Mzee wangu anakaribia kustaafu, uwekezaji upi ni mzuri?

Mzee wangu anakaribia kustaafu, uwekezaji upi ni mzuri?

Sasa hapa ndio inakuja tofauti ya wala vumbi na wabeba mabox, mbeba mabox akistaafu akiamua kuja kujikalia bongo tu bila uwekezaji wowote pesa ya chini sana kuvuta kila mwezi ni 3m. zinaingia zinatulia kwa account. Akiwa na apartments zake kapangisha uhakika wa 10m kwa mwezi rahisi. 😂 😂 😂
 
Kosa limeshafanyika tayari. Uwekezaji huwa unafanywa mtu akiwa kazini, akiwa na nguvu na kujifunza, baada ya kustaafu ni ufatiliaji mdogo tu sana sana na kuongeza mtaji. Unaposema mzee wako awekeze saa hizi ni uongo.

Shida ya wastaafu wengi huwa wanataka akipata kiinua mgongo ndo awekeze, this is not right. Na bahati mbaya wanaowadanganya wastaafu wengi ni watoto wao, au ndugu na kimsingi ndio wanaotaka kutoka kwa kupitia hicho kiinua mgongo.

We jamaa uliyeandika hapa, tafuta kazi ya kufanya achana na hela za huyo mzee. Huyo mzee anahitaji counseling tu ili hizo hela zake azile Pole Pole hadi atakapokufa. Mwacheni huyo mzee na hela zake tafuteni zenu. Mtu kapambana kajifanyia kazi zake miaka 30+ anastaafu mnaibuka mnataka kuanza kumshauri namna ya kuishi na namna ya kutumia hela zake.

Hela ya kustaafu ni hela ya kujikimu sio ya uwekezaji. Inaaminika mtu anapostaafu ameshamaliza kusomesha, ameshamaliza kujenga pa kuishi so hela yake ni ya kula tu.
 
UTT hii mbeleni naona kuna watu watatoa machozi

Sababu hisa zinaweza shuka...vilevile ongezeko na migogoro duniani na hizi pandemic desease
Kunaweza kuleta mtikisiko wa uchumi kidunia
Jielimishe kuhusu UTT ni nini na mmiliki ni nani. Pia utuambie ni biashara gani ambayo itabaki salama baada ya huo mtikisiko wa kidunia ili watu wawekeze kwenye hyo biashara.
 
Utt uwekezaji wa muda mrefu let say 10+ anaweza kuwa anaingiza 10% ya akichowekeza kwa nwaka. Sasa kwa hiyo 30M kwa mwaka anaweza kuwa anapata gawio la 3M ambayo kila mwezi atakuwa anaingiza 250,000. So ukitaka aingize let say 500,000 lazima aongeze mpunga ufike 60M

Sent from my SM-A025U using JamiiForums mobile app
Asante sana mkuu nimekupata vema kabisa. Nadhani nitaliangalia na kulichunguza vema kabisa.
 
Jielimishe kuhusu UTT ni nini na mmiliki ni nani. Pia utuambie ni biashara gani ambayo itabaki salama baada ya huo mtikisiko wa kidunia ili watu wawekeze kwenye hyo biashara.
HAya tuendelee hii comment siku utaitafuta
Km waanzilishi wa mifumo ya bank wenyewe waliwai kuliwa kichwa rothchild banks .sembuse Huu mfuko pili sera zetu sio rafiki rejea utawala wa awamu ya tano ...watu wengi waliyumba sababu serkali kuchota fedha rejea mr kuku
 
Mkuu nahisi Wala huyo mshua wako hajakuomba umfanyie namna ya kunufaika na hayo malipo ya uzeeeni. Bali wewe ndiyo unazipigia hesabu hizo Hela unufaike nazo au wewe ndiye huyo Mzee mwenyewe.

Kama unazipigia hesabu hizo Hela aibu na iwe kwako.
Hapana mkuu. Ni kweli mkuu
 
Acha kumtesa mzee, muacheni ale pesa yake hadi iishi halafu kaeni kikao muone namna ya kumsaidia mzee kifedha baada ya kumaliza mafao na hajafa. Kazi na uwezkezaji vinafanywa na vijana wenye nguvu.Isitoshe mtafutieni binti mdogo ili atangulie mapema kama Mrema.Mtakuja kunishukuru
 
Kuna watu wameongeza thamani ya mfumo kwa kuingiza pesa ndefu haswa bllion na kitu..

Hawa jamaa siku watatoa na thamani ya kipande itashuka kwa vile speculation upande wa kununua itakuwa chini....Sasa hapa wabongo watajua wamepigwa kumbe hawana uelewa wa soko la hisa ngoja tuone
Factor zipo nyingi sana sera za nchi pia sio rafiki mamlaka wanaweza kuingia na kuchota fedha then wakabadili sheria
 
HAya tuendelee hii comment siku utaitafuta
Km waanzilishi wa mifumo ya bank wenyewe waliwai kuliwa kichwa rothchild banks .sembuse Huu mfuko pili sera zetu sio rafiki rejea utawala wa awamu ya tano ...watu wengi waliyumba sababu serkali kuchota fedha rejea mr kuku
Unadhani wapi kuna usalama? Kama serikali ikiamua kukufikia huna uwezo wa kukimbia. Umesahau kipindi hicho pia cha awamu ya Tano account za watu zilikuwa zinazuiliwa ama kuchotwa pesa? Hivyo basi utawala ukiamua kufanya lolote huna utakacho zuia.
 
But kumbuka pesa zinazochotwa ni bulk km hizo Utt
Mtu mwenye vimillion 100 au hamsini serikali hawa muda nazo otherwise uwe money lounder au economy saboteger...
 
Back
Top Bottom