Mzee wangu yupo hoi, huenda Serikali ingeweka wazi, Mzee wangu asingeshiriki kuzika rafiki yao aliyefariki kwa changamoto

Mzee wangu yupo hoi, huenda Serikali ingeweka wazi, Mzee wangu asingeshiriki kuzika rafiki yao aliyefariki kwa changamoto

HII habari kama si'' kahawa ya asubuhi'' au'' hadithi za shigongo,'' inasikitisha sana!
Usiombe yakufike na wewe! Kumuona mpendwa ambaye ni nguzo kuu! Kiunganishi cha ukoo, akiumwa bila matumaini inaumiza sanasana ...moyo unauma , mwili unatetemeka
 
Naandika huku naumia sana.

Maisha ya mzee wangu yako hatarini sana anapumua kwa shida sana.

Chanzo cha kuumwa.
Kuna rafiki yao mzee mwenzao alifariki, wakaambiwa kuwa chanzo cha kifo cha huyo rafiki yao ni mapafu.
Kutoka hospital ya Bugando ndugu wa marehemu walipewa mwili kwenda kuzika kijijini geita bila tahadhari wakiamini kafa kwa ugonjwa wa kawaida.

Alipofikishwa huko kijijini, ndipo wazee wenzake wakawa wamejiandaa kumzika mwenzao kama ilivyo ada yao.
Jukumu la kubeba mwili kuzika, lilifanywa na wazee kama ishara ya heshima kwa mwenzao.
Miongoni mwa wazee hao! Na mzee wangu alishiriki.

Msiba ulikuwa na msongamano mkubwa kama ada na mila za vijijini.

Wazee hawa maskini ya Mungu pasipo kujua walibeba mwili bila tahadhari! Hadi atua ya mwisho ya kumzika mwenzao.

Baada ya hapo jioni mzee akanisimulia ilivyokuwa, akadai pia walibeba na jeneza liliwavujia majimaji.
Baada ya siku kadhaa wazee hawa wameanza kuumwa.
Watatu wana hali mbaya sana, na mzee wangu usiku wa kuamkia Leo kabanwa mbavu haswa! Ametumia dawa ya malimao, vitunguu, pilipili na tangawizi lakini hali si hali, kwanza kaanza kuchanganyiwa na haongei tena.
Yuko hospital kalazwa lakini hali ni mbaya sana.
Huenda serikali wangetangaza tahadhari hasa misibani haya yasingetokea.
Huenda serikali ingetangaza wazi misiba ya korona ingezikwa na vijana walivalia kinga.
Hapa najaribu kuwaza kama hali iko hivi, maambukizi yameathiri wangapi kwa uzembe wa serikali?

Hatuhitaji lockdown, lakini chamhimu tamko litoke lifike hata kijijini watu wapewe mbinu.

Imeniuma sana kwa uzembe huu mkubwa! Kama nitapoteza busara za mzee wangu, yamkini na mama yangu atakuwa kaambukizwa maana wanalala pamoja mda wote wa kuuguza.

Yamkini tungeweza kuwalinda wazee lakini watoto wa shule hawa wadogo bado ni Carrier wa kuleta homa hiyo nyumbani.
Serikali ingefunga shule hata kwa miezi miwili ingesaidia kupunguza kasi kama mwaka 2020 sambamba na kuchukua tahadhari.

Utafaa nini utajiri katikati ya misiba?

Serikali ingeweza hata kuja na mikakati, kama hawana pesa za chanjo, wangeipokea hata watu wakachomwa kwa hiari hata kwa malipo tungelipa.

Katiba imuondolee mamlaka mtu mmoja kutegemewa kutoa tamko ili kuliokoa taifa.

Inauma sana.
Serikali imeoza.

Halafu mnasubiri tamko la serikali mkuu?

Za kuambiwa changanya na zako.
 
Naandika huku naumia sana.

.

Baada ya hapo jioni mzee akanisimulia ilivyokuwa, akadai pia walibeba na jeneza liliwavujia majimaji.

