Poleni,
Kitu kimoja cha kutambua:
1: Ni vyema mhusika afikishwe hospitali aanzishiwe tiba na kuangalia maendeleo yake kwa ujumla.
2: Kutambua kwa nini ameamua kusitisha dawa ili aweze kusaidiwa kurejea kwenye tiba akiwa na uelewa mzuri.
3: Kwa presha ya kiasi hicho, hili ni tatizo la kudumu maisha yake yote. Ni vyema kutambua kuwa hamezi dawa kwa sababu alianza dawa za presha au dawa za presha zinaongeza tatizo. Bali, tatizo hili kwa kiasi hiki kwake litakuwa la kudumu maisha yake yote.
4: Madhara ya presha kiasi hiki kuendelea kuwa juu inaweza kusababisha:
A: Kupata kiharusi/stroke
B: Kuumiza viungo vya mwili kama: figo/kufaili, moyo/shambulio la moyo, ini/kufaili, macho/uoni hafifu.
5: Presha kusoma sawa wakati unatumia dawa, maana yake ni matokeo ya dawa husika kufanya kazi vyema. Ukiacha kutumia dawa presha itapanda tena.
6: Tiba ya presha iambatane na mabadiliko ya kupunguza visababishi kama: kupunguza matumizi ya chumvi, kupunguza matumizi ya pombe, kuacha kuvuta sigara, kupunguza matumizi ya wanga, kufanya mazoezi mepesi.