Mzee wa Upako: Kuoa wake wengi sio dhambi, katazo ni propaganda

Mzee wa Upako: Kuoa wake wengi sio dhambi, katazo ni propaganda

Mbona kaongea hoja nzuri na nzito mnashindwa kumjibu mnamtukana ebu jibuni hoja hio vizur
Mnapinga wake wengi afu mnaongoza kwa michepuko
Ukiona mtu anashindwa kujibu hoja, ujue somo kalielewa bali ubishi tu unamsumbua. Somo alilotoa mzee wa upako limeeleweka kwa wakristo wengi.

Na kama halijaeleweka, Basi na anayebisha na kamaameoa atupe jiwe la kwanza kama hana kimada huko nje. Na kwanini iwe ruksa kuwa na kimada nje eti ukajidanganya, si bora uowe tu ili hata watoto wako wote wapate haki ya kama elimu, malazi, matibabu hata kurithi mali zako pale Mwemyeezi mungu atapokuchukua.
 
Daah Huwa hasomi Biblia anafikiria tu biashara yake ya maji na udongo
 
Inashangaza badala ya wachangiaji kujikita kwenye hoja,wanamjadili Lusekelo.
Mwenyewe anawajua sana hawa watani zake- akasema kesho watanitupia mawe, ndio haya wanayotupa. Kwasababu alijua kuwa hawana hoja hao. Na hawawezi kupata popote penye kusimamia hoja zao.

Watatukana sana bila hoja. Mzee wa upako kashamaliza tena.
 
c55bace8-94e2-46a2-ae29-0040cb7028fe.jpg

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC) nchini Tanzania, Anthony Lusekelo 'Mzee wa Upako' amesema suala la kuoa wake wengi linatafsiriwa kama ni dhambi hivi sasa wakati hapo zamani na katika ushahidi wa vitabu vitakatifu haikuwa ni dhambi.

Mchungaji Lusekelo ameeleza hayo Julai 11, 2024 wakati akihojiwa na kituo cha redio cha Wasafi FM ambapo amehoji kama agizo la Mungu ni kuja duniani na kuongezeka ni kwa vipi tutaongezeka bila wake wengi. "Mimi kule kwetu ni Chifu hivyo nilitakiwa niwe na wake sita, si kwa maana ya uzinzi, hapana.

Mungu amesema mkazae ili muongezeke mkajaze nchi, haiwezekani wakati wa Abraham (kuwa na wake wengi) haikuwa ni dhambi halafu leo iwe ni dhambai, Yesu mwenyewe ambaye ni mwokozi wa dunia ni mtoto wa mama mdogo, Daud alioa mke mdogo, mke wa Uria ndio ikaenda akamzaa Selemani na Yesu huko huko." alisema Mchungaji Lusekelo na kuongeza " Inakuwaje leo kuwa na wake wengi inakuwa ni dhambi?

Wakiristo leo wako tayari wanaume kwa wanaume waoane kanisani lakini si ndoa mbili. Ulaya wa Ulaya wanaume kwa wanaume wanaoana, wasagaji wanabarikiwa lakini si suala la kuoa mke wa pili, kuna kitu gani hapa wazungu wanatufunga? "
 
Tulitegemea atupe majibu mujarabu ya kimaandiko, mbona katuuliza maswali tena?

Polygamy ilikuwa dhambi zamani kama ilivyo dhambi sasa - hilo halijawahigi kubadilika.

The fact that it was a prevalent practice which was almost wholly acceptable even by those who were highly regarded by God, doesn't make it any less sinful.
 
Wewe mbona hujatoa hayo maandiko?
 
MTU aliyekengeuka ni hatari Sana kuliko asiyeamini kabisa

Tangu kuumbwa kwa ulimwengu na mwanzo wa ndoa ya kwanza
Ndoa ni watu wawili tu tena mume na mke na si vinginevyo
Ndo maana Yesu alikuja kukamilisha yaliyokuwa yamepungua katika torati ya Musa
Na Musa alitabiri juu ya Yesu alisema Mungu atawainulia nabii Mwingine msikilizeni

5 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.
Marko 10:5

6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.
Marko 10:6

7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
Marko 10:7

8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
Marko 10:8
 
Ukengengeufu ni hatari Sana Kwa kanisa
Maana MTU anatumia biblia ile ile lakini anatoa tafsiri yake anayotaka kwa hila
 
Kitu kinachotutafuna kwa sasa ni kuingia kwenye mtego wa ndoa ya mke mmoja.

Hata tamaduni zetu zenyewe zilidharau mwanaume mwenye mke Mmoja.

Zaidi Hakuna mahali biblia imesema tuoe mke mmoja au tuwe na mke mmoja.

Tuendelee kufungwa na sheria za kanisa ambazo tuliamini hazibadiliki ila kwa sasa zinaendelea kubadilika.
Kumbe ndoa ya mke mmoja ni mtego[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] mliooa mke mmoja toeni mawazo yenu
 
MTU aliyekengeuka ni hatari Sana kuliko asiyeamini kabisa

Tangu kuumbwa kwa ulimwengu na mwanzo wa ndoa ya kwanza
Ndoa ni watu wawili tu tena mume na mke na si vinginevyo
Ndo maana Yesu alikuja kukamilisha yaliyokuwa yamepungua katika torati ya Musa
Na Musa alitabiri juu ya Yesu alisema Mungu atawainulia nabii Mwingine msikilizeni

5 Yesu akawaambia, Kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu aliwaandikia amri hii.
Marko 10:5

6 Lakini tangu mwanzo wa kuumbwa ulimwengu, aliwafanya mume na mke.
Marko 10:6

7 Kwa sababu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe;
Marko 10:7

8 na hao wawili watakuwa mwili mmoja; hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja.
Marko 10:8
Pia aliwahi kusema Yes sio Mungu...unasemaje kuhusu Hilo?
 
Kama mimi ningekuwa Mkristo basi ningem challenge hivi huyo Pastor.

Kama lengo la Mungu ni kuzaa ili kuijaza dunia, kwanini option ya kuwa na mwenza zaidi ya mmoja iwe fixed upande mmoja?

Kwanini iwe wanaume tu peke yao ndio wenye hiyo access ya kuwa na wanawake wengi?

Kwanini na wanawake nao wasipate hiyo option ya kuwa na wanaume wengi ili kuharakisha zoezi zima la kuijaza dunia lifanyike kwa haraka?
Mwanaueme kapewa mamlaka ya kumiliki.l tofauti na mwanamke
 
Back
Top Bottom