.
Mkuu unapata faida gani kuu potosha umma na kutaka kuzua taharuki kwa umma? Mtu afie bugando harafu jeneza lake litoe majimaji? Huu ni utani wa ajabu sana

Sidhani kama kwa hospital kubwa kama bugando walishindwa kuchoma mwili wa marehemu dawa za kuzuia mwili kuharibika,tuacheni utani kwenye mambo muhimu

Mzee wangu alipofariki alikaa mochwari siku kumi na baadae tulimsafirisha kwa maziko kwa takribani siku mbili ya tatu tukazika lakini mwili wake haukuwa ukitoa majimaji,how comes mkuu?
 
Huu ndio ujinga umewajaa.

Unashindwa kuelewa Kuna Mambo yanahitaji National Intervention na sio Individual Intervention tu. Sijui Kama unaelewa?

Watoto wadogo wanaenda shule za kata wanakutana na walimu. Wakirudi majumbani wanawaambukiza Babu na Bibi zao! Sijui Kama unaona hapo. Hapa Ni suala la serikali kuweka intervention In National Level kuwalinda wazee wetu.
Kwa hiyo kama serikali ikikataa kutangaza ugonjwa kuwa upo ndio nsitumie akili zangu za kuzaliwa kuilinda nafsi yangu? Usiniite mjinga wakati nailinda nafsi yangu. Mkuu sina nguvu ya kuufungua mdomo serikali itoe tamko . Ujinga wa kuchukua tahadhali ya nafsi yangu ni bora kuliko kuifikiria National intervation. Bora ujinga wangu . Naupenda ujinga wangu kwenye kuchukua tahadhari binafsi juu ya afya yangu binafsi . Mkuu wewe mwerevu endelea kila mtu atumie nafsi yake kama alivyozaliwa nayo . Asante 🙏🏽
 
Mkuu unapata faida gani kuu potosha umma na kutaka kuzua taharuki kwa umma? Mtu afie bugando harafu jeneza lake litoe majimaji? Huu ni utani wa ajabu sana

Sidhani kama kwa hospital kubwa kama bugando walishindwa kuchoma mwili wa marehemu dawa za kuzuia mwili kuharibika,tuacheni utani kwenye mambo muhimu

Mzee wangu alipofariki alikaa mochwari siku kumi na baadae tulimsafirisha kwa maziko kwa takribani siku mbili ya tatu tukazika lakini mwili wake haukuwa ukitoa majimaji,how comes mkuu?
Ukiniuliza na mimi nitakuuliza kwanini wameweza kunyamaza! Usiwe na kiburi cha uzima itakusaidia nini? Tunaouguza ndiyo tunaoumia!
Waliobeba jeneza wanasema walivujiwa maji, we we unabisha! Unataka kumfurahisha nani ndugu, Naomba Mungu akuguse upate kuona, huenda siku tutaongea lugha moja
 
Mimi nawashauri wazee kijijini kwetu msiba wowote unaotokea mjini, kama ajali haijahusika, wasihudhurie hata kama waliofariki ni watoto wao.Full Stop!
Wazee wetu wengi sidhani Kama wataelewa wakiambiwa hivyo
 
Watu mnapenda propaganda za kijinga sana nchi hii.
Kwahiyo Rais asiposema kuna Corona nyie hamtachukua tahadhari?
Hii nchi imejaa pimbi wengi, kwahiyo unamlaumu Rais kwa uzembe wa baba yako?
Rais kashasema watu wachukue tahadhari na waendelee kumuomba Mungu, nyie mlitakaje ili mchukue tahadhari?
Wewe ndiye pimbi na mpumbavu mkubwa, very idiot!!! Chanjo ziko wapi? Where is protective gears kule mahospitalini?? Wapi umesikia extra bajeti kununua ventilators, mitungi ya oxygen and PPE? Bunge limeisha juzi nini cha maana as emergency measures kimekuwa tabled and approved?? Pumbavu sana, kichwani mmejaza mifunza tuuu.
 
Walimwosha bila kutumia disinfenctant. Itakuwa,
Pili hawakuwa na mask au gloves,
Ama hawakufanya decontamination baada ya shughuli...
 
