1 yupo kwenye dawa za presha takribani miaka9 Sasa na mwaka juzi tu nkafanyiwa operation ya kuzibua mrija ktk moyo ulioziba..dawa ana mwezi kaacha Jana ndo kaanza Tena kunywa hizo dawa za presha
2.sababu yakuacha anadai amekunywa dawa amechoka maana anakunywa vidonge vingi ,anakunywa vidonge 7 Sasa anaona vingi sana na presha haishuki inachezea 170 akiwa kwenye dawa
2.anaclinic jkci miaka Sasa
4.vip unatushauri nin kuhusu kubadilisha daktar hapo jkci
5.je anatakiwa afanye uchunguzi wa Figo moyo,ini?
6. Alishawahi fanyiwa operation ya kuzibua mishipa kwenye moyo miaka 2 Sasa imepita
7. Unaweza tufahamisha daktar mzuri awe anamuatend,maana daktar huyu anaemuona hatuoni mabadiliko ktk presha ya Mzee kwa miaka sasa
1: Kwa presha hiyo inayotajwa labda kama inatokea mara chache na kushuka chini/kurudi sawa, ila si muda wote kuwa 170mmHg.
Kama kila siku iko hivyo, unahitajika kuwa na mawasiliano ya karibu na daktari ili kupata maelekezo au maelezo mahsusi ya mwelekeo wa tiba ya mzazi wako.
2: Pia, wingi wa dawa si kwa suala la presha tu. Kuna magonjwa mengine mwambata kama unavyosema alishawahi kupata shida ya moyo hivyo anaweza kuwa na dawa za:
1: Presha
2: Mafuta
3: Kulainisha damu
4: Kuweka mapigo ya moyo sawa.
5: Kuzuia shambulio la moyo
Nk.
3: Vipimo vya kuangalia maendeleo ya mgonjwa hutegemea na tatizo la msingi na matatizo mwambata. Mgonjwa huweza kufanyiwa vipimo mara mbili kwa mwaka kwa wale walio sawa na wanaendelea vyema na dawa zao. Lakini, kwa wale ambao hawako sawa na kuwa na mwendelezo ambao si mzuri wa dawa, huweza kufanyiwa vipimo mara nyingi zaidi.
Lengo la vipimo huwa ni:
1: Kuangalia madhara yaliyosababishwa na ugonjwa/baseline.
2: Kuangalia maendeleo baada ya kuanza kutumia dawa/kulinganisha na wakati anaanza dawa.
3: Kuangalia dawa zipi zaweza kumfaa mgonjwa yupi wakati wa tiba kulingana na hali yake.
4: Kunapokuwa na viashiria vya mabadiliko kwa mgonjwa/dalili tofauti na matarajio ya daktari.
Hivyo, inategemea na mwenendo wa kliniki yake.
NB: Wakati wa kliniki ya baba muombe uwe nae kwa daktari kabla ya kufanya maamzi yoyote juu ya aina ya daktari. Uliza masuala ya muhimu kuhusu mgonjwa wako ueleweshwe vyema:
1: Presha yake ilivyo.
2: Aina ya dawa anazotumia.
3: Maono ya daktari kuhusiana na mgonjwa na ugonjwa wake.
Nk.