Mzee wangu anakaribia kustaafu, uwekezaji upi ni mzuri?

Mzee wangu anakaribia kustaafu, uwekezaji upi ni mzuri?

Jielimishe kuhusu UTT ni nini na mmiliki ni nani. Pia utuambie ni biashara gani ambayo itabaki salama baada ya huo mtikisiko wa kidunia ili watu wawekeze kwenye hyo biashara.
Naona umekuja tetea.

Makampuni makubwa kama Evergrande zinafirisika sembuse UTT ya wabongo?
 
Achana na UTT, achana na Fixed account, awekeze hela zake kwenye Bond atulie. Atapata hela kila baada ya miezi 6 lakini ni uhakika. Faida ni 10 to 12% kabla ya kodi
Bond za BOT ni bora maana uhakika wa kulipwa upo
 
Kama ana mzigo mzuri na wakutosha atafute nyumba ya vyumba kadhaa uswazi kisha afungue guest ..ataokota maokoto kila siku ..short time..full time..vinywaji
 
Matajiri (hata waliozeeka) wanakwenda benki kuomba mikopo ili wafanye mambo.
Maskini anaamua kuweka pesa benki.

Baba yangu alistaafu 1983. Bado yuko hai.
Alipewa kiinua mgongo sh.30,000/=(elfu thelathini).
Aliamua kupanda kahawa na miti. Ndiyo inayotuunga mkono kumtunza.

Angeiweka benki angekuwa ana nini, ukizingatia makato yao yasiyo na huruma, mfumuko wa bei, kushuka kwa thamani ya pesa nk.
Mwaka jana, Desemba; sukari ilikuwa 3,000/=. Leo ikoje?

Muwe makini sana.
Maana yake ana miaka 100?
 
Atafute mil 10 atie mkeka wa odds 2. Uhakika wa mil 20 upo hapo. Ina maana anapata faida ya mil 10. Sasa hiy mil 10 aizungushe kwa mikeka ya mil 2, 2 sure odds 2 au 1.5 kila mwezi anabet mara moja tuu....

Au mnasemaje ndugu zangu..
Ohooooo..... Hiyo kubet ni kama Mzee mmoja Afisa elimu alipata fedha akaenda kugombea ubunge watu Wana yeye tupo pamojaaa tupo pamojaaa.... Kilichomkuta.... Mungu anajua
 
Ushauri wa Bond za benki kuu au unit za utt kwa mzee mstaafu kama huyo ndugu yako ni bora kabisa.

Mambo ya kujenga, kulima, kufanya biashara, nk sio risk ya yeye kuichukua kwa umri wake. Pressure zaweza kumdhuru akaaga wakati si wake.

Usiogopeshwe na wanaodai fedha zaweza kukwapuliwa, au wanaosema faida ni kidogo. Bond na mifuko aina ya utt ni uwekezaji wa uhakika duniani pote.

Nchi yetu ilipitia wakati wa pesa za mifuko kama NSSF kukopwa/ kuchukuliwa na serikali, lakini Utt iliheshimiwa kabisa. Najua kwa sababu nina unit za utt toka inaanza.
 
Kama katika maisha yake ya kazi hakuwekeza na anataka kuwekeza kutumia kiinua mgongo mwambie tu hawezi maliza miaka 5 zaidi anakuwa ameshapendwa zaidi
 
Hicho unachokitaka ukiwa na mkwanja mrefu ndio inanoga, sio milioni ngapi ngapi, anzia milioni mia kadhaa huko, unaweka bond BoT pale unakaa miguu juu. Huku kwingine kutafuta presha tu.
 
Kama katika maisha yake ya kazi hakuwekeza na anataka kuwekeza kutumia kiinua mgongo mwambie tu hawezi maliza miaka 5 zaidi anakuwa ameshapendwa zaidi
Mkuu

Wewe unayemtaka hiyo 30m yake asiiwekeze, kwa vile eti amechelewa, ndio humtakii mema.

Mleta mada kaomba ashauriwe mahali salama pa kuweka hiyo pesa ili iliwe polepole. Wewe unamtabiria kifo katika miaka mitano! Si sawa.
 