Kwa hiyo kama serikali ikikataa kutangaza ugonjwa kuwa upo ndio nsitumie akili zangu za kuzaliwa kuilinda nafsi yangu? Usiniite mjinga wakati nailinda nafsi yangu. Mkuu sina nguvu ya kuufungua mdomo serikali itoe tamko . Ujinga wa kuchukua tahadhali ya nafsi yangu ni bora kuliko kuifikiria National intervation. Bora ujinga wangu . Naupenda ujinga wangu kwenye kuchukua tahadhari binafsi juu ya afya yangu binafsi . Mkuu wewe mwerevu endelea kila mtu atumie nafsi yake kama alivyozaliwa nayo . Asante [emoji1431]
Kama umeshindwa kuelewa logic ya nilichoandika basi Sina haja ya kuendelea kujibizana.
 
Watu wataangamia kwa watu kushindwa kuwajibika kidogo tu
 
mgonjwa Amesha anza kuchanganyikiwa oxygen imesha goma mwenda kwenye ubongo 🙆
 
Serikali ingefunga shule hata kwa miezi miwili ingesaidia kupunguza kasi kama mwaka 2020
Nilivyofika hapa nimepuuza kusoma uzi mzima.

Kama janga la wote kwanini unataka wenzio waji Sacrifice kwaajiri yako huwoni wewe ni mbinafsi, kuna Dozen ya watu wanategemea mlo wao wakilasiku humo mashuleni wao wafe njaa wewe ukiendelea kula na kushiba.

Ningeona Hekima ungesema ipigwe TOTAL LOCKDOWN sio kikundi fulani kitaabike kwa faida ya wote.

Nipo tayari wote tufe na korona kuliko ubinafsi wa aina hii.
 
Hata wewe unaweza kuwa pimbi pia, Rais kasema tuchukue tahadhari we unatakaje tena?
Vipeperushi? Kwahiyo kama hakuna vipeperushi ndio huwezi kuchukua tahadhari? Pimbi wengi sana hata JF humu
We kenge rais katoa lini hiyo kauli kama sio jana watu wanacho laumu ni kutochukuliwa hatua toka mwanzo maana dalili zimeonekana kitambo lakini mamlaka zimekuwa zikikanusha leo hii hapa Dar daladala zinajaza watu kama kumbikumbi hivi hiyo barakoa itasaidia nn kwenye ule mbinyo lazima serikali ichukue hatua acha kujimwambafai kishamba hapa.
 
Pole mkuu,ila serikali wafunge shule za msingi na sekondari,vyuo waache,watu tunakula kupitia vyuo wakifunga hali itakua mbaya kwa baadhi yetu
Bora TZ nzima wote wafe kuliko Ubinafsi wa kipuuzi unaandika kibinafsi kabisa wafunge shule vyuo waache kwasababu mlo wako unayegemea chuo So na wanaotegemea mlo wao shule...unapoamua vita acha ubinafsi na wanaosema Shule na vyuo vifungwe nao waninafsi wengine.

Kilakitu kifunge mbali na hapo hakuna kufunga shule wala chuo tufe tu.
 
Naandika huku naumia sana.

Maisha ya mzee wangu yako hatarini sana anapumua kwa shida sana.

Chanzo cha kuumwa.
Kuna rafiki yao mzee mwenzao alifariki, wakaambiwa kuwa chanzo cha kifo cha huyo rafiki yao ni mapafu.
Kutoka hospital ya Bugando ndugu wa marehemu walipewa mwili kwenda kuzika kijijini geita bila tahadhari wakiamini kafa kwa ugonjwa wa kawaida.

Alipofikishwa huko kijijini, ndipo wazee wenzake wakawa wamejiandaa kumzika mwenzao kama ilivyo ada yao.
Jukumu la kubeba mwili kuzika, lilifanywa na wazee kama ishara ya heshima kwa mwenzao.
Miongoni mwa wazee hao! Na mzee wangu alishiriki.

Msiba ulikuwa na msongamano mkubwa kama ada na mila za vijijini.

Wazee hawa maskini ya Mungu pasipo kujua walibeba mwili bila tahadhari! Hadi atua ya mwisho ya kumzika mwenzao.

