Mimi nitaendelea na msimamo wangu, kwamba mazingira ya muungano yaliyopo sasa ni muungano jina. Zanzibar wameshajitoa kwenye huu muungano kinyemela, na Tanzania bara inaendelea kuwahudumia na kuwafanya kama taifa kupe kwenye huu muungano. Ndio maana nasema wazi, katika mazingira kama haya yaliyopo, raisi wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania hapaswi kabisa kutoka Zanzibar, wala kuwa na watumishi wengi kama ilivyo sasa katika serikali ya muungano kama mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi wizarani, wakurugenzi Tamisemi nk. Kwa vitu walivyofanya Zanzibar katika kuuhujumu muungano ni lazima raisi wa Tanzania atoke Tanzania bara. Mbadala wa hili ni kuwa na serikali tatu, lazima kuwe na serikali ya Tanganyika. Hili halipaswi kuwa na mjadala tena.
Hatuna tatizo na raisi Samia, amaefanya mengi mazuri kwa nia nzuri, japo kuna makosa mengi pia. Lakini katika mazingira ya muungano yaliyopo haifai tena yeye kuendelea kuwa raisi wa Tanzania. Kwa kuwa katiba inamruhusu kugombea, jambo la busara ni yeye kujitoa kugombea uraisi wa 2025 ili kutoa nafasi kwa mtu wa Tanzania bara kuwa raisi wa Tanzania. La sivyo itabaki kuwa jukumu la kila Mtanzania bara kuhakikisha uchaguzi wa 2025 unatoa raisi kutoka Tanzania bara, bila kujali yuko chama gani cha siasa.
View attachment 3124746
Kuendelea kukubali hali kama hii kwenye mikutano ya kimataifa ni matusi kwa Watanganyika