Mkuu siyo kila mtu anaweza kuwekeza mapema. Kuna sababu nyingi zinazofanya mtu asiweze.
Uko sahihi,watumishi wengi wanapokuwa kwenye ajira wanabanwa sana na madeni,hii kitu inawafanya mpk wanastaafu ndio deni linaisha,kwahiyo muda wote huo anaishi na mshahara mdogo sana wa kukidhi mahitaji yake ya kila siku,kwahiyo anapostaafu ile hela ya kustaafia ndio anaipangia mikakati ya kuwekeza,hili ni kwa wengi...
 
Pesa za mzee alizopigania kwa jasho na damu kwa miaka 20+ wewe huna mamlaka ya kumpangia mtu. Tafuta zako ndugu uziweke Utitiii
 
Ukishaona kitu kinapigiwa sana chapuo jua kuna watu watalia
Ubaya watu hawaambiwi wasome vigezo na taratibu hadi mwisho kabisa ambapo pameandikwa vizuri
Msimu huu naona inapigiwa debe sana ...Ngoja tuone huko mbele...
 
Haya naona jibu unalo ila unataka tick tu
Kwa kuweka akiba ni kwa vijana ila sisi wazee tunataka tuwe active uzeeni na sio kula kulala hebu msitujaza haya mambo
Yaani miaka yote nimefanya kazi na nimeweka malimbikizo ya kustaafu na kusubiri kiinua mgongo halafu nikazilaze tena bank hell NO
Boro niwe na shamba la kisasa na kufuga mifugo isiyozidi 50 tena wa Breed nzuri halafu nakula kuku na mboga fresh kila leo
Afya ndio kila kitu
Mzee akae anasubiri laki 5 kila mwezi ale alale mpaka kisukari na pressure hapana
Usimfanye hivyo
Ajenge nyumba nzuri kwenye shamba la ekari 15 na aweke fence na mifugo na bustani ale Bata tu
Wajukuu wakija wafurahi na babu yao
 
Mkuu hili wazo pia zuri. Ngoja nitafakari pia. Lakini huoni kuwa ufugaji pia una changamoto zake za kutosha? Vipi changamoto za usimamizi wa hiyo mifugo? Malisho ya mifugo usimamizi ukoje ukizingatia hulka ya vijana wa leo katika utendaji kazi wao? Vipi mlipuko wa magonjwa kwa mifugo ikianza?.Mkuu huoni anaweza kupata presha za ajabu ajabu?
 
Salamu ziwafikie wana Jf wenzangu.
Ninaomba msaada katika uwekezaji wa fedha benki.

Ni hivi mimi nina mzee wangu anayetarajia kustaafu mwaka huu. Sasa kama kijana wake wa pekee na anayeniamini ameniomba nimsaidie namna ya kuwekeza fedha zake kwa ajili ya kufurahia uzee wake.

Sasa mimi cha kwanza kabla ya mengine ninachotamani ni kwamba mzee awekeze fedha zake benki ili ikiwezekana kila mwisho wa mwezi awe kama anapokea mshahara wa kati ya 500,000-700,000 za kitanzania huku ile hela yake aliyohifadhi ikibaki kuwa dhamana yake katika uwekezaji na akiitaka aichukue muda wowote ule.

Nimefatalia kwa umakini sana humu JF uwekezaji wa namna hii mfano, hisa, UTT, fixed account n.k. lakini bado sijapata kile ninachokifikiria kuwa afungue tu akaunti awekeze hela huko kisha kila mwezi awe anavuna kiasi tajwa hapo juu. Sasa maswali yangu ni haya hapa chini.

i. Je Kuna uwezekano wa kupata akaunti ya kuwekeza labda tuseme milioni 20 au 30 za kitanzania na mtu akapata mavuno ya laki 5 Kila mwezi?

ii. Kama ni ndio je ni kiasi gani kinaweza kuleta mavuno ya laki 5 kama jibu ni sio je ni akaunti gani naweza kuwekeza angalau kupata kiasi kizuri kwa mzee kwa kila mwezi?

iii. Je ni benki gani nzuri itafaa Kwa uwekezaji huo kwa ajili ya mzee?

N.B: Kumbuka sitamani uwekezaji mwingine zaidi ya huo hapo juu. naomba ushauri ujikite katika muongozo huo. Natanguliza shukrani zangu.

Soma Ushauri kwa wastaafu na wanaopata hela nyingi kwa mkupuo
Nasikitika Sana sijui kwann wabongo wengi hatuna elimu sahihi ya biashara... Sema kwakua Mzee anakaribia kustafu na sijui kama ana uzoefu na biashara yyt?
 
Back
Top Bottom