Baada ya hapo jioni mzee akanisimulia ilivyokuwa, akadai pia walibeba na jeneza liliwavujia majimaji.
Baada ya siku kadhaa wazee hawa wameanza kuumwa.
Watatu wana hali mbaya sana, na mzee wangu usiku wa kuamkia Leo kabanwa mbavu haswa! Ametumia dawa ya malimao, vitunguu, pilipili na tangawizi lakini hali si hali, kwanza kaanza kuchanganyiwa na haongei tena.
Yuko hospital kalazwa lakini hali ni mbaya sana.
Huenda serikali wangetangaza tahadhari hasa misibani haya yasingetokea.
Huenda serikali ingetangaza wazi misiba ya korona ingezikwa na vijana walivalia kinga.
Hapa najaribu kuwaza kama hali iko hivi, maambukizi yameathiri wangapi kwa uzembe wa serikali?

Hatuhitaji lockdown, lakini chamhimu tamko litoke lifike hata kijijini watu wapewe mbinu.

Imeniuma sana kwa uzembe huu mkubwa! Kama nitapoteza busara za mzee wangu, yamkini na mama yangu atakuwa kaambukizwa maana wanalala pamoja mda wote wa kuuguza.

Yamkini tungeweza kuwalinda wazee lakini watoto wa shule hawa wadogo bado ni Carrier wa kuleta homa hiyo nyumbani.
Serikali ingefunga shule hata kwa miezi miwili ingesaidia kupunguza kasi kama mwaka 2020 sambamba na kuchukua tahadhari.

Utafaa nini utajiri katikati ya misiba?

Serikali ingeweza hata kuja na mikakati, kama hawana pesa za chanjo, wangeipokea hata watu wakachomwa kwa hiari hata kwa malipo tungelipa.

Katiba imuondolee mamlaka mtu mmoja kutegemewa kutoa tamko ili kuliokoa taifa.

Inauma sana.
Mkuu umenihuzunisha sana.
Mi hii nchi kwa wakati huu siielewi kabisa inaendaje, juzi nikihudhuria Msiba Wa Mzee mmoja maarufu tu ana watoto wasomi kwelikweli ila hakukuwa na tahadhari yoyote maji tiririka ya kunawa hakuna.

Na bado wakati Wa ibada mchumgaji ni full kumsifia magu jinsi alivyoimaliza corona nchini eti ni kiongozi anaemjua Mungu,na mataifa yamengine eti wamemkubali kwa jinsi alivyoshughulika na gonjwa LA corona, mi nikajisemea moyoni conyo hawajaujua moto Wa covid 21 aka second wave.aka toleo jipya.
 
We kenge rais katoa lini hiyo kauli kama sio jana watu wanacho laumu ni kutochukuliwa hatua toka mwanzo maana dalili zimeonekana kitambo lakini mamlaka zimekuwa zikikanusha leo hii hapa Dar daladala zinajaza watu kama kumbikumbi hivi hiyo barakoa itasaidia nn kwenye ule mbinyo lazima serikali ichukue hatua acha kujimwambafai kishamba hapa.
Huyo jamaa hajitambui,Rais ametoa tamko lini, alimuona Rais kavaa barakoa lini.
 
MK254 njoo uone Sasa madhila tuliyoletewa na Chanzo Cha Matatizo, Chama Cha Mazezeta

Jameni poleni sana ila Watanzania nawaona kama mna ujuha wa kiaina (samahani ila itabidi tu), yaani mumekalia kusubiri rais aseme ndio mjue kweli corona iko kwenu huko, inapaswa mfahamu rais wenu mnaye ni wale akina baba zetu wa kitambo, namkumbuka sana marehemu baba yangu alikua wa sampuli ya rais wenu, ilikua akifanya maamuzi yaani hata mfe wa mwisho asingebadilisha, hakuwa tayari kutumia neno "sorry".

Sitegemei na sioni rasi wenu akibadilisha kauli zake hizo, hivyo mwenye akili ajijazie na kuchukua tahadhari, epuka kusongamaana kwenye midaladala, epuka misongamano ya aina yoyote, nawa mikono, vaa barakoa na mengine yaachie Mola wako, lakini leo usiniambie unakwenda kilabu kunywa pombe kisha unamgegeda changudoa halafu unasema corona umeishinda kwa maombi ilhali unatenda dhambi.
 
Back
Top Bottom