Mzee wangu anakaribia kustaafu, uwekezaji upi ni mzuri?

Kwa kweli upande wangu nimefanya utafiti sana kuhusu mifugo
Kwanza hao mifugo lazima wawe wamewekewa uzio na wanakula humo humo ila sio zero grazing bali wanakuwa wanatoka na kuzunguka humo humo

Kila kitu kina changamoto zake nafikiri mimi naweza kuwa na umri sawa na mshua ila plan yangu ndio hii
Kupata wafanyakazi wanaolala hapo hapo wapo na madokta wa mifugo wapo wengi ambao naweza kuwalipa kwa mwezi na wakawa wanakuja kuangalia mifugo kila wakati
Kuhusu kufa na maradhi kwa mifugo kama mbuzi ni ngumu hata kuku pia maana ukiwaangalia kwa umakini na kuzuia watu kuingia wakiwa wametoka kwenye mifugo mingine hilo ni hatari sana

Kwa kudhibiti hilo kuna wellington boots 👢 unaweka pa kuingilia na wanavaa hivyo
Labda kwq kuwa unawasi wasi tu na ni kawaida kwa binadamu kuwa na shaka ila kumbuka kuna wafugaji wengi sana ambao ni wastaafu

Jaribu kuangalia YouTube utaona tena wazee wa kiswahili wengi tu na hata wengine walioacha kabla ya uzee na kuamua kujikita kwenye ufugaji

Kama una ekari 50 au Mia hapo utalima mazao ya chakula na majani ya mifugo pia
Sio kazi ngumu kama unavyoiona na kila kitu kinakuwa kigumu kama huna hela mkuu

Ila lilikuwa ni wazo tu usilifikirie sana
 
Nimekuelewa sana mkuu. Ngoja nimshirikishe mzee nione kama kuna kitu atasema. Japo mimi nimeliona ni wazo zuri ukizingatia kuwa mshua mambo ya kilimo anayawezea sana na amekuwa akifanya muda mrefu. Kwa wazo hili naona mzee akipata eneo akatulia mwenyewe akawa analima huku anafuga anaweza kufanya jambo zuri na kubwa sana. Mkuu nashukuru sana Kwa kuniondoa wasiwasi nadhani nitakupa mrejesho.
 
Mkuu

Wewe unayemtaka hiyo 30m yake asiiwekeze, kwa vile eti amechelewa, ndio humtakii mema.

Mleta mada kaomba ashauriwe mahali salama pa kuweka hiyo pesa ili iliwe polepole. Wewe unamtabiria kifo katika miaka mitano! Si sawa.
Nashukuru sana mkuu Kwa kuelewa lengo langu kuu. Hoja ni kuwa aweke fedha hizo wapi ili awe anakula pole pole na sio kuwekeza. Nadhani wajumbe wengi wameshindwa kuelewa kusudi kuu la andiko langu
 
Wala usihofu kwani maisha ni mafupi na kama unapumua mshukuru sana Mola na pia tuangalie afya zetu
Ila kwa ushauri kama unataka afanye kitu afanye biashara au kitu anachokuona kwa karibu
Vitu kama usafiri ni changamoto kubwa sana na hiyo ndio imaleta maradhi ya kila aina
Kwa mfano Bus au lorry, boda nk hata mashine za aina zote ni mtihani kwa wazee
Lakini mifugo, niamini wazee tunapenda utulivu kuona nyanya zinakuwa na mayai kila siku
 
Pesa za mzee alizopigania kwa jasho na damu kwa miaka 20+ wewe huna mamlaka ya kumpangia mtu. Tafuta zako ndugu uziweke Utitiii
Mkuu samahani sana kama nitakosea kukuuliza swali. Naamini wewe una wazazi. Vipi wazee wako wakikuomba ushauri? Utawashauri au utakataa kuwashauri kwa kuwa wewe hauna mamlaka ya kuwapangia? Ni nini mchango wako Kwa wazee wako? Je ni kuwapa pesa tu?
 
Hicho unachokitaka ukiwa na mkwanja mrefu ndio inanoga, sio milioni ngapi ngapi, anzia milioni mia kadhaa huko, unaweka bond BoT pale unakaa miguu juu. Huku kwingine kutafuta presha tu.
Nimekupata mkuu. Shukrani Kwa maoni mazuri
 
Habari mkuu naona umeiongelea utt kama unashaka nao naomba na mimi unisanue mapema
Haipo kama walivyoandika humu. Mkuu. Zipo namba unaweza piga moja kwa moja ukapata maelezo. Mimi ni muwekezaji huko ila sio kama alivyoshauriwa na huyo bwana. Huyo bwana hajui kitu
 
Mkuu samahani sana kama nitakosea kukuuliza swali. Naamini wewe una wazazi. Vipi wazee wako wakikuomba ushauri? Utawashauri au utakataa kuwashauri kwa kuwa wewe hauna mamlaka ya kuwapangia? Ni nini mchango wako Kwa wazee wako? Je ni kuwapa pesa tu?
Nilikuwa nao bahati mbaya wametangulia mbele za haki. Hawakuwa na ajira rasmi.
 
Nakubaliana pia na mawazo yako, kwamba asianze kitu kipya kwa sasa..Muhimu usimamizi mzuri tu wa hizo fedha.
 
Ajenge lodge au guest house ale pesa zake ..
 
Uzoefu unaonyesha, karibu 80% ya wastaafu walioamua kuwekeza pensheni zao kwenye aina yoyote ya biashara au shughuli ya kuzalisha mali mpya, ndani ya miaka mitano walifirisika, walirudi kwenye zero level.

Ukiondoa UTT na bond za serikali kwingine kote ni chenga tupu.
 
UTT hii mbeleni naona kuna watu watatoa machozi

Sababu hisa zinaweza shuka...vilevile ongezeko na migogoro duniani na hizi pandemic desease
Kunaweza kuleta mtikisiko wa uchumi kidunia
Kumjua mchawi sio kazi ngumu
 
Biashara au uwekezaji unategemea mazingira, uzoefu, passion ya mtu, uwezo binafsi, interests na kadhalika na kadhalika,

Kutaka ushauriwe kitu cha kufanya ni mambo ya ajabu!
 
Biashara au uwekezaji unategemea mazingira, uzoefu, passion ya mtu, uwezo binafsi, interests na kadhalika na kadhalika,

Kutaka ushauriwe kitu cha kufanya ni mambo ya ajabu!
Wala sio ajabu labda wewe haujawahi kufanya biashara yeyote ndio maana unashangaa hilo
 
Kuna hotuba aliekuwa mkuu wa mkoa wa Dodoma Mh Mtaka alitowa kwa wastaafu wa serikali. Nadhani iko youtube. Alitoa maneno mazuri sana kuwashauri wastaafu kuhusu pesa zao baada ya kustaafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…