Mzee wangu kaacha dawa za presha presha yake Iko 200/93 pr 46

Mzee wangu kaacha dawa za presha presha yake Iko 200/93 pr 46

Presha is overrated kuna mtu Msanga Zalala ana dawa ya asili ya presha watu wanatumia na wanapona kabisa. Hizo dawa za kizungu zinaharibu figo
Mkuu msanga zalala ndio wapi huko na anapatikanaje
 
Presha is overrated kuna mtu Msanga Zalala ana dawa ya asili ya presha watu wanatumia na wanapona kabisa. Hizo dawa za kizungu zinaharibu figo
Anatibu presha na magonjwa Gani
 
Sasa Unataka Ushauri Gani?
Kwanza Kabisa Ulipaswa kuona Red flag hizo na kuzifanyia kazi ikiwemo Kuwa Mkali kwa Mzee wako Maana Anakoelekea Ni kupata Cerebral Vascular Accident (CVA) Au kama wengine wanavyoita Stroke..

So jitahidi Umshauri arudi Kutumia Dawa
Ni hatari sana..

Na Kumbuka Hypertension Is The SILENT KILLER
Mkuu anaweza Rudi tumia dawa zake bila kurudi kwa daktar ..maana anatumia vidonge 7 na presha walau huwa inakua 160 Sasa anaona kama vidonge vingi na presha haishuki
Alishafanyiwa operation ya kuzibua mshipa wa moyo miaka2 nyuma hapo jkci
Mkuu ushauri wako vip abadilishe daktar wakumuatend na je daktar Gani mzuri mwenye uzoefu mkubwa hapo jkci
 
Presha is overrated kuna mtu Msanga Zalala ana dawa ya asili ya presha watu wanatumia na wanapona kabisa. Hizo dawa za kizungu zinaharibu figo
Mkuu msaada wa mdau wa msanga zalala pls
 
Habar wakuu ushauri wenu tafadhali Mzee wangu amekalua akitumia dawa za presha kwa miaka9 Sasa .hivi karibuni kaacha kutumia dawa,inaweza kuwa ni mda miezi kadhaa tangu aache,Sasa hivi presha yake inasoma hivo mda wote 200-199/90-97 pr 50-45..nin chakufanya nikama Hana mpango wakurudia kuzitumia, nb naalisha fanyiwa uporesheni ya kuzibua mshipa wa moyo ulioziba imepita kama miaka miwili afanyiwe hiyo operation
Ushauri wenu wadau
Jiandae kumchangia figo moja kama ni baba yako kweli
 
1 yupo kwenye dawa za presha takribani miaka9 Sasa na mwaka juzi tu nkafanyiwa operation ya kuzibua mrija ktk moyo ulioziba..dawa ana mwezi kaacha Jana ndo kaanza Tena kunywa hizo dawa za presha
2.sababu yakuacha anadai amekunywa dawa amechoka maana anakunywa vidonge vingi ,anakunywa vidonge 7 Sasa anaona vingi sana na presha haishuki inachezea 170 akiwa kwenye dawa
2.anaclinic jkci miaka Sasa
4.vip unatushauri nin kuhusu kubadilisha daktar hapo jkci
5.je anatakiwa afanye uchunguzi wa Figo moyo,ini?
6. Alishawahi fanyiwa operation ya kuzibua mishipa kwenye moyo miaka 2 Sasa imepita
7. Unaweza tufahamisha daktar mzuri awe anamuatend,maana daktar huyu anaemuona hatuoni mabadiliko ktk presha ya Mzee kwa miaka sasa

1: Kwa presha hiyo inayotajwa labda kama inatokea mara chache na kushuka chini/kurudi sawa, ila si muda wote kuwa 170mmHg.

Kama kila siku iko hivyo, unahitajika kuwa na mawasiliano ya karibu na daktari ili kupata maelekezo au maelezo mahsusi ya mwelekeo wa tiba ya mzazi wako.

2: Pia, wingi wa dawa si kwa suala la presha tu. Kuna magonjwa mengine mwambata kama unavyosema alishawahi kupata shida ya moyo hivyo anaweza kuwa na dawa za:
1: Presha
2: Mafuta
3: Kulainisha damu
4: Kuweka mapigo ya moyo sawa.
5: Kuzuia shambulio la moyo
Nk.

