Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Jana nilikutana na class mate wa utotoni. Tuliachana tukiwa shule ya msingi, mzee wao alistaafu walirudi kwao huko mikoa ya Bara.
Huyu rafiki alikuwa mmoja wa vipanga darasani na aliitendea haki akili yake. Ana nafasi nzuri sana huko aliko. Katika maisha yake binti aliyemuoa alitoka famila ya matawi ya juu.
Jana alikuwa ananieleza magumu wanayopitia kwenye ndoa yao. Ana kumbuka siku ya harusi yao, familia yake ilitoka Bara huko na wakati wa kutoa zawadiilikuwa tofauti na upande wa mke waliowazawadia vitu vya thamani kama gari , kiwanja, ticket za honeymoon. Mzee wake alifunga Bible kwa unadhifu na alimkabidhi meza kuu.
Ananiambia kipindi hiki anatambua kuwa zawadi ya muhimu kuliko zote. Mali zilileta mzozo wala ha itamani. Tegemeo la furaha yake liko kwenye Bibilia ambayo mzee wake Alimhusia asimalize siku bila kuisoma.