Mzee wangu yupo hoi, huenda Serikali ingeweka wazi, Mzee wangu asingeshiriki kuzika rafiki yao aliyefariki kwa changamoto

Pole sana ndugu yangu.

Watanzania waliowengi hasa wasio na access ya vyombo vya habari vya kisasa kama hizi smartphone hawana taarifa juu ya hali halisi ya Korona nchini.

Serikali imewaacha wananchi kwenye mataa
Huo ni uuwaji wa kudhamiria. Sawa na unyang'anyi wa kutumia nguvu tu.
 
Mimi nawashauri wazee kijijini kwetu msiba wowote unatokea mjini, kama ajali haijahusika, wasihudhurie hata kama waliofariki ni watoto wao.Full Stop!
Mpige stop kwenye msiba wowote ule mikusanyiko ndio inasababisha maambukizi kwa kasi kwenye lile kundi liliotajwa (wazee na watu wenye kinga zilizoshuka chini) so asiende tu kwenye mikusanyiko period✋🏽
 
Ni kujiongeza tu rafiki, mtu akifa kwa tatizo la upumuaji basi nyie ndugu chukueni tahadhari. Pole sana mtoa mada
Hivi wewe umeshawahi kukaa kujijini,unawajua watu wa kijijini walivyo?Kipindi kile cha mlipuko wa kipindupindu ,serikali ilitumia nguvu kubwa sana kupiga marufuku nyingi ili kipindupindu kisisambae.Sasa leo umewapa uhuru wa kufanya mambo yao kwa uhuru kwa kuwapa tahadhari ya mdomo,unategemea watafuata unachokisema?
 
pole sana mkuu,
 

Wale wasio na access na taarifa sahihi nao unasema je?

Kwa vile wewe una taarifa sahihi nini kinakufanya udhani ni hivyo kwa kila mtu?

Au watanzania wote ni wewe tu mkuu?
 
Huko kwenu wazee ndio wanabeba jeneza kupeleka mazikoni, sio vijana! Hao wazee walikuwa wanapokezana jeneza linalowavujia maji vijana wa huko huwa wapi?
 
Jana hapa kijijin nilipo palikua na ufunguz wa bar moja
Njemba zimeminyana ndani
Bia wanakunya haziishi kumbe mijasho yao inajaa kwenye chupa
 

Hata wewe unaweza kuwa pimbi pia, Rais kasema tuchukue tahadhari we unatakaje tena?
Vipeperushi? Kwahiyo kama hakuna vipeperushi ndio huwezi kuchukua tahadhari? Pimbi wengi sana hata JF humu
 
Pole mkuu,ila serikali wafunge shule za msingi na sekondari,vyuo waache,watu tunakula kupitia vyuo wakifunga hali itakua mbaya kwa baadhi yetu
 
Mheshimiwa wetu Hana huruma Wala hataki ku sympathize na raia wake awe na huruma na aseme sasa kila corner ni mwendo wa barakoa, kila sehemu kunawa kuwe na marufuku na misongamano isiyo na lazima shule zifungwe hata mwezi hatari itapungua bila hvo Hali itakuwa mbaya. Raisi wetu asiwe na roho ngumu ka ya farao Hadi apate pigo ndo ashtuke
 
Utavaa barakoa ila wengine hawJikingi wanakuletea, mwaka jana kila mtu alikuwa makini corona tukaishinda saa mbili ila sasa watu wengi wagonjwa
 
Pole sana ndugu Mungu ni mwema atamponya....ila pia nna maswali mawili.

1. km ugonjwa wa corona unaambukizwa kwa njia ya hewa na mtu hapumui tena na kafungiwa kwenye jeneza kubeba jeneza kuna shida gani?

2. Mtu akifariki anaanza kukauka, damu inaganda..hayo majimaji yanatoka wapi, tena mpaka yatoke nje ya jeneza?

Otherwise tuchukue tahadhari...kuzilinda Afya zetu ni jukumu letu sio la serikali wala mtu wa pembeni, we need to be smart on this.
 
Huko kwenu wazee ndio wanabeba jeneza kupeleka mazikoni, sio vijana! Hao wazee walikuwa wanapokezana jeneza linalowavujia maji vijana wa huko huwa wapi?
Hiiiiii bagosha!



Watauliza hata rangi za vyupi za wabeba jeneza. Lengo likiwa lile lile kujaribu kuwapoteza wowote maboya.

Ama hakika iziraeli mtoa roho za watu yu mwema mno kuliko nyie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…