3: Vipimo vya kuangalia maendeleo ya mgonjwa hutegemea na tatizo la msingi na matatizo mwambata. Mgonjwa huweza kufanyiwa vipimo mara mbili kwa mwaka kwa wale walio sawa na wanaendelea vyema na dawa zao. Lakini, kwa wale ambao hawako sawa na kuwa na mwendelezo ambao si mzuri wa dawa, huweza kufanyiwa vipimo mara nyingi zaidi.

Lengo la vipimo huwa ni:
1: Kuangalia madhara yaliyosababishwa na ugonjwa/baseline.

2: Kuangalia maendeleo baada ya kuanza kutumia dawa/kulinganisha na wakati anaanza dawa.

3: Kuangalia dawa zipi zaweza kumfaa mgonjwa yupi wakati wa tiba kulingana na hali yake.

4: Kunapokuwa na viashiria vya mabadiliko kwa mgonjwa/dalili tofauti na matarajio ya daktari.

Hivyo, inategemea na mwenendo wa kliniki yake.

NB: Wakati wa kliniki ya baba muombe uwe nae kwa daktari kabla ya kufanya maamzi yoyote juu ya aina ya daktari. Uliza masuala ya muhimu kuhusu mgonjwa wako ueleweshwe vyema:
1: Presha yake ilivyo.
2: Aina ya dawa anazotumia.
3: Maono ya daktari kuhusiana na mgonjwa na ugonjwa wake.
Nk.
 
Mkuu anaweza Rudi tumia dawa zake bila kurudi kwa daktar ..maana anatumia vidonge 7 na presha walau huwa inakua 160 Sasa anaona kama vidonge vingi na presha haishuki
Alishafanyiwa operation ya kuzibua mshipa wa moyo miaka2 nyuma hapo jkci
Mkuu ushauri wako vip abadilishe daktar wakumuatend na je daktar Gani mzuri mwenye uzoefu mkubwa hapo jkci
Arudi JKCI na awe Mkweli Aseme pia kwamba Aliacha Dawa wafanyr vipimo Upya ECHO,ECG na Vingine vingi wataamua Ni dawa Gani wampatia
 
Mkuu Mzee yupo ktk dawa kwa miaka9 Sasa na dawa kaacha kama mwezi mmoja mpaka kufika Jana ndo kaanza kuzinywa Tena anatumia vidonge 7 Sasa anaona vingi ndo sababu iliyosababisha aache na pia Kuna ndgu alimdanganya dawa yakienyeji
2.Anaclinic jkci
3.alishafanyiwa operation ya kuzibua mrija kwenye moyo hapo jkci kama miaka2 imepita
4.kunywa vidonge vingi takriban7 kwasiku napresha yake kuwa 160 haishuki kwa muda mrefu.ndo kumemchosha anadai mbona wangine wanakunywa 1 tu au 2 kwasiku napresha zao ziko normal
5 mkuu ushauri je abadilishe daktar wakumuatend? Je daktar Gani mzuri jkci mwenye uzoefu wa muda mrefu anaeweza akasaidia kumpa mabadiliko

Pole sana.

Miili yetu haifanani kwa asilimia 100 katika utendaji kazi na hata katika uchakataji dawa nk.

Pia mnaweza kuwa na ugonjwa mmoja wote lakini mkatumia dawa tofauti kwa sababu ya tofauti hizo ndogogo pamoja na hatua ya ugonjwa wenyewe.


Simshauri abadilishe daktari, aende kwa huyo huyo aliyekuwa anamhudumia ili ashauriane naye kuhusu dawa zake, kupunguza au kuacha.

Hao wanaomshauri aache dawa sijui kama watakuja kumsaidia siku akipata madhara makubwa ya hiyo presha ya juu. Ni muhimu akashauriana na daktari wake tu.

Kila la kheri.
 
Tiba NAMBA Moja water fasting. Then herbs na maelekezo mengine sahihi ndio tiba. Haanze na funga. Hapate MAELEZO zaidi.
 
Back
Top Bottom