingi Sana Rais Samia kuwa Rais wa JMT kwa kutumia jina la Mwanamke..

Kwa hiyo mnaojihangaisha sijui kumuangusha mnapoteza mda,Mungu ndio atamtoa kama alivyomtoa Mwendazake.
Kweli Mungu anasingiziwa vingi! Mnafanya mchezo na Mungu wewe pamoja na hawa matapeli kama anayejiita mzee wa upako.
 
Mzee wa upako akiwa kwenye kongamano la viongozi wa dini la kumuombea na kumpongeza Rais Samia ameongelea kuhusu uongozi na ameongelea jinsi viongozi wa Tanzania walivyopatikana ikiwemo Samia, Magufuli na mwl Nyerere.

Mzee wa Upako(Anthony Lusekelo): Wakati Jakaya anamaliza uenyekiti wa chama, sherehe yake ya mwisho wakiwa Singida, Samia alikuwepo pale kama makamu wa Rais. Mwisho wa sherehe, Jakaya alimuita makamu wa Rais, Samia akasimama akaenda, Jakaya akampa mkono.

Mimi moyo wangu ulishtuka nilikuwa naangalia TV, usiku saa nane nikampigia simu Jakaya. Nikamwambia mheshimiwa ule mkono uliompa Samia, ingekuwa kwetu ningekwambia umemuachia upako wa ufalme, ule mkono haukuwa wa kawaida, akasema mie nilikuwa nampa mkono, ule mkono una jambo.

Haina maana kwamba Samia Suluhu anafurahia kifo cha Magufuli, ni ramani ya Mungu, Mungu alijua kwamba John ataishi miaka hii ataondoka, nani ataongoza nchi hii, akatazama mioyo ya watanzania wote akaenda Unguja akampata Samia, akamuingiza katika mfumo wa uongozi ndio nyota ikawaka.

Pia mzee wa upako amesema alibahatika kuongea na John Magufuli, akasema hata yeye hakufikiria kuwa Rais wa Tanzania na alichukua fomu alikuwa 'anadeep'. Anadai Magufuli alimwambia aliota kiti cha ufalme, sauti ikamwambia akae akakataa lakini akalazimishwa.

Pia mzee wa Upako amemuongelea Kambarage ambae anasema alikuja Dar kama mwanachama aliyevaa kaptula na hakutegemea kuwa mwenyekiti wa chama cha ukombozi, amesema kwenye chama chao hawakuangalia udini kwani waislamu walikuwa wengi lakini akawa mwenyekiti na akaacha alama ya kujenga umoja na mshakamano wa waafrika.

Mzee wa upako amesema watu wanaodhani Samia hajachaguliwa kwasababu hakupigiwa kura ni sawa hata ikiwa hivyo kwani kwenye biblia watu wote ambao walifanya makubwa hawakupigiwa kura. Amesema alipoteuliwa makamu wa Rais alisita.

Mwisho amesema kiongozi hakubaliki kwao.

View attachment 2245461
Kwamba uncle aliota "Kiti Cha Ufalme'' sauti ikamwambia akae akakataa, lakini akalazimishwa.

Mimi sikatai maana sikuwepo alipoota, bt nachokijua ni kuwa Mzee wa Lupaso alimwambia chukua fomu.

Tatizo la Watawala wengi wanaipenda waotewe ndoto nzuri nzuri tu, ndoto za maonyo hawazitaki.

Waotaji jukwaani tunamuona haendelei Awamu ingine bt wanapuuza. Anashauriwa ktk utawala wake iandikwe KATIBA mpya. itakuwa ZAWADI na ALAMA Kwa vizazi vingi vijavyo. Amen
 
Back
Top Bottom