Mzee wa Upako: Kuoa wake wengi sio dhambi, katazo ni propaganda

Mzee wa Upako: Kuoa wake wengi sio dhambi, katazo ni propaganda

Hivi kuna mkristo mwenye akili kama mm anaweza kumsikiliza huyu mlevi

USSR
Yuko sahihi sana, kuoa wake wengi haijawahi kuwa dhambi kokote kule, zaidi ilikuwa ni ushauri tu wa mtume mmoja.
 
Kama mimi ningekuwa Mkristo basi ningem challenge hivi huyo Pastor.

Kama lengo la Mungu ni kuzaa ili kuijaza dunia, kwanini option ya kuwa na mwenza zaidi ya mmoja iwe fixed upande mmoja...
Mwanamke hana uwezo wa kubeba mimba za wanaume wawili kwa wakati mmoja lakini mwanaume anauwezo wa kubebesha mimba wanawake hata mia kwa wakati mmoja.
 
Yeye kama anataka kuoa wake wengi aoe tu! Lakini ndoa ni ya Mme mmoja na Mke Mmoja kama ilivyokuwa mwanzo,kama Yesu Kristo anavyosema,
Mathayo19:4-7
Mwanzo2:21-24
Kila mtu awe na Mke wake Mwenyewe na kila Mwanamke awe na Mme wake Mwenyewe,
(1Wakorintho7:1-4)
Kwa hiyo Mfalme Suleiman alifanya dhambi?
 
Kama mimi ningekuwa Mkristo basi ningem challenge hivi huyo Pastor.

Kama lengo la Mungu ni kuzaa ili kuijaza dunia, kwanini option ya kuwa na mwenza zaidi ya mmoja iwe fixed upande mmoja?

Kwanini iwe wanaume tu peke yao ndio wenye hiyo access ya kuwa na wanawake wengi?

Kwanini na wanawake nao wasipate hiyo option ya kuwa na wanaume wengi ili kuharakisha zoezi zima la kuijaza dunia lifanyike kwa haraka?
Hebu rudia kusoma ulichoandika alafu jitathmini, Kwa msaada ni kwamba Mwanamme anaweza wapa mimba wanawake wengi kadri ya uwezo wake, lakini kila mimba Kwa mwanamke itajazwa na mwanamme mmoja tu hapo Tena mpaka baada ya miezi Tisa ajifungue ndipo ataweza kupewa na mwanamme mwingine.
 
Yesu unaye muiga alikuwa na mke huyo mmoja au alizaa watoto wangap ww unamfuata mtu ambaye hata hakuwa na mke wala mtoto kweli utapeli mwingi
Nani amekwambia Yesu akuacha watoto, tatizo mnasoma Biblia peke yake ilhali imefanyiwa mchujo wa kutosha. Soma na vitabu vingine vilivyoandikwa na wale ambao hawakuwa wafuasi wa Yesu.
 
View attachment 3040240
View attachment 3040244
Amesema katazo la kuoa wake wengi ni propaganda za wazungu ambapo wao wapo tayari wanaume waoane lakini sisi kuoa wake wengi waone kosa.
Ameongeza siku ya mwisho mwanaume mmoja atakuwa na wake saba
Nadhani Yesu alipokuja ndo alinyoosha

Ukiruhisu kuoa wanawake wengi je utaweka limit???

Yesu kwa kuliona Hilo litaleta shida na wanadamu wata:-abuse hii opportunity kwa kuoa wake wengi bila idadi maalum, akashauri mke mmoja

Pili ili kuishi ndani ya upende wa kweli bila unafiki na matanio ya mwili ndani ya ndoa Yesu alishauri mke mmoja

Mchungaji kama ana ushauri jinsi ya accommodate hayo aliyoyaona bwana Yesu yatatusumbua atuambie
 
Usimshambulie mtoa hoja

Kwanini Ibrahim haikua dhambi?
Katika kileo Kuna ukweli siyo unafiki.

In vino veritas is a Latin phrase that means 'in wine, there is truth', suggesting a person under the influence of alcohol is more likely to speak their hidden thoughts and desires.
njoo na reference
katoa reference kwa Ibrahim
ukimpinga njooo na reference
Mimi naanza kumuamini, huyu ndiyo mtume wa kizazi kipya
Kipindi cha agano la kale kabla Yesu kuja duniani, kulikua na sheria nyingi kama talaka, ndoa za mitala, ndugu kwa ndugu kushiriki ngono

Yesu alipokuja aliweka kila kitu sawa kwa mafundisho mapya ambayo yanaitwa Agano jipya.

Mkasome Mathayo 19:3-6
 
Binafsi huyu alikuwa ni mmoja wa wahubiri wangu PENDWA, nilikuwa namuelewa sana katika mafundisho yake.

Lkn lilipokuja suala la NAFSI 3 ZA MUNGU hapa nikaanza kumuogopa na kujiuliza mara miamia hivi ni huyu kweli au copy yake!! Aliniacha njia panda nikifikiria zaidi.

Kaingiza suala jingine sasa la NDOA ya wake wengi !! Bado najifikirisha snaa, ila naamini na nakubali anao UWEZO mkubwa sana juu ya maandiko !!

Huyu ni kati ya WAHUBIRI waliosoma biblia kwa muundo ya IMANI KATOLIKI licha ya yy mwenyewe kutolitamka hilo lkn upeo wake UNATHIBITISHA hivyo.

Muumini wa kawaida kumlisha maandiko mengine mwisho ni kumpoteza kabisa na hili ndo msimamo wa Kanisa Katoliki
Mfano KAZUNGUMZIA ADAM mke wake wa kwanza ni LILIS na siyo HAWA.
 
Kwa hiyo Mfalme Suleiman alifanya dhambi?
Kabisa....na ndio ilikuwa sababu ya anguko lake.

Alioa wake wengi kutoka kwenye mataifa ambayo Mungu aliwakataza Waisrael wasio huko na wasioze binti zao huko.

Soma kwa Utulivu...

1 Wafalme 11
1 Mfalme Sulemani akawapenda wanawake wengi wageni, pamoja na binti yake Farao, wanawake wa Wamoabi, na wa Waamoni, na wa Waedomi, na wa Wasidoni, na wa Wahiti,

2 na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa Israeli, Msiingie kwao, wala wasiingie kwenu; kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu yao. Sulemani akaambatana nao kwa kuwapenda.

3 Akawa na wake mia saba binti za kifalme, na masuria mia tatu; nao wakeze wakamgeuza moyo.

4 Maana ikawa, Sulemani alipokuwa mzee, wake zake wakamgeuza moyo wake, afuate miungu mingine, wala moyo wake haukuwa mkamilifu kwa Bwana, Mungu wake, kama moyo wa Daudi baba yake.

5 Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi, mungu mke wa Wasidoni na Milkomu, chukizo la Waamoni.

6 Sulemani akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfuata Bwana kwa utimilifu, kama Daudi baba yake.

7 Sulemani akamjengea Kemoshi, chukizo la Wamoabi, mahali pa juu, katika mlima uliokabili Yerusalemu, na Moleki, chukizo la wana wa Amoni.

8 Na kadhalika ndivyo alivyowafanyia wake zake wa nchi za kigeni, waliofukiza uvumba, wakawatolea miungu yao dhabihu.

9 Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea mara mbili,

10 akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu mingine; lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.

11 Kwa hiyo Bwana akamwambia Sulemani, Kwa kuwa umefanya hayo, wala hukuyashika maagano yangu, na sheria zangu nilizokuamuru, hakika nitaurarua ufalme usiwe wako, nami nitampa mtumishi wako.
 
Na Yesu akamuoa nani?, au aliwaambia tuu muoe ila yeye hakuoa?
Hakuja duniani kuoa! Alikuja kwa kazi moja ya kuuokoa ulimwengu na dhambi! Harafu asili yake ni mbinguni,mbinguni hawaoi wala kuolewa,
Luka20:34-36
 
Sahihi kabisa, Mimi na huyu mzee tunaenda Sambamba sana katika kuyatafsiri maandiko, kuna watu wamemix tamaduni za Kirumi/kizungu na wajaziita Ukristo ila Mungu hajaagiza hayo.

Kuoa wake wengi haijawahi kua dhambi na haitokua dhambi kamwe.
 
Back
Top